Nape ataka Akaunti ya Deni la Taifa ichunguzwe na iwekwe bayana Fedha hizo zilikopwa na kupelekwa wapi?

Nape ataka Akaunti ya Deni la Taifa ichunguzwe na iwekwe bayana Fedha hizo zilikopwa na kupelekwa wapi?

Nimezisikia na kuzisoma hoja za Nape ila, ukweli kuwa Nape kwa kujua au kutokujua amemuonea mzee mkapa(apumzike salama).
Nape akiwa na confidence ya Hali ya juu amesema mkapa kwa miaka 10 alikopa dola Bilioni 9.
Hii si kweli kabisa, na sijajua kwa nini mh.Nape aliamua kusema hivi.
Mkapa aliingia madarakani 1995 Deni lilikuwa ni dola bilion 7.37. na hadi anaondoka madarakani kwa mwaka wa fedha alioishia nao Deni lilikuwa ni dola Bilioni 8.4
Hivyo kwa miaka 10 mkapa alikopa dola bilion 1 tu ambayo ni sawa na trillion 2.3 ya sasa na sio bilion 9 ambayo ni sawa na trillion 20 Kama alivyosema mh.Nape.
Kutokana na mpango wa kufutiwa madeni Deni lilifutwa na kufikia dola bilion 4 mwaka 2006 mwanzoni, ila likatoka hapo na kufikia dola bilion 15 Hadi kikwete anaondoka.
Hivyo kikwete alikopa dola bilion 11 na sio Bilioni 7 Kama alivyosema Nape
Mh.Nape kwa hesabu ulizopiga unaenda kumhukumu mama Samia bila kujua, maana kwa kipindi chake Cha miezi 6 tu ameshakopa zaidi ya Trillion 4 ( 2.7 za world Bank na 1.3 za IMF).
Mh.Nape umesifia mikopo hii kwa mama, lakini jua kwa kipindi Cha miezi 6 mkopo kwa mama samia umezidi mkopo wa mkapa kwa kipindi chake cha miaka 10.
Lakini mimi sitamhukumu jiwe mwendazake, mama Samia na atayekuja. Kwa sababu;
Kipindi cha mkapa na mwanzoni mwa kikwete mfumuko wa bei ulikua mdogo sana na pesa yetu ilikuwa na thamani kwenye dola 1.
Mfano: kipindi Cha mkapa ili kujenga darasa 1 ilihitaji si zaidi ya mil 5. Hivyo akienda kukopa atakopa pesa kidogo na deni kwa sasa litaonekana dogo kipindi chake.
Sasa hivi kujenga darasa moja si chini ya mil 20, bati kipindi cha mkapa liliuzwa sh.5,000 Ila leo bati ni sh.25,000 hivyo mama Samia akienda kukopa ni lazima atakopa kingi.
Mfano mwingine rahisi tu, Kuna kipindi Cha mkapa bajeti ya nchi ilikuwa Trillion 4 tu.
Lakini sasa hivi hizi trillion 4 ukiweka kwenye barabara tu zote zimeisha kutokana na thamani ya pesa kwa sasa.
Hivyo kwa hesabu rahisi tu kwa kipindi Cha miaka 5 inayokuja mama samia atakopa hadi trillion 30(huu ni ukweli). Na atayekuja baada ya mama Samia nae atakopa zaidi ya hizo 30.
Nini kifanyike ili deni lisikue;
  • kupandisha thamani ya shilingi dhidi ya dola. mfano dola moja iwe sh.1200. na hapo Deni letu litakuwa limeshuka kwa nusu. Badala ya trillion 64 litakuwa trillion 32.
  • kupunguza mfumuko wa bei, mfano bati liwe sh.8000, cement sh.7000, nondo sh.9000.
Hayo yote yanawezekana Ila kwa serikali ambayo itakuwa na vision na watu wenye akili kubwa sana
Screenshot_20211109-092226_1.jpg
Screenshot_20211108-230301_1.jpg
 
Anajidai kun'gata kule na kupuliza huku wakati CCM ni hiyo hiyo na yeye akiwa miongoni mwao, namuona anaropoka tu, kumsifia Samia sasa hivi wakati alimuomba msamaha Magufuli nae akaanza kumsifia badala ya kubaki na msimamo wake ni upuuzi tu.
Kwahiyo asiseme. Wakisema mnalalamika, wasiposema mnalalamika. Hii nchi ya kipumbavu sana
 
Zilikopwa likajengwa Listiggler pale watu wapate umeme nafuu.... zilikopwa ijengwe SGR chap...Zilikopwa Bandari ya Dar iongezewe uwezo kwa maana ya no of berth, zilikopwa daraja la busisi lijengwe, zilikopwa meli ziwa victoria na vivuko nchi nzima viwe kazini..
Zilikopwa kujenga stand za kisasa nchi nzima, zilikopwa kujenga masoko ya kisasa nchi nzima.
Mkopaji alikopa ili miundombinu ya umeme iwe madhubuti...Mkopaji alikopa kufufua shirika la ndege na usafiri wa reli nchi nzima..

Mkopaji akasimamia mwenyewe alichokopa ili kinachokusudiwa kipatikane... Uzuri zaidi mkopaji alifocus kuspeed up uzarishaji..Uzuri wake hata mtoto mdogo anaona tafsiri sahihi ya mkopaji ni nini alichokusudia kwa Tanzania..

Mkopaji alidhamiria kuondoa kelele za umeme wa dharula kila siku na makesi yanayonufaisha Pumbavu kila kukicha, mkopaji alidhamiria tupate umeme nafuu na uwe mwingi kiasi cha kuuza nje...mkopaji alikuwa na dhamira ya kukopa leo lakini tusikope tena kesho kwa kuwekeza kwenye maeneo ambayo yatatufanya tuwe strong na strong huko mbeleni...

Bila ushabiki, mkopaji wa awamu ya tano alikuwa anajua nini anafanya inawezekana kuliko wakopaji woote huko nyuma...Pumbavu hazitaki nchi ijitegemee na tuache kuwa ombaomba ili Pumbavu na waume zao waendelee kutunyonya leo kesho, vizazi na vizazi... vibaraka na wengine wafuata upepo hawajui wanashabikia Cartel za wahuni ambazo dhumuni kuu ni kuwanyonya ndugu zao na nchi..
 
Anajidai kun'gata kule na kupuliza huku wakati CCM ni hiyo hiyo na yeye akiwa miongoni mwao, namuona anaropoka tu, kumsifia Samia sasa hivi wakati alimuomba msamaha Magufuli nae akaanza kumsifia badala ya kubaki na msimamo wake ni upuuzi tu.
Turudi kwenye point trillion 20 zimetumikaje
 
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema Deni la Taifa limefikia Tsh. Trilioni 64, ambapo awamu ya tano ilikopa Dola Bilioni 9 (takribani Tsh. Trilioni 20) bila kuwa na uwazi
-
Ametaka Deni la Taifa kuchunguzwa na miradi iliyofanywa kwa mikopo katika Serikali ya Awamu ya Tano iangaliwe kama inaendana
-
Aidha, Nape ameshauri uwazi uliopo kwenye Tsh. Trilioni 1.3 za IMF alizokopa Rais Samia uendelee kwa fedha nyingine
-
Tatizo la nchi hii ni KATIBA imemuumba Rais asiyehojiwa maamuzi na matendo yake. Hata huyu wa sasa atafanya madudu na tutaishia kumtukuza , badala ya Mungu wetu. Tatizo letu ni KATIBA
 
Alimuomba msamaha kwa kosa gani??! Ulitaka asiombe msamaha halafu apotezwe na bwana yule,

Watu walishajua kuwa itafika wakati si muda mrefu atakaa pembeni atatuachia Nchi yetu, haya kiko wapi Sasa!, Tanzania Bado hipo,yeye hayupo,
na Kina January wamerudi kusukuma gurudumu la maendeleo chini Ya Samia
Hizi akili zenu sijui mmeshikiwa na nani, yani unaona sifa kabisa nchi kuliwa na kikundi fulani cha watu?!

Kama hakuwa na kosa alienda ikulu kufanya nini na Magufuli akasema Nape aliwatuma viongozi waandamizi CCM wakamuombee msamaha, mpaka Mama Maria Nyerere alimtumia, wewe ulikuwa kijijini bado.

Naona mnatetea upuuzi, ndio maana CCM inatutawala kwa sababu ya uwepo wa vichwa vya sampuli yako.
 
Mimi sioni kama Nape anamshambulia Magufuli bali naona kama anatufumbua macho. Hebu tuchukue hoja yake tuangalie Serikali ya Magufuli ilikopa kiasi gani? Katika hizo pesa kiasi gani kilibaki bara na kiasi gani kilienda Zanzibar. Tukifanya kwa Magufuli tutakuwa tumeweka misingi ya kufanya pia kwa Samia. Tutajua kiasi gani Samia anakopa, kiasi gani kinabaki bara na kiasi gani kinaenda Zanzibar. Katika hao wawili, Magufuli hatuna la kumfanya maana yeye kitabu chake kimeshafungwa lakini kwa Samia bado tutakuwa na uwezo wa kumuondolea shilingi kwenye mshahara wake. Kwa hiyo hoja ya Nape ichakatwe itatufikisha pazuri. Lakini tukijihami kumtetea Magufuli hatutayajua ya Samia.
 
Ya Kikwete ilikopa ngapi ?Sasa mnamuonea Magufuli kwa vile hawezi kusema tena.Wewe Nape unajiona msafi wakati ni fisadi tu.Hivi Magufuli angekuwa ni Rais mstaafu na yupo hai ungetoa hayo maoni ?.Akiwa hai nyote mlimuogopa kama Ukoma. Akiwa kafa muogopeni hivyo hivyo.Idiots.
 
Kwahiyo asiseme. Wakisema mnalalamika, wasiposema mnalalamika. Hii nchi ya kipumbavu sana
Kiongozi asie na msimamo ni mpuuzi, hata aseme kitu gani ataonekana mpayukaji tu, hapo anatafuta teuzi akishaipata ataanza kusifia hata madudu ya serikali iliyopo, kumuamini mtu wa sampuli ya Nape na anayoyasema ni uzuzu.
 
Aangalie asije tembea kwa magoti kwenda kuomba msamaha pale kaburini, huo uwazi wa 1.3t uko wapi......au kwa sababu yeye yupo kwenye mgao, ukiwa mnafiki na mchumia tumbo ni shida sana......
 
Mbona hakuyasema haya wakati wa serikali husika!,siasa inaunafiki mwingi sana yule aliesema watashinda hata kwa bao la mkono sahivi huo mkono ndio unaanza kujisonta.
 
Huyo mama yenu atakuwa nakazi kubwa sana, mama kila mtu anataka afikiriwe kwenywe kanafasi fulani. Amepata Makamba, sasa naona huyu nae kakomaa kwelikweli😁
 
Kiongozi asie na msimamo ni mpuuzi, hata aseme kitu gani ataonekana mpayukaji tu, hapo anatafuta teuzi akishaipata ataanza kusifia hata madudu ya serikali iliyopo, kumuamini mtu wa sampuli ya Nape na anayoyasema ni uzuzu.
Unanzisha na vichaa mkuu, hivi NApe nae ni wakusimama kuikosoa CCM?? Kinachotafutwa hapo ni teuzi tu, mwenzie Makamba kapata kwahiyo na yeye inabidi akomae hivyo.
 
Back
Top Bottom