Sidhani kwani Moses Nnauye alikuwa active sana enzi za Nyerere akiwa kanali na mhamasishaji (kamisaa) wa jeshi na na baadaye akastaafu enzi za Mzee Mwinyi akiwa Brigedia, cheo alichopata baada ya Vita ya Kagera ambapo makanali wengi walipandishwa kuwa mabrigedia. Kabla ya vita tulikuwa na mbrigedi wasiozidi watano. Sasa ukifuatilia historia ya Membe, inaonyesha kuwa enzi ambazo Moses Nnauye akiwa active kwenye politics, yeye ama alikuwa ni mtu junior sana na sehemu ya muda huo ndipo alipokuwa masomoni. Ila kwa sababu ya "nepotism" inawezekana alimjua kama "mtu wa kwetu" Mtama, basi.