Nape anaendelea vipi kuwa Waziri baada ya kupatikana ushahidi wa kitendo dhalili cha kuwakanyaga wanawake migongoni jimboni Mtama?

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Mheshimiwa rais Samia inashangaza kwamba unakuwa na waziri katika baraza lako mtu ambaye imedhihirika wazi kwa ushahidi wa kutosha kuwa mwaka 2015 aliona fahari kuwakanyaga akina mama waliojilaza chini huku akipita juu yao mithili ya mtu atembeaye juu ya carpet!

Itashangaza mno kama wewe mheshimiwa rais utamwacha Nape kuwa waziri baada ya kitendo chake chenye udhalilishaji mkubwa wa heshima ya wanawake, hasa ikizingatiwa kuwa wewe kama mwanamke ndio kiongozi mkuu wa nchi. Tafadhali chukua hatua stahiki, hii ni kashfa kubwa mno kwa mtu anayetakiwa kuwa kioo cha jamii, hafai kuwa katika baraza la mawaziri.

1689845758571.jpeg
 
Hizi ndo siasa chafu ...
Kuna harusi nyingi Sana za hawa watu wa kusini ..wamama wanalala chini maharusi wanapita juu Kwa kuwakanyaga....
Bottom line ni culture Yao...Nape sio WA kwanza wala sio WA mwisho....

Ajabu mnaojifanya mna maadili ..ndo mnakuwa WA kwanza kutukana watu hapa JF mkipishana Tu mawazo na mitizamo
 
Sikubaliani na Nape kwa vingi ila kama mijitu mizima na akili zao timamu imejilaza chini kwa utashi wao wenyewe ili ikanyagwe hapo kwanini alaumiwe Nape?

Wapumbavu ni hao mashangazi yaliyokosa kazi na kwenda kujilaza chini ili ikanyagwe na mpuuzi mmoja kwa jina la mila.
 
Upumbavu wakati ni utamaduni
Kuna kabila Tanzania lisilo na na tamaduni za "ajabu"?
 
Mheshimiwa rais Samia inashangaza kwamba unakuwa na waziri katika baraza lako mtu ambaye imedhihirika wazi kwa ushahidi wa kutosha kuwa mwaka 2015 aliona fahari kuwakanyaga akina mama waliojilaza chini huku akipita juu yao mithili ya mtu atembeaye juu ya carpet!

Itashangaza mno kama wewe mheshimiwa rais utamwacha Nape kuwa waziri baada ya kitendo chake chenye udhalilishaji mkubwa wa heshima ya wanawake, hasa ikizingatiwa kuwa wewe kama mwanamke ndio kiongozi mkuu wa nchi. Tafadhali chukua hatua stahiki, hii ni kashfa kubwa mno kwa mtu anayetakiwa kuwa kioo cha jamii, hafai kuwa katika baraza la mawaziri.

View attachment 2694151
Nyie UVCCM msitutoe kwenye reli kuhusu hoja za bandari. Mwacheni aliyekanyagwa mgongoni ndio akalalamike sio nyie hapo Lumumba. Sasa hivi tumestick kwenye hoja za mkataba wa kijambazi wa bandari zetu. Ni spana baada ya spana mpaka muite maji mma. Mmejimilikisha rasilimali za nchi utafikiri ni mali za familia zenu.Nyambafu!!!
 
Back
Top Bottom