Nape ataka Akaunti ya Deni la Taifa ichunguzwe na iwekwe bayana Fedha hizo zilikopwa na kupelekwa wapi?

Nape ataka Akaunti ya Deni la Taifa ichunguzwe na iwekwe bayana Fedha hizo zilikopwa na kupelekwa wapi?

Unakopa trillion 20 ili ukanunue ndege cash hahahahaaa
 
Hili la mikopo ya kibiashara kujenga miradi mikubwa tulilisema sana hasa, kama sikosei, wakati zinakopwa pesa toka benki moja ya Uturuki kugharamia ujenzi wa SGR. But Nape ulikaa kimya, why now? Any way hatujachelewa
 
"Kwa takwimu zilizopo deni la taifa limefikia Sh.64 trilioni. Awamu ya tatu zilikopa dola bilioni 9, awamu ya nne dola bilioni 7 kwa miaka 10, awamu ya tano kwa miaka 5 zimekopwa dola bilioni 9. Naomba ufanyike ukaguzi ili tujue kilikopwa nini"- Mbunge Nape Nnauye
 
Huwezi kuuliza swali la namna hii,lazima tumuenzi sana Bwana yuuuleee.
 
Usiwaamini ccm naludia tena usiwaamini ccm ni wale wale tu
 
Anajidai kun'gata kule na kupuliza huku wakati CCM ni hiyo hiyo na yeye akiwa miongoni mwao, namuona anaropoka tu, kumsifia Samia sasa hivi wakati alimuomba msamaha Magufuli nae akaanza kumsifia badala ya kubaki na huu msimamo wake anaojidai nao sasa ni upuuzi tu.
 
Jana muheshimiwa nape kashika vichwa vingi mitandaoni baada ya kuonyesha ukopaji wa madeni awamu zote ila kilicholeta hamasa zaidi ni kuwa alijikita na awamu ya tano,je hoja za nape zinamashiko ama ni kutafuta attention ya kisiasa
 
Huyo si aliombaga msamaha kwa jiwe , sasa anahangaika nini ama ndio akili zinarudi baada ya jiwe kufa
 
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema Deni la Taifa limefikia Tsh. Trilioni 64, ambapo awamu ya tano ilikopa Dola Bilioni 9 (takribani Tsh. Trilioni 20) bila kuwa na uwazi
-
Ametaka Deni la Taifa kuchunguzwa na miradi iliyofanywa kwa mikopo katika Serikali ya Awamu ya Tano iangaliwe kama inaendana
-
Aidha, Nape ameshauri uwazi uliopo kwenye Tsh. Trilioni 1.3 za IMF alizokopa Rais Samia uendelee kwa fedha nyingine
-
"Tembeeni vifua mberee, Tanzania ni dona kantri"
 
Wachunguzeni wote Wanaolalamika KWA Sasa baada ya mwendazake kuondoka alafu rudini KWA historia zao za nyuma,mtapata picha halisi kwann wanalalamika sasa.
Nape ashukuru hata kwa huo ubunge alionao. Chuma Magufuli angeweza kumfukuza hata uanachama au kumteua mtu mwingine agombee hukk jimboni kwake. Ashukuru anao hatahuo ubunge kwani kwa u_snitch aliomfanyia Rais wa nchi angeweza hata kupotezwa.
 
Pamoja na kwamba Nape ni mnafiki, lakini kasema ukweli kuwa dhalimu alikuwa anakopa kiboya ili kusaka sifa za kijinga. Uchunguzi ufanyike ili ifahamike dhalimu alipeleka wapi hela na genge lake la sukuma gang.
Hata mbowe achunguzwe, zile posho na mishahara ya wabunge aliyokua anakata tujue imeenda wapi, maana hata ofisi hatuna.
 
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema Deni la Taifa limefikia Tsh. Trilioni 64, ambapo awamu ya tano ilikopa Dola Bilioni 9 (takribani Tsh. Trilioni 20) bila kuwa na uwazi
-
Ametaka Deni la Taifa kuchunguzwa na miradi iliyofanywa kwa mikopo katika Serikali ya Awamu ya Tano iangaliwe kama inaendana
-
Aidha, Nape ameshauri uwazi uliopo kwenye Tsh. Trilioni 1.3 za IMF alizokopa Rais Samia uendelee kwa fedha nyingine
-
Serikali ya Mama Samia imekooa Trilion 1 tu toka iingie madarakani? Aaangalie vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni cha msingi. Isije kuwa nchi ilikuwa inakopa fedha kwa ajili ya nchi nyingine. Yaani, unakuta fedha imekopwa na Tizi lakini pesa inapelekwa utusini.

Aaargggg, sijui hata nimekomenti nini sasa.
 
Jana muheshimiwa nape kashika vichwa vingi mitandaoni baada ya kuonyesha ukopaji wa madeni awamu zote ila kilicholeta hamasa zaidi ni kuwa alijikita na awamu ya tano,je hoja za nape zinamashiko ama ni kutafuta attention ya kisiasa
Ni Muhimu ila ichunguzwe mikopo ya awamu zote, sio ya JPM tu then tupewe mbivu na mbichi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anajidai kun'gata kule na kupuliza huku wakati CCM ni hiyo hiyo na yeye akiwa miongoni mwao, namuona anaropoka tu, kumsifia Samia sasa hivi wakati alimuomba msamaha Magufuli nae akaanza kumsifia badala ya kubaki na msimamo wake ni upuuzi tu.
Alimuomba msamaha kwa kosa gani??! Ulitaka asiombe msamaha halafu apotezwe na bwana yule,

Watu walishajua kuwa itafika wakati si muda mrefu atakaa pembeni atatuachia Nchi yetu, haya kiko wapi Sasa!, Tanzania Bado hipo,yeye hayupo,
na Kina January wamerudi kusukuma gurudumu la maendeleo chini Ya Samia
 
Back
Top Bottom