Nape: Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge haupo kwenye ilani, sie tulinadi mradi wa gesi. Huu tumedandia tu

Nape: Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge haupo kwenye ilani, sie tulinadi mradi wa gesi. Huu tumedandia tu

Napeee kwani kama jambo halipo kwenye ilani hamuwezi lifanya ?
mbona yapo ya kwenye ilani mengi hamkuyafanya enzi ya Kikwete ?
wapi katiba mpya ?
wapi maisha bora kwa kila mtanzania (mliahidi aise) ?
wapi mahakama ya kadhi (au mlibahatisha kuandika ) ?
kama ni lazima kila kilichopo katika ila kifanyike,basi hamasisha watu kuhusu mahakama ya mafisadi.
 
Stiegler gorge hata kipindi cha JK iliongelewa sema haikuanza kutekelezwa tu, nadhani Nnape angeuliza tu kama suala la gas limeachwa au vipi? Maana kama tumeachana na mradi wa gas kweli basi tunafanya makosa makubwa sana. Ni bora tungemaliza mradi wa gas kwanza then tuanze na stieglers gorge. Tunahitaji umeme wa kutosha hasa if we real want an industrialised Tanzania.
Kweli kabisa mkuu ila Nape kabeza kama vile stiegler gorge hauna maana.

Ila nahisi gesi inafanana kama iptl mkuu.
 
Mhe. Nape labda ana hoja. Ni kweli wawekezaji wanaikimbia Mikoa ya kusini. Juzi nimeshuhudia kupitia luninga kuwa kwa sasa mahoteli ya Mtwara yanajaza kwa asilimia 15% mpaka 20% kinyume na hapo mwanzo. Pili hoja ya Stieglers Gorge nayo ina mashiko. Nadhani CCM ina ilani na kama mradi huo haupo kwenye ilani ana sababu zote za kuhoji.
Ilani ya CCM ni msaafu au biblia mkuu?

Nape kakurupuka tu. Ukimsikiliza sana utaona chuki na visirani, unawezaje kusema Waziri mkuu unatoka kusini basi apendelee kusini,kwani Waziri mkuu ni wa kusini au JMT ?
 
Dikteta ni yule ambae amebadili katiba ya Chadema na kufanya nafasi ya mwenyekiti wa chama haina ukomo wa uongozi. Dikteta niyule ambae pesa za ruzuku za chadema anajilipa madeni ambayo hayaeleweki na hayana mwisho.Dikteta ni yule nafasi za Viti maalumu anazigawa kwa rushwa ya ngono.
Kwahiyo nyerere alipokuwa mwenyekiti wa ccm kwa miaka 24 alikuwa dikiteta ?
 
Nimemsikiliza aiseeee, @Nape Nnauye ndio leo wa kulia? Ndio wakuiponda serikali yake? Iwe funzo Kwa akina Mwigulu na wengine. Ni suala la muda tu
Iwe funzo kwa akina Mwigulu au iwe funzo kwetu unafiki wa wanasiasa?
 
Nape siku zote huwa hana akili na hata huo ubunge aliupata kwa shida sana. 2020 tutaona kama atanusa hata uenyekiti wa mtaa atapata. Kichwani tu ni ziro sijui hata hao wananchi wa mtama waliwezaje kumpa ubunge.
 
Ilani tu haiwezi kuwa dira tosha ya utekelezaji wa miradi nchini - lzm tunapomaliza uchaguzi huwa tunafanya mapitio ya Ilani za vyama vingine vya siasa na kuchomoa chomoa kile chenye maslahi kwa taifa na wananchi.
 
Nape NNAUYE, atulie Serikali ya CCM ifanye kazi - akiwa waziri wa habari alipenda ingewezekana hata mitandao ya kijamii izimwe, Bunge lizimwe nk nk

Yako mambo hayamo ktk Ilani ila tunayafanya kwa sbb ya hali ya kisiasa - suala la wapinzani kuwapa nafasi CCM (Kitila, Anna, Mrema nk) ili kujenga mshikamano wa kitaifa.

YEYE akiwa kamati kuu kwa nini alikuba (Christopher CHIZA - Buyungu, Wasira STEPHEN - Bunda, Kagasheki HAMIS - Bukoba) majina yalirudije wakati alifahamu uchafu wao?? Leo ndiyo anainadi kanda ya kusini kwa kutumia Gas??
 
Hasira za kutimuliwa uwaziri !
Utawezaje kuwa na sera ya viwanda bila umeme wa uhakika?
Nape, binadamu tumeumbwa kukubali mabadiliko, hatuwezi Kuchelewesha maendeleo kisa ilani!
Wewe na JK wakati wenu mlikuwa mnatekeleza ilani ipi ?
Au na dili ilikuwa ilani
 
Kwahiyo nyerere alipokuwa mwenyekiti wa ccm kwa miaka 24 alikuwa dikiteta ?

Kwa hiyo mbowe ndio nyerere wa chagadema, hahahahahahaha hapo nimekuelewa mkuu. Muasisi wa chama mpaka aamue. Kumbe ndio maana amekiuza na aliyemuuzia kamsifia Mkuu Magu na hakuna anayeweza kumuuliza kitu hahahahaha nacheka kichaga
 
Nape anakitu anaogopa kukisema direct kwamba kwa sasa nchi inaongozwa kwa vision ya mtu mmoja sio ilani au lolote lile!
Na kwa vyovyote vile kwani kuna ubaya gani kupanua wigo wa nishati mbona Kinyerezi I - V zinaendelea vizuri tu! Na kama hakuikataa vision Tanzania ya viwanda anatarajia ifikiwe vipi kwa megawati 1440 za sasa? Stieglers gorge ni utundu na ujasiri wenye tija!
 
Hasira za kutimuliwa uwaziri !
Utawezaje kuwa na sera ya viwanda bila umeme wa uhakika?
Nape, binadamu tumeumbwa kukubali mabadiliko, hatuwezi Kuchelewesha maendeleo kisa ilani!
Wewe na JK wakati wenu mlikuwa mnatekeleza ilani ipi ?
Au na dili ilikuwa ilani
Mh,basi jamani msiende ndani sana...
 
Tumechoka na zilipendwa hizo! Nyimbo zilizochuja unatuwekea hapa? Nenda nawe ukaliwe upewe viti maalumu!
Sawa kabisa, si haya aliyoeleza yalishaisha toka kitambo! Katiba ilishabadilishwa sasa mwisho wa uongozi wa chama unajulikana, si ndiyo?

Ruzuku sikuhizi inafika hadi kwenye matawi.

Hakuna ushahidi wa upendeleo kwenye uteuzi wa nyadhifa mbalimbali ikiwemo ubunge wa viti maalumu.

Haya ni zilipendwa.
 
Waziri wa zamani na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) ameishangaa Serikali kuweka nguvu nyingi kwenye mradi wa umeme wa Stigler’s George ambao haupo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 na kuachana na umeme wa gesi ambao waliunadi wakati wa kampeni.
Nionavyo mm hata bunge halina kazi awamu hii, mambo yanakwenda hata bila bunge.
 
Huna hoja, hata gesi inaweza kutoa umeme mwingi kama uwekezaji ukiongezwa kwenye gesi.
 
Nadhani sio yote aliyoongea ni ya hovyo, tuchukue yale mazuri tuyafanyie kazi na yale ya hovyo tuyaache. Kwanza ni vyema tukajua je ni kweli issue ya gas imewekwa pembeni? If not then ajibiwe tu. Je issue ya mbaazi na korosho ni kweli? If not ajibiwe tu. Ila kusema stieglers gorge haikuwepo kwenye ilani so isitekelezwe hapo ni kupitoka, rais akitekeleza ya kwenye ilani na akaenda extra mile inapendeza so long as ni kwa maswali mapana ya nchi. Na pia kama kuna miradi ambayo ni white elephant projects akaamua kuiacha hata kama ipo ndani ya ilani sio kosa kabisa, kosa ni pale kama ataacha miradi yenye tija na maslahi mapana kwa taifa na kutekeleza miradi isitokuwepo kwenye ilani na haina tija wala maslahi mapana kwa taifa.
I get it, ni vzr kwa uongozi wowote kukubali critics, lakini this guy hajawahi kuwa na critical thinker. In fact, sijui kama ana huwezi huo wa kufikiri. Anatafuta popularity kupitia matamko ya kwenye majukwaa. And to some point anadhani yeye na CCM are synonyms. Policies za maendeleo lazima ziwe dynamic. Frankly, this guy hana chembe ya positive criticism. He is more driven na chuki, kuliko maslahi ya nchi.
 
Back
Top Bottom