Nape, muda mwingi unaotumia kumsema vibaya Hayati Magufuli ungeutumia kupigania Tozo za Intaneti na Miamala

Nape ni aina ya mwanasiasa ambaye mimi binafsi hunivutia mara chache sana; akiwa na madaraka hujisahau kirahisi na kuwa jeuri. Akiwa nje ya madaraka hujitambua na kuwa mnyenyekevu. Pamoja na huo udhaifu kwa hili analolalamikiwa kuwa anamsema vibaya marehemu namuelewa; anayo sababu ya kutosha kufanya hivyo. Anayesemwa na Nape pamoja na raia wengine wengi siyo marehemu wa kawaida tu; huyu ni marehemu aliyeaminiwa na kukabidhiwa mamlaka ya umma. Nape alindwe na aachwe atumie uhuru wake kwa kuyasema yote ambayo hakuyapenda; wenye mazuri ya kuyasema nao wafanye hivyo hivyo! Hii ndiyo njia pekee ya yeye Nape kujifaraji nafsi yake na kujipunguzia machungu ya ule udhalilishaji wa kutembezwa kwa miguu mbele ya kamera kwenda mbele ya "mtukufu" kufanya toba na kuomba msahamaha wa dhambi.

Akiwa kiongozi wa kuchaguliwa na watu, kibinadamu siyo jambo rahisi yeye Nape binafsi pamoja na wananchi waliomwamini na kumchagua kusahau na kusamehe huo udhalilishaji aliofanyiwa. Mambo mengine ni ya kishetani na hayasahauliki wala kusameheka; kutaka kufanya hivyo kirahisi ni sawa sawa na kufungamana na shetani na kazi zake zote na mambo yake. Nchi hii inahitaji kuweka utaratibu wa kitaifa wa kutafakari, kutubu na kuomba msamaha kwa uovu wote wa kipindi kile cha giza. Hili siyo jambo la kuwataka watu mmoja mmoja wanaotoa hisia zao za maumivu hadharani kunyamaza kwa sababu tu aliyewaumiza kwa kutumia mamlaka ya umma amefariki. Isitoshe, mamlaka hayo yaliyotumika kuumiza raia sasa yamekabidhiwa mtu mwingine! Kwani kuna tatizo gani kama mamlaka hayo yakitumika sasa kwa hekima kuwaomba radhi raia ambao wameumizwa kwa matumizu mabaya ya hayo mamlaka?
Tumefurahi kujua kuwa kumbe na Wewe pia huna / hauna kabisa Akili kama Yeye.
 
Baba wa Watu ameshalala tokea mwaka Juzi (2021) lakini cha Kushangaza (tena ukiwa Mtoto wa Kiume) Wewe kila Siku ni Kumsengenya mara Kumfumbia Mafumbo tabia ambazo tumezoea kuona zikifanya na Dada zetu (Watoto wa Kike)

In short Unaboa japo wenye akili tunajua unafanya hivyo (Kumsema vibaya Hayati Magufuli) Kimkakati kabisa ili umfurahishe boss wako (Rais Samia) ambaye hakuupenda Uongozi wa aliyekuwa boss wake japo Kimaamuzi walikuwa wakifanya pamoja kwa mujibu wa Katiba ili asifikirie Kukutumbua katika huo uwaziri wako ambao mpaka sasa GENTAMYCINE nikiambiwa nikupe Marks za Kiutendaji nikikupa nyingi basi ni 10% tu ila 90% umeharibu na hufai kuwa hapo.

Hovyoooooo......!!!!!!
Halafu eti wametuwekea awe mgeni rasmi pasaka tamasha la dini
Pumbavu sana,hatuendi.
 
Vibao vya makaazi vimeishia wapi
Majina ya mitaa inaandikwa kwa kutumia mikaa navimbao vya kuchonga vikishikiliwa na fito ambazo si muda mchwa watazuaghusha.mbwembwe za helicopter zimeishia wapi.malizeni hiyo kazi iliyoishia HEWANI.
 
Nape ni aina ya mwanasiasa ambaye mimi binafsi hunivutia mara chache sana; akiwa na madaraka hujisahau kirahisi na kuwa jeuri. Akiwa nje ya madaraka hujitambua na kuwa mnyenyekevu. Pamoja na huo udhaifu kwa hili analolalamikiwa kuwa anamsema vibaya marehemu namuelewa; anayo sababu ya kutosha kufanya hivyo. Anayesemwa na Nape pamoja na raia wengine wengi siyo marehemu wa kawaida tu; huyu ni marehemu aliyeaminiwa na kukabidhiwa mamlaka ya umma. Nape alindwe na aachwe atumie uhuru wake kwa kuyasema yote ambayo hakuyapenda; wenye mazuri ya kuyasema nao wafanye hivyo hivyo! Hii ndiyo njia pekee ya yeye Nape kujifaraji nafsi yake na kujipunguzia machungu ya ule udhalilishaji wa kutembezwa kwa miguu mbele ya kamera kwenda mbele ya "mtukufu" kufanya toba na kuomba msahamaha wa dhambi.

Akiwa kiongozi wa kuchaguliwa na watu, kibinadamu siyo jambo rahisi yeye Nape binafsi pamoja na wananchi waliomwamini na kumchagua kusahau na kusamehe huo udhalilishaji aliofanyiwa. Mambo mengine ni ya kishetani na hayasahauliki wala kusameheka; kutaka kufanya hivyo kirahisi ni sawa sawa na kufungamana na shetani na kazi zake zote na mambo yake. Nchi hii inahitaji kuweka utaratibu wa kitaifa wa kutafakari, kutubu na kuomba msamaha kwa uovu wote wa kipindi kile cha giza. Hili siyo jambo la kuwataka watu mmoja mmoja wanaotoa hisia zao za maumivu hadharani kunyamaza kwa sababu tu aliyewaumiza kwa kutumia mamlaka ya umma amefariki. Isitoshe, mamlaka hayo yaliyotumika kuumiza raia sasa yamekabidhiwa mtu mwingine! Kwani kuna tatizo gani kama mamlaka hayo yakitumika sasa kwa hekima kuwaomba radhi raia ambao wameumizwa kwa matumizu mabaya ya hayo mamlaka?
Wewe ni pimbi na umeandika upumbavu
 
Wewe ni pimbi na umeandika upumbavu
Sawa na asante kwa matusi yako. Sikulaumu kwa sababu wako wengi walioambukizwa hiyo roho ya kishetani ya kutamani kila wakati kunyamazisha watu wengine badala ya kutoa hoja. Kama tulivyofanya kipindi kile cha giza, licha ya kutukuzwa na pengine kuombewa na wanaoitwa viongozi wa dini, nasi tutaendelea kumuomba Mungu aliye hai nanye bila shaka atatujibu kama ambavyo amekuwa akitujibu siku zote. Mungu atawalipeni kwa mawazo, kauli na matendo yenu.
 
Baba wa Watu ameshalala tokea mwaka Juzi (2021) lakini cha Kushangaza (tena ukiwa Mtoto wa Kiume) Wewe kila Siku ni Kumsengenya mara Kumfumbia Mafumbo tabia ambazo tumezoea kuona zikifanya na Dada zetu (Watoto wa Kike)

In short Unaboa japo wenye akili tunajua unafanya hivyo (Kumsema vibaya Hayati Magufuli) Kimkakati kabisa ili umfurahishe boss wako (Rais Samia) ambaye hakuupenda Uongozi wa aliyekuwa boss wake japo Kimaamuzi walikuwa wakifanya pamoja kwa mujibu wa Katiba ili asifikirie Kukutumbua katika huo uwaziri wako ambao mpaka sasa GENTAMYCINE nikiambiwa nikupe Marks za Kiutendaji nikikupa nyingi basi ni 10% tu ila 90% umeharibu na hufai kuwa hapo.

Hovyoooooo......!!!!!!
mie sikuwahi kumpenda magu japo tulikuwa marafiki na nilimfamu kwa long time but huyu nape sipendi kumsema magu yeye afanye kazi tu
 
Baba wa Watu ameshalala tokea mwaka Juzi (2021) lakini cha Kushangaza (tena ukiwa Mtoto wa Kiume) Wewe kila Siku ni Kumsengenya mara Kumfumbia Mafumbo tabia ambazo tumezoea kuona zikifanya na Dada zetu (Watoto wa Kike)

In short Unaboa japo wenye akili tunajua unafanya hivyo (Kumsema vibaya Hayati Magufuli) Kimkakati kabisa ili umfurahishe boss wako (Rais Samia) ambaye hakuupenda Uongozi wa aliyekuwa boss wake japo Kimaamuzi walikuwa wakifanya pamoja kwa mujibu wa Katiba ili asifikirie Kukutumbua katika huo uwaziri wako ambao mpaka sasa GENTAMYCINE nikiambiwa nikupe Marks za Kiutendaji nikikupa nyingi basi ni 10% tu ila 90% umeharibu na hufai kuwa hapo.

Hovyoooooo......!!!!!!
Huyo hakuwa baba wa watu bali kiongozi wa nchi. Raia waliovutiwa na uongozi wake hawaachi kumkumbuka, kumuimbia mapambio na hata kumtukuza. Kadhalika walioumizwa na uongozi wake nao wanayo haki kumlaani na kuendelea kuyaweka bayana maovu yake ambayo mengi haikuwezekana kuweka hadharani bila mtu kuhatarisha maisha yake. Wakati hayuko ndiyo wakati salama kuzungumzia maovu yake yote. Matarajio ya raia wema wa nchi hii ni kwamba tafiti zitafanyika na majarida na vitabu vitaandikwa juu ya kipindi kile cha giza ili vizazi vyetu viweze kujua jinsi nchi iliyopata kujiamini sana kisiasa kwa miaka zaidi ya 50 ilivyoharibika na kuwa mfano mbaya ndani ya ya miaka isiyozidi 5!
 
Inawezekana maana vita ya madawa ilikuwa inaonekana ya wateja wake wa siku nyingi na alijua nguvu yao ndiyo maana akaona bora zali la kufukuzwa uwaziri lakini siyo kutofautiana na hao jamaa. Ndiyo maana Nape siyo msafi na hana credibility ya kujilinganisha na Dkt Magufuli, ila bado ni kijana anaweza kubadilika na akaeleweka sema wenye nchi aliowatukania mtu ambaye alikufa mikononi mwao lazima watakuwa walishazika file lake succh that he will never amount to anything, ni suala la muda
Kuwaza ipo siku huyo popoma atabadilika ni sawa na kufukuza upepo.. mi nilishamtoa maanani namdharau na sitawahi kumwani asilani abadani. Ni aina ya watu wajinga wasio na sitaha hata chembe.
 
Kwani wewe Ndiyo Unachagua Viongozi. @
Tangu lini nyie mkachaguliwa? Hii Nchi alichaguliwa Nyerere na Mwinyi peke yao. Wengine nyie mnachaguliwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Huyo hakuwa baba wa watu bali kiongozi wa nchi. Raia waliovutiwa na uongozi wake hawaachi kumkumbuka, kumuimbia mapambio na hata kumtukuza. Kadhalika walioumizwa na uongozi wake nao wanayo haki kumlaani na kuendelea kuyaweka bayana maovu yake ambayo mengi haikuwezekana kuweka hadharani bila mtu kuhatarisha maisha yake. Wakati hayuko ndiyo wakati salama kuzungumzia maovu yake yote. Matarajio ya raia wema wa nchi hii ni kwamba tafiti zitafanyika na majarida na vitabu vitaandikwa juu ya kipindi kile cha giza ili vizazi vyetu viweze kujua jinsi nchi iliyopata kujiamini sana kisiasa kwa miaka zaidi ya 50 ilivyoharibika na kuwa mfano mbaya ndani ya ya miaka isiyozidi 5!
Kwenye uongozi wa nchi iliyokuwa na matakataka kama hii wakati JPM anaingia kulikuwa hamna namna zaidi ya watu kuumia baada ya kutuumiza kwa miongo mingi.

Ukiwasikiliza wote waliodai kuumizwa bibi yenu aliwarudisha wote, akiamini walionewa! Leo hii report ya CAG inasema nini kuhusu infration kwenye kila mradi, bibi hajawaita wapumbavu na anataka watolewe? Hajawaambia mawaziri wake wamsaidie wakati anajua na wao wanahusika kwenye wizi? Leo Nape anawatetea wafanyabiashara kuongeza faida mara 100 na kuwaponda wananchi kwa gharama kubwa za mawasiliano.

Internet is all most everything nowdays unapoipaisha unatarajia watu wafanyeje? Kumsema Magu vibaya haiondoi upungufu wa Nape... na hatuta muhesabia mazuri ya uongozi wake... eti enzi zake alitusaidia kumsema Marehemu Magufuri mpaka jambo fulani likapata unafuu... ukikumbuka Mwl alisema "Mnaacha ya maana mnashika ya kijinga" alikuwa anawaambia watu wa aina yenu na waziri wako.
 
Haya mambo bhana basi tu., mfano tu yeye kungekuwepo na Mwamba anamsemasema saana Mzee wake Nauye angejisikiaje.
Mzee Nauye hakuwa malaika; watu wanajua kama kuna watu aliowakosea basi hayo yalitokea kwa ubinadamu wake wa kawaida na siyo kwa roho mbaya ya kishetani. Roho ya kishetani ni ile inayomfanya mtu mwenye mamlaka au uwezo mwingine kuumiza watu wengine ili kufurahisha nafsi yake mwenyewe yeye na kujijengea utukufu kwa wafuasi wake!
 
Na wewe huu mda mwingi unaoutumia kumtetea dictator kwa Swala lililowazi kazi kwamba nape kidogo apigwe bastola ungeutumia kutafuta pesa ili uishi vizuri tofauti na Sasa unaugulia ingekuwa vizuri sana
Yeye hana shida ya kutafuta pesa; alishapata ya kutosha kipindi kile cha giza ambapo hata CAG alifukuzwa kwa kutekeleza wajibu wake wa kikatiba ikiwa ni pamoja na kufichua upotevu na matumizi mabaya ya rasimali za umma chini ya uongozi wa kizalendo na wenye uchungu na nchi hii!
 
Sijawahi kusikia popote duniani Waziri anaenda field kuchunguza tukio la jinai

Hata Lyatonga Mrema hajawahi

Ni aina ya kisasi kilicho kwenye Tabia ni kama ugonjwa vile!
Nape anafikiri maneno yake yanafurahisha wakubwa hasa Rais. Amefanikiwa kufanya kazi hadi jikoni lakini hajui harufu za vyakula.

Anachofanya kwenye macho ya elites ni uhuni na wanamchora tu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom