nape alipokuwa mwanza siku chache zilizopita, alitamka matamshi ya ajabu na ya kitoto sana.ni matamshi ya kichochezi ambayo hayakupaswa kutamkwa na kiongozi wa ngazi za juu wa chama,tena chama tawala.alisema,"ccm itashinda uchaguzi wa 2015 hata kwa bao la mkono."kwa maneno haya,nape anatufanye tuamini kwamba katika chaguzi zote zilizopita,ccm walishinda kwa hila na katika uchaguzi wa 2015,ccm itatumia hila tena ili kuhakikisha kwamba inashinda.hata kama ccm ilishinda kwa hila,nape hakupaswa kutamka hadharani.alipaswa kutambua athari za matamshi yake.kwa kutumia hila kushinda chaguzi, ccm inawatawala wananchi wa tanzania kinyume na matakwa yao,na kwa kweli inawatawala kwa nguvu.kwa mantiki hiyo, hakuna tofauti yeyote kati pierre nkurunzinza na ccm,na kwa kweli ccm haina uhalali wa kumnyooshea nkurunzinza kidole. Nape alipashwa kutambua kwamba maneno aliyotamka yalikuwa maneno ya kichochezi,ambayo katika serikali makini, yalipaswa kustahili adhabu kali, kwa kuwa yanaweza kuingiza nchi katika machafuko, na kwa kweli hata katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.kwa mshangao mkubwa, sijasikia akikemewa na chama chake.kwa ukimya huu, sijui tuelewe nini.kwamba katumwa na chama chake kutamka maneno yale ya kijinga?kama chama chake hakijamtuma, wananchi tungependa kuona na kusikia akikemewa kwa nguvu zote.niseme wazi,kwamba wanaoitwa viongozi wetu wamepoteza kabisa mvuto kwa wananchi wanaowaongoza kwa sababu ya tabia zao zisizokubalika.viongozi wa kitaifa wote ni lazima wawe mfano wa kuigwa na wale wanaowaongoza.inapofika mahali kama ilivyo sasa, ambapo wanaoongozwa hawana cha kujifunza kabisa kutoka kwa viongozi wao, ni hali ya kutisha sana.viongozi wetu wamepoteza moral authority kabisa.sijui tunajenga taifa la namna gani,la waovu?mungu atusaidie sana.