Namuunga mkono asilimia mia moja waziri. Kuna uelewa mdogo wa watumiaji wa smart phones, hicho anachokisema ni sahihi kwa sababu binafsi kuna wakati nilihisi bundle langu linaisha bila kuelewa lina isha vipi.
Nilichofanya nili install app ya ku track all my internet usage, hii app inakuonesha kabisa una bundle lenye mb ngapi na jinsi linavyoenda likiisha. Pia hii app ilikua ina list apps zote kwenye simu ikianza ile inayotumia bundle zaidi, mfano ticktock, instagram, twiter, telegram etc.
Kwa hili nikaja kujua nini kinamaliza bundle langu. Hii app nilikuta inatumia hadi mb 12 saa nyingine wakati hata sijaifungua. Nilifanya maamuzi ya kuitoa kwenye simu yangu, tokea hapo bundle linatumika vizur.
Kwa hiyo ni kweli, hakuna anayesema anaibiwa bundle ataweza kuleta ushaidi wa hilo, sana sana tu mtu ana back ground apps zinazo run na kumaliza bundle lake na hazijui.
Sent using
Jamii Forums mobile app