Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nchi inaendeshwa kwa matamko ya Rais pekeeSahihi kabisa
Huwa wanabadili plate no ya gari pekeeAngepelekwa eneo la karibu zaidi la makazi ya watu, ndipo atashushwa. Hata Chalamila alipotenguliwa ukuu wa mkoa, alidandia lift, akapanda kwenye noah, kurudi kwake.
Alichokifanya Dereva ni sahii , gari inakua na plate no ya waziri wa wizara husika , sasa kama waziri ametumbuliwa anapanda iyo gari kama nani? Ndo utaratibuKuna video clips zinatembea zikionesha gari ya serikali iliyo na plate namba ya waziri wa habari na mawasilno ikidondoka muda mfupi tu baada ya taarifa za kutumbuliwa kwa Nape kuwekwa mitandaoni. Wakati huo Nape ndiyo alikuwa meza kuu akigawa tuzo kama mgeni rasmi, na hata hotuba alikuwa bado hajatoa.
Hii si sawa. Hata kama alikuwa na mapungufu ktk uongozi wake ama kuna kosa kalifanya basi hakustahili kulipwa udhalilishaji huu. Huu siyo utamaduni wetu watanzania na hii si tu inamdhalilisha mhusika, bali inajenga chuki kwa ndugu, jamaa, marafiki, wananchi wa Jimbo lake na watanzania kwa ujumla dhidi ya mamlaka ya uteuzi.
Kama mtu aliteuliwa kwa heshima, akapewa majukumu fulani, basi hata siku ya kumuondoa aondolewe bila kudhalilishwa.
Uovu kama huu aliwahi kufanyiwa pia Dr. Mwigulu Nchemba kipindi cha rais kichaa. Dr. Mwigulu Nchemba alishushwa njiani akiwa safarini kuelekea Mwanza.
Tusiibomoe nchi yetu kwa tabia zetu mbaya na chuki zetu binafsi. Uongozi ni hekima
View attachment 3052842
Basi utaratibu huu uangaliwe upya, vinginevyo kuna siku waziri wa maliasili na utalii atakuja kuachwa katikati ya mbuga ya wanyama.Alichokifanya Dereva ni sahii , gari inakua na plate no ya waziri wa wizara husika , sasa kama waziri ametumbuliwa anapanda iyo gari kama nani? Ndo utaratibu