Nape na ombi la CAG kukagua mikopo; kuna watu wamepanic!

Huwa nawashangaa sana watu wakisema na kujimwambafai Magufuli kafanya hiki, Magufuli kafanya hiki. Ingekuwa kazi ya urais ni kuchukua mamikopo na kujenga madalaja basi Marais wote wangefanya hivyo. Urais una takiwa kuangalia mambo mengi sana na yote yaende kwa pamoja.

Awamo ya tano tuliingizwa chaka na itachukua miaka mingi sana kufix athari iliyosababaisha
 
Hata mimi shabiki kindakindaki wa Hayati Rais Magufuli naunga mkono hoja ya CAG kukagua pesa zote za mikopo za Awamu ya Tano na matumizi yake. Na katika kufanya good comparison CAG pia akague na za Awamu ya Nne na Tatu na matumizi yake ili tuone zipi zilileta tija zaidi. Kukagua za Awamu moja tu utakuwa ni usanii.
 
Jamani kagueni kote tena muanzie awamu ya kwanza mpaka ya sasa ya 6.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa Jf mmoja wao ni jingalao
Nae ameanza kutaka ukaguzi pia ufanyike kwenye matumzi ya fedha za ziara ya Kinana na Nape.
Yaani ni full migambo wanaruka na kukanyagana!!!
Kuna waliofaidika na JPM kwa kula cha juu kikubwa!
Utawasikia wakienda kwa waganga ili kuzuia uchunguzi🙂🤣🤣
 
Ikinyesha ndo tutajua inapovuja. Acha inyeshe sasa.
 
CAG anafanya kazi yake kila mwaka kwa ufanisi mkubwa.
JPM alipoanza kukafiliwa tu, kwa vile anajua anakwapua fedha za umma , akamfukuza CAG Assad, hilo kila mtu anajua.
Ni wewe tuna akili yako kung'amua kuwa tulikuwa na kiongozi si mwamiifu.
 
CAG anafanya kazi yake kila mwaka kwa ufanisi mkubwa.
JPM alipoanza kukafiliwa tu, kwa vile anajua anakwapua fedha za umma , akamfukuza CAG Assad, hilo kila mtu anajua.
Ni wewe tuna akili yako kung'amua kuwa tulikuwa na kiongozi si mwamiifu.
Kwahiyo hoja yako ni ipi? Kwamba CAG akague pesa za mkopo kipindi cha Magufuli ambazo aliishazikagua ila asikague za Awamu zingine kwasababu aliishazikagua?
 
Naunga mkono hoja, lakini asikague kulinganisha tija. Tukianza kulinganisha tija na wizi hapo hakuna ukaguzi tena.
 
Mbaya zaidi alikopa ili kujenga zaidi sana kule kwao.
Uwanja Chato, Busisi na SGR kwenda kwao wakati hata kuikarabati TAZARA hatukuwahi kumsikia.
Asulubiwe!!
 
Magroup yoote ya whatsap ccm wamepigwa na ganzi

Hawaamini hiki kinachoendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…