Nape anaendelea vipi kuwa Waziri baada ya kupatikana ushahidi wa kitendo dhalili cha kuwakanyaga wanawake migongoni jimboni Mtama?

Nape anaendelea vipi kuwa Waziri baada ya kupatikana ushahidi wa kitendo dhalili cha kuwakanyaga wanawake migongoni jimboni Mtama?

Sikubaliani na Nape kwa vingi ila kama mijitu mizima na akili zao timamu imejilaza chini kwa utashi wao wenyewe ili ikanyagwe hapo kwanini alaumiwe Nape?

Wapumbavu ni hao mashangazi yaliyokosa kazi na kwenda kujilaza chini ili ikanyagwe na mpuuzi mmoja kwa jina la mila.
Mila za Wamakonde hizo!

Wale sio wa pumbavu ni wajinga wakielimishwa wataacha, hata kama ni mila kuna mila zingine zimepitwa na wakati.
 
Mheshimiwa rais Samia inashangaza kwamba unakuwa na waziri katika baraza lako mtu ambaye imedhihirika wazi kwa ushahidi wa kutosha kuwa mwaka 2015 aliona fahari kuwakanyaga akina mama waliojilaza chini huku akipita juu yao mithili ya mtu atembeaye juu ya carpet!

Itashangaza mno kama wewe mheshimiwa rais utamwacha Nape kuwa waziri baada ya kitendo chake chenye udhalilishaji mkubwa wa heshima ya wanawake, hasa ikizingatiwa kuwa wewe kama mwanamke ndio kiongozi mkuu wa nchi. Tafadhali chukua hatua stahiki, hii ni kashfa kubwa mno kwa mtu anayetakiwa kuwa kioo cha jamii, hafai kuwa katika baraza la mawaziri.

View attachment 2694151
Tofauti yako na Nnauye unaijua?
Unazijua tamaduni za kabila lao?
 
Aiseeehh siwezi kubali huo ujinga regardless mila zinasemaje!!
 
Upumbavu wakati ni utamaduni
Kuna kabila Tanzania lisilo na na tamaduni za "ajabu"?
Jambo lolote lisiloleta mantiki katika fikra za kawaida ni upumbavu tu.

Ukeketaji ni tamaduni kwa baadhi ya makabila lakini kimantiki ni upumbavu na unyanyasaji wa kijinsia.

Sipingi tamaduni ya mtu lakini sitosita kuuita ni upumbavu kwa mtu mzima na akili zake timamu kujilaza sakafuni ili akanyagwe kwa kisingizio cha mila.

Na hata ingekuwa ni tamaduni ya kabila langu nisingeruhusu mtu mwenye nasaba na mimi anilalie chini ili nimkanyage.

Tusihalalishe upuuzi kwa jina la mila na nasema hivi kwa upana wa jambo lenyewe la mkanyagaji na mkanyagwaji; na sio kuongelea kitendo cha Nape kama Nape.

Na hao wanaoibua hili swala kisiasa ndio wapumbavu zaidi maana kama hawakuona dosari kipindi alipofanya hilo tendo na waje kuona dosari sasa hivi kwa vile tu imekaa sawa kwao kisiasa ni ujinga.
 
Sema wapinzani kuna muda wanakuwa na weak points mpaka unajiuliza na hao kama wanastahili kupewa nafasi ya kuongoza nchi
 
Tofauti yako na Nnauye unaijua?
Unazijua tamaduni za kabila lao?
Tamaduni za kudhalilisha watu hazikubaliki. Huu sio utamaduni unaopendeza kwa watanzania. Au tuwaache na wale wakeketaji kuendelea na mambo yao kwani si utamaduni wao pia?
 
Halafu alifanya wakati wa ushindi wa ubunge mwaka 2015..imagine mtu anakuja Leo kushinikiza Samia amtoe uwaziri...imagine that
Leo hii Wajeruman wanapelekwa mahakamani kwa makosa waliyotenda mwaka 1907, watanzania tumezoea kudhalilishwa, vp wewe ni mmoja wa hao wamakonde wasiojua kudhalilishwa? Kuna watu kukeketa ni mila na desturi zao, je waachwe tu? Muwe mnafikiri kidogo.
 
Wajerumani walifanya jinai
Hao wamama wanafanya jinai
Hapo kuna jinai?

Kama wamama kudhalilishwa ...wangapi wanacheza uchi kwenye mabaa na hampigi makelele..
Au kwakuwa huko kwenye mabaa Nape hayupo?
 
Jambo lolote lisiloleta mantiki katika fikra za kawaida ni upumbavu tu.

Ukeketaji ni tamaduni kwa baadhi ya makabila lakini kimantiki ni upumbavu na unyanyasaji wa kijinsia.

Sipingi tamaduni ya mtu lakini sitosita kuuita ni upumbavu kwa mtu mzima na akili zake timamu kujilaza sakafuni ili akanyagwe kwa kisingizio cha mila.

Na hata ingekuwa ni tamaduni ya kabila langu nisingeruhusu mtu mwenye nasaba na mimi anilalie chini ili nimkanyage.

Tusihalalishe upuuzi kwa jina la mila na nasema hivi kwa upana wa jambo lenyewe la mkanyagaji na mkanyagwaji; na sio kuongelea kitendo cha Nape kama Nape.

Na hao wanaoibua hili swala kisiasa ndio wapumbavu zaidi maana kama hawakuona dosari kipindi alipofanya hilo tendo na waje kuona dosari sasa hivi kwa vile tu imekaa sawa kwao kisiasa ni ujinga.
Uthibitisho umepatikana kiasi cha kutosha sasa Nape awajibike kwa aliyowatendea watu wanyonge ni udhalilishaji mkubwa sana au wewe unaona poa tu?
 
Wajerumani walifanya jinai
Hao wamama wanafanya jinai
Hapo kuna jinai?

Kama wamama kudhalilishwa ...wangapi wanacheza uchi kwenye mabaa na hampigi makelele..
Au kwakuwa huko kwenye mabaa Nape hayupo?
Boss kumbe unamtetea Nape tu, mimi natetea akina mama wote dhidi ya dhalili hizi. Kweli wewe mwana ccm unafikiri kuwa kosa lazima liwe jinai tu! Kama hukerwi na kitendo hicho dhalili basi nawe ni mtu wa hovyo.
 
Niliona Dada Fulani hv akilalamika kuumizwa na Huyo School mate Wangu Mh Nape Moses Nnauye.
Kuwa hataki kuhudumia baada ya kupita juu ya mgongo wake na kumtegea mgongo wake.
Lakini kwanini Wafanye hvo Kwa ajili ya ulaji wa MTU Mwingine.?.
Sioni kosa la Nape.
Mambo ya siasa siyataki katika Maisha yangu
I prefer dictatorship ndo uwe mfumo wa uongozi.
Democracy Ina drama kibao na Bla Bla .
 
Back
Top Bottom