Nape: Membe alinisaidia kwa Rais Kikwete nikapewa u-DC

Nape: Membe alinisaidia kwa Rais Kikwete nikapewa u-DC

Kweli katiba mpya iweke wazi nafasi zote za kazi nchini ziombwe na waajiriwe watu kutokana na sifa zao. Mkapa aliweka ile tume alafu JK akaiondoa kwa kejeli kwamba nafasi za serikalini huwezi kuomba ila unachaguliwa au kuteuliwa nk mimi najua washikaji walikuwa wengi hivyo ilibidi ile tume ifutwe na mtendaji mkuu akastaafishwa
Ni kweli,na kuanzia wakati wa Kikwete ndio heshima ya ma-DC ilianza kuporomoka,nakumbuka David Kafulila(Tumbili) aliwahi kupata kesi mahakamani ya kumwambia DC mmoja kwenye jimbo lake kwamba "Ndio tatizo la raisi kuchagua DC mwenye hadhi sawa na changudoa"
 
Kumbe UONGOZI yanapeana
Ulikuwa hujui eeh! Mwenda zake alisema hawezi kumpa uongozi mtu ambaye hamfahamu vizuri, wenyewe waliokaribu na mteuaji wakiona nafasi iko wazi wanaanza kutuma vimemo.
 
Sidhani kwani Moses Nnauye alikuwa active sana enzi za Nyerere akiwa kanali na mhamasishaji (kamisaa) wa jeshi na na baadaye akastaafu enzi za Mzee Mwinyi akiwa Brigedia, cheo alichopata baada ya Vita ya Kagera ambapo makanali wengi walipandishwa kuwa mabrigedia. Kabla ya vita tulikuwa na mbrigedi wasiozidi watano. Sasa ukifuatilia historia ya Membe, inaonyesha kuwa enzi ambazo Moses Nnauye akiwa active kwenye politics, yeye ama alikuwa ni mtu junior sana na sehemu ya muda huo ndipo alipokuwa masomoni. Ila kwa sababu ya "nepotism" inawezekana alimjua kama "mtu wa kwetu" Mtama, basi.
Kama kuna aliyekuelewa ulichoandika basi naomba bani toka jf
 
Mbona ipo wazi kabisa kama ya mbuzi...Nape bila kubebwa bebwa ungekuta ni dereva bodaboda tu huko Lindi.
kuna watu wanauwezo mkubwa mara 100 zaidi yake lakini ni nobody tu hapa bongo!.
Kama ni ubodaboda Nape angeufanyia Bukumbi Mwanza
 
"Nilipokosa ubunge wa jimbo la Ubungo, Mzee Membe akanifata na kuniambia tulia kijana wangu. Mwaka 2015 nitakuachia jimbo la Mtama mimi nitakuwa namaliza muda wangu.

Kutokana na ukaribu wa Mzee Membe na Rais Kikwete nikapewa Ukuu wa Wilaya ya Masasi ambapo ni karibu na jimbo la Mtama" - Mh. Nape Nnauye akimuelezea Mh. membe.

Umejifunza ni nini hapo? Tafuta connection kwa hali na mali
Naona Nape akikomba hapa msibani
 
😆😆😆😆😅 Acha kunishambulia kwa lugha za dharau utafikiri Mimi nimesema natafuta U DC hapa,Hata hivyo Nakusamehe bure maana Mimi Ni mtu wa watu nayependa amani na watu wote
Kaka mimi wewe ndo DC wangu
Tumshukuru mama samia kwa kufungua uhuru wa kujadili na kucomment kama hivi jf
 
Katiba Mpya! Katiba Mpya! Katiba Mpya!

Tukisema tunataka Katiba Mpya mtuelewe. Hatufanyi kwa hasira wala kukurupuka.

Tunaposema tunataka Katiba Mpya, ni kwa sababu tunajua na kuipenda nchi yetu bila unafiki na maslahi binafsi au ukada.

Tunatambua na kuamini ndio njia pekee na sahihi itakayotuwezesha kutatua sehemu kubwa ya matatizo yetu kama Taifa; pia kutuwezesha kujenga misingi mathubuti ya utawala bora, uwajibikaji n chaguzi huru.

Nape amewakumbusha tu jinsi uwanja ulivyo na jinsi mchezo unavyochezwa.

Nchi yetu vye kama ubunge, ukuu wa mkoa na wilaya, ukurugenzi, ubalozi.....hata uwaziri - ni kama APENDAVYO Rais.

Vetting na "hadaa" za namna hiyo ni upuuzi na uongo; hazinaga uhalisia wowote....kigezo ni apendavyo mkuu.

Wana kauli zao husema '...ikikupendeza mh..... au ikupendeze mh....."
 
Back
Top Bottom