Nape kutumbuliwa ni sawa, lkn kutelekezwa na dereva akiwa bado anatoa tuzo ukumbini siyo sawa

Labda dereva wake alikuwa anatania kama yeye alivyotutania
 
wewe Nape jifunze kuheshimu watu Dunia inabadilika sn
 
Dereva hawezi kuondoa bila kupewa maelekezo na wakubwa wake.pamoja na Hivyo,nape alistahili kudhalilishwa kabisa maana wakiwa na madaraka huwa hawathamini wananchi.Na kama angekuwa anapendwa na wananchi hata dereva angemwambia na siyo kumuacha
 
Ni sawa tu, sasa ushavuliwa uwaziri uendelee kusubiriwa kwa cheo gani ? huoni kwamba dereva kama angemsubiri angekua anahatarisha ajira yake.
 
Sasa wewe ulitaka gari ya Waziri imbebe mbunge mkuu? Unajua pritokali za utenguzi with immediate effect? Usitetee ujinga mkuu.
 
Ndiyo vizuri ili wajue umuhimu wa kubadili mfumo na siyo kumwacha mtu mmoja anayeitwa rais kufanya atakavyo. Huyu ni mmoja ya mawaziri ambao hawakuona umuhimu wa kukaa upande wa wananchi.
Hapa unatetea tu ujinga. Huyu waziri katumbuliwa, lakini bado anawajibika kurudi ofisini kukabidhi ofisi na mali nyingine alizokabidhiwa. Kwa hadhi yake sio sahihi kuachwa ukumbini/barabarani bila usafiri. Jamii yetu inapaswa kustaarabika na sio kuwa jamii ya kudhalilishana. Wengine pia mna wivu wa kike au wa kimasikini ukiona mtu kateleza unafirahi na kusema acha wote tule kisamvu. Pengine hutawahi kufika alipofika. Anyways, maccm yatajuana huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…