Nape: Kampuni za simu acheni kutuma ujumbe ambao mteja hajaomba, hii tabia ikome

Ipo siku nape atakuja kuwa rais wa nch HV hv
 
Malalamiko kwake ni kelele!!!

Hivi ule uzinduzi wa line moja mitandao yote uliishia wapi au walitupiga changa la macho wachote pesa
 
Pia Waache kutuunganisha huduma ambazo hatujaomba
Aisee mimi kuna siku nimewapigia voda nikawatolea uvivu. Nilikua nashangaa unakuta nna bando la data, nna bando la dakika na nna bando la sms. Cha ajabu kila nikiweka muda wa maongezi ili nifanye miamala ya simbanking nakuta hela yote imeliwa! Saa nyingine unakuta nimeweka hela dakika hiyo hiyo nikicheki balance nakuta 0.

Kuwapigia wananiambia eti nimejiunga sijui huduma ya miito, sijui whatsap status, sijui huduma gani kanitajia huduma zaidi ya 5! Wakati mimi huduma hizo kwanza sijawahi kujiunga wala siihitaji! Nikamuambia acheni ujinga wa kuunganisha watu maujinga yenu automaticaly halafu mnakata hela. Tangu siku hiyo nikiweka hela naikuta kama ilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…