Point ya Nape inavitu viwili ambavyo ameongea kwa wakati mmoja ,nafikiri nape ameongea uchumi wa wanamtwara kwa kutegemea gas, sasa hapo either anaongelea shughuli za uzalishaji akiwa maana ya kuchakata na kuanza kuuza zifanyike, pili suala la gas asilia kutumika katika kama nishati ya umeme, kuhusu suala la gasi kutumika katika nishati ya umeme hili linafanyika maana kuna ujenzi kinyerezi I umeshakamilika na uliingiza kiasi cha umemem katika grid ya taifa, pia upanuzi wake wa kinyerezi I unaendelea na utakamilika mwakani, kinyerezi II pia juzi magufuli kazindua, zifuatazo kinyerezi III, na kuendelea zitaendelea kulingana na ratiba na upatikanaji wa pesa, haya ni kwa mujibu wa taariza zao serikali.
Nahisi kikubwa ambacho nape anashangaa ni kwamba mradi wa gas mbona serikali hawaufatilii, au kwa nini hauko kwenye hotuba ya waziri mkuu kama shughuli za uzalishaji kuanza na kupatikana kwa gasi ,uuzaji ndani na nje ili kuwakomboa watu wa mtwara ,lindi na watanzania kwa ujumla, hapa ndipo nape nafikiri kichwa kinamuuma, kwa kweli sio yeye tu, ni watanzania wengi, ila tuliuza kwa wawekezaji, kipindi kile kile cha awamu ya nne, pengine serikali ya awamu ya tano ifuatilie na itueleze kuna nini? mbona mradi kwa ujumla umekuwa kimya? awamu ya tano wao wamekuta mambo yalishakwisha, mikataba ilishafungwa,kinachofuata ni wawekezaji watekeleze,kwa hiyo serikali watueleze ni lini shughuli rasmi za uzalishaji zitaanza,maana wana mtwara wengi wanasubiri ili waweze kujikwamua, kwa kweli ni swali zuri na jambo jema kuuliza, hapa nakubaliana na nape.
Umeme wa gasi kuanzia phase I, II, III ...., kwa ujumla yake tutapata 2400MW+lakini hazizidi 3000MW, je kama taifa umeme wa kwa ujumla wa 3000MW unatutosha? unatufanya tulizike au tuendelee kuongeza ili tuwe na options mbalimbali na tuweze kupata umeme mwingi na kwa bei ndogo? jibu ni ndio, hivyo magufuli kwenda na Stiegler's bado ni option nzuri ukizingatia nia yake ya uchumi wa viwanda.