Nape: CCM itashinda tu uchaguzi mkuu ujao hata kwa goli la mkono

Nape: CCM itashinda tu uchaguzi mkuu ujao hata kwa goli la mkono

Nape juzi akiwa sengerema alisikika akisema kwenye mkutano wa hadhara kuwa ccm itashinda hata kwa bao la mkuno . Aliongeza kuwa ushindi ni ushindi imradi tu refari hajaona. Tafadhari naomba ufafanuzi wa haya maneno
 
eti na hii nayo ni thread! hivi huko mashuleni mlienda kufanya nini?
 
Nape juzi akiwa sengerema alisikika akisema kwenye mkutano wa hadhara kuwa ccm itashinda hata kwa bao la mkuno . Aliongeza kuwa ushindi ni ushindi imradi tu refari hajaona. Tafadhari naomba ufafanuzi wa haya maneno

Bao la mkono alimaanisha hata kwa kusaidiwa? ImageUploadedByJamiiForums1435101206.508040.jpg
 
Nape hajielewi,amebaki kuwa msemaji wa ccm huku akichorwa kwa kauli zake tata,waliomtuma wanamtega.
 
CCM ni chama kizi zaid afrika mashariki kama haujui...vyama vingi vnajfunza wiz toka ccm ktk nchi zao
 
Kwani Nape anawapenda wagombea wote, asije akapitishwa mtu akatafuta mlango wa kutokea
 
Hayo ni maneno ya Nape na si CCM ye ajiongeleshe tu amalize kampen yake kwanza naami hatosimamishwa huyo.CCM itashinda tu kihalali kabasaaa
 
Bao la mkono alimaanisha uchakachuaji kwa kuanza na

: kuweka muda mfupi wa kuandikisha BVR maeneo ambayo upinzani una nguvu

:Kuchengesha ratiba ili wanafunzi wa elimu ya juu wasipige kura as uchaguzi utawakuta wakiwa likizo while wamejiandikishia vyuoni

:Kutumia vyombo vya dola kama jeshi na polisi kuwatisha wananchi watakaojaribu kuzuia wizi wa kura

:Kuanzisha vyama muda mfupi kabla ya uchaguzi ili kugawa kura za upinzani eg ACT

:Kuwaengua wagombea wa upinzani kwa sababu ndogo ndogo ili wao wapite bila kupingwa rejea kilichotokea serikali za mitaa

:Kuwanunua wagombea wenye njaa ili wajitoe kwenye mchuano

:Kutangaza walioashindwa kwa mabavu kwa kutumia vyombo vya dola

:Kukimbia na maboksi ya kura rejea kilichotokea Segerea

Na mbinu nyingine nyiiiingi ambazo wamekuwa wakitumia kufungia magoli ya mkono,vidole na sometimes hata kiuno

Labda huyu ataeleza mbinu zingine
CC @Vuta Nkuvute
 
Mkuu nimekupata asante kwa ufafanuzi sikuwa nimeelewa vzuri
 
hizi kauli za Nape ni za kupuuzwa kabisa ,
 
Asante sana Nape kwa mafunuo haya, hakika CCM kipo madarakani kwa wizi na uchakachuaji wa kura na mabavu ya vyombo vya dola.
 
Amethibitisha kuwa wanashinda kwa rafu na uchakachuaji , ila safari hii ngoma nzito hatulali wala kuzubaa tutalinda kura na tutathamini kura ata moja ya bibi kizee
 
amethibitisha kuwa wanashinda kwa rafu na uchakachuaji , ila safari hii ngoma nzito hatulali wala kuzubaa tutalinda kura na tutathamini kura ata moja ya bibi kizee

tanzania hakujawa na uchaguzi hata mara moja, kuna uchafuzi tu
 
Siku mbili zilizopita gazeti la Mwananchi katika habari yake kuu liliandika na mimi nanukuu "CCM itashinda tu hata kwa goli la mkono" Mimi binafsi hii habari ilinistua sana kwamba huyu mtu anasimama jukwaani tena kwa kujiamini anatoa kauli kama hiyo bila woga hata kidogo. Kwa nchi yenye watu makini hili halikutakiwa kupita hivi hivi, ingekuwa ni skendo kubwa, lakini kwetu hapa limeonekana kama la kawaida.

Statement kama hiyo nilitegemea vyama vya upinzani vingekuja na kauli kali kuikemea au kulaani kwa nguvu zote, lakini nimefuatilia katika vyombo vya habari hakuna kiongozi yeyote aliyekemea. Kukaa kimya kwa watu hawa kunanitia shaka na uelewa wao wa mambo ya siasa, siasa kama shughuli nyingine inabidi ujue ni wapi pa kuchukulia point na kujenga publicity, hilo hawakulitambua na fursa imewapita.

Lakini pia kauli ya Nape inatoa taswira mbaya kwa nchi yetu, kwamba cheating katika nchi yetu imeota mizizi kiasi kwamba linaanza kuonekana kitu cha kawaida, kama hivyo ndo hivyo tutatoa wapi moral authority ya kuwaonya au kuwakemea watoto wetu wasifanye cheating katika mitihani yao kama mwanasiasa kama Nape anaweza kusimama jukwaani akashadadia wizi wa kura?

Kwa kauli hiyo ya Nape ni dhahili shahiri tunafanya uchaguzi siyo kwa nia ya dhati bali ni kuwafurahisha mataifa ya magharibi ili yaendelee kutoa misaada. wanahubiri Amani na utulivu midomoni huku chini kwa chini wanapanga mipango ya wizi wa kura, hii ni aibu kubwa na haiashirii mwisho mzuri. Ndo maana wananunua magari ya washawasha na kuajili polisi wapya kila ukifika uchaguzi.

Na vyama vya upinzani inabidi vijitambue la sivyo vitabaki upinzania mpaka yesu arudi.

Nawakilisha wanajanvi
 
Ila kama kulikua na uzi uliotoa kauli ya upinzani Kuhusu hili kama kumb zangu ziko viruzi
 
Wizi wa kura tu hana la maana....nadhani mwaka huu Upinzani walinde kura zao kwa jasho na damu hadi kieleweke
 
Tusubiri Inawezekana Wanafanya Vikao Ili Watoke Na Kauli Ya Pamoja Kama Vyama Vya Upizani
 
Back
Top Bottom