Hii kitu nilishawahi kuiandikia uzi hapa nakumbuka miaka miwili au mitatu iliyopita.
Na nilielezea vema ni kwa namna gani hizi simu za kisasa especially hizi cheap brand kama Tecno, Infinix,itel, na zinginezo namna zinaconsume bundle bila sisi kujua.
Niliwaelezea vema kuwa ndani ya hizi simu huwa ukishaanza kutumia baada ya kununua kuna app huwa zinaji install na kuanza kurun back ground data collection na kuzituma pale unapoweka bundle au kuwasha data.
Mimi nilitafiti sana na nilitumia mita ya simu kustudy data use. Kiwango cha bundle kilikuwa kinakwenda sawa na ujazo nilionunua ila kwa kasi isiyo ya kawaida.
Hili tatizo limeshakemewa pale South Africa na walitishia kuzikataza simu hizo kuingizwa kule kwasababu kupandikiza secret apps zinazoconsume data kwa siri kwenye simu za watu na kutumia taarifa binafsi kugenerate business information kwaajiri ya makampuni yanayotengeneza bidhaa mbali mbali.
Nimekuwa nikitrack bundle uses na kitu kilichotokea ni kuwa huwa nikipata sms ya kunambia bundle limeisha nikicheki mita ya simu nakuta inasoma bundle limesha pia kama kile kiwango cha bundle nililonunua kilivyoisha.
Mfano nikinunua 2GB then kabla sijajiunga kwanza naiset mita ya simu isome 2GB kwenye Total bundle then ninapoanza kutumia inanisomea ile ninayotumia huku ile total ikipungua kulingana na ninavyotumia .... Ikifika tu 1.9GB utaona sms inaingia bundle yako imeisha , nikirudi kwenye mita naona pia 2GB used.
So hapo ndipo nikajua simu za sasa zinakuja na apps zinazotumia data kwenye background bila sisi kujua. Na ndipo hapo shida inapoanzia kwasababu ya kutokujua tunabakia kulaumu makampuni ya simu na kuona yanatuibia ila kiukweli majizi halisi ni hizi simu in the background...... Zinakwapua data kisiri sana. Na hizo apps ni bug apps maana hazionekani zimefichwa sana.