beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Bungeni kuwa Serikali inaendelea kuchambua malalamiko ya matumizi ya Bundle kwenye simu.
Amefafanua, "Malalamiko kwamba kuna Bundle zinawekwa kwenye Simu, zinatumika bila Mtumiaji kuzitumia yamekuwepo, yamefikishwa Mamlaka husika na Uchambuzi umefanyika. Matokeo yanaonesha hakuna wizi uliotokea, isipokuwa kuna tatizo la matumizi ya simu za kisasa".
Ameongeza, "Matatizo hayo yamejikita kwenye maeneo mawili; 1) Hizi simu za kisasa wakati mwingine hata ukiwa hutumii kuna baadhi ya Applications zinaendelea kufanya kazi nyuma ya simu. 2) Simu hizi unaweza kuweka Bundle lako ukawasha 'Hotspot' kinachoruhusu mtu mwingine kutumia Data uliyonayo".
Kupitia Twitter Waziri Nape ameandika.
"YEYOTE ANAYEAMINI KAIBIWA KIFURUSHI KABLA HAJATUMIA AKAKUTA KIMEISHA, ALETE USHAHIDI TUTAFANYA UCHAMBUZI KWA KUTUMIA VIFAA VYA KISASA NATUTAWEKA HADHARANI KUONYESHA TATIZO LILIPO. Lakini mpaka leo malalamiko yote yaliyopokelewa tatizo limekutwa ni uelewa wa matumizi ya simu JANJA"