"Prevention is better than cure". Sikuwahi kusikia tume ya uchaguzi, viongozi wakuu wa CCM wala vyombo vya usalama vikimkaripia wala kumhoji Mh. Nape kuhusu kauli yake ya bao la mkono aliyoitoa hivi karibuni kuhusu uchaguzi wa October 2015. Hii ni kauli nzito sana isiyopaswa kuachwa ipite hivi hivi bila kutolewa tafsiri sahihi na Nape au CCM.
Uchaguzi mkuu ni chanzo kikuu cha uvunjifu wa amani duniani, pia ni chanzo kimojawapo chenye gharama kubwa kukiandaa na kukitekeleza. Bao la mkono ni tukio kwenye mpira wa miguu ambalo linaambatana na adhabu kubwa kwa aliye na waliolifanya, na mara nyingi halimo kwenye kanuni na sheria za mpira wa miguu duniani.
Iweje Nape afananishe ushindi wa CCM wa October 2015 na bao la mkono? Nape sio kichaa na CCM inafahamu hivyo pia bila shaka kuna kitu chenye ukweli alichokidhamiria.
Kinachoshangaa Tanzania na vyama vya upinzani kuna wanasheria wengi wenye uwezo wa kumvalia njuga Nape hadi atoe ufafanuzi wa kauli yake ile ambayo ina uwezo na hadhi ya kuweza kusababisha uvunjifu wa amani kama ikitekelezwa kama alivyoitamka Nape.
Sote tunafahamu kuwa Mwenyekiti wa CCM ndo Rais na Amirijeshi mkuu wetu nchini, lakini hata yeye hakusikika akimuonya Nape kuhusu kauli yake hii.
Nashauri wanasheria wote muungane dhidi ya kauli hii ovu kwenye vyombo vya sheria na taasisi mbalimbali. Kauli hii iwasilishwe rasmi kwenye tume ya uchaguzi, vyombo vya usalama, mahakamani, jumuiya ya east africa, AU, ICC, UN, EU na Marekani ili Nape akahojiwe na kueleza alichokuwa amekimaanisha kuhusu ushindi wa bao la mkono kwenye uchaguzi.
Hii itasababisha dunia nzima ione kiashiria muhimu cha uvunjivu wa amani kwenye uchaguzi wetu ujao hivyo kujiandaa na kubaini matuo yasiyofaa kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.
Haitoshi kulalama tu kwenye majukwaa ya siasa kuhusu kauli hii, nendeni hatua nyingine zaidi mbele. Wanasheria chukueni nafasi yenu kwenye jamii.