Nape na ombi la CAG kukagua mikopo; kuna watu wamepanic!

Nafikiri serikali iliyopo Sasa ni ile ile iliyokuwepo, kuanzia Rais, Makamu na waziri Mkuu.

Ni mwendo wa kupiga tu
Yaani leo umeme badala walete wa uhakika tunaambiwa wamesaini na Mhindi $30m
Upigaji umerudi bila woga
Ule wa kwanza tulikuwa tunaambiwa tunajenga kwa hela zetu ila mmh
Lakini sasa mkataba unapita na huna la kufanya
 
Kama uchunguzi ukifanywa na Bunge kwa kuamriwa hivyo, basi utakuwa uchunguzi dedicated kwa hiyo mikopo tu ya Awamu ya Tano, kama alivyoomba Nape!
Kumbuka CAG alifungishwa virago alipohoji Trillioni 1.5 zimeenda wapi!
Bila maelekezo hawezi kufanya?
 
Yaani huko mtafurumua madudu ya ajabu ya mwendazake - acheni tufunike kombe.
 
Bila maelekezo hawezi kufanya?
CAG anaweza na atafanya hiyo, lakini ni in general terms kama anavyofanya ukaguzi kila mwaka.

Lakini kwa msimamo huo wa kufanya Annual Audit ya CAG, hoja ya jinsi mikopo ya Awamu ya Tano ilivyotumika inaweza kupotelea kwenye mafaili.
 
Zimbabwe kuna waziri alikumbwa na tuhuma za rushwa, na kwakua ilimhusisha mkuu, walipomfuata kumhoji akasema "go on but I will not sink alone" aliishia kubadilishwa wizara tu.

Nnachotaka kusema ni kwamba, hata ukifanyika ukaguzi madudu yakabainika, hakuna wa kumuwajibisha mwenzake, wengi sio wasafi. Watu ni walewale waliokuwepo awamu iliyopita.

Nnachojiuliza sasa, Nnnnape anafanya haya yote sasa hivi kwa uzalendo au kwa vile hakunufaika na ufisadi?
Kwahiyo kama kuna kigogo ana tuhuma za wizi tukae kimya kwakuwa hakuna hatua zitakazochukuliwa?
Huoni kama kitendo tu cha kufanya uchunguzi kitatufanya angalau kujua uadirifu wa viongozi tulionao ?
Inawezekana kweli Nape amesema hayo kwavile hakuwa na mahusiano mazuri na utawala uliopita, kwahiyo hilo limfunge mdomo hata akinusa harufu ya ufisadi ?
 
Chief, sipo kabisa kwenye kutoa maamuzi au kupendekeza nini kifanyike, lakini ni haki yangu kutoa maoni. Chukulia haya kama maoni yangu na mtazamo wangu.

Uchunguzi/ ukaguzi unahitaji pesa. Na kama CAG anafanya kazi zake kwa ufanisi, alitakiwa awe ameshabaini tuhuma za huyu Nnnnnape.

Ni kupoteza rasirimali za taifa kwa vitu ambavyo mnajua havitatufikisha popote zaidi ya kutumika kisiasa tu.
 
Kuna waliofaidika na JPM kwa kula cha juu kikubwa!
Utawasikia wakienda kwa waganga ili kuzuia uchunguzi🙂[emoji1787][emoji1787]
Watu hawa kila siku hapa Jf walituamisha kuwa utawala wa awamu ya 5 ulikuwa msafi, usiokuwa tuhuma, kwamba kila senti ya serikali imefanya kilichokusudiwa, lakini cha kushangaza wanaogopa uchunguzi .
Kuna nini?
 
CAG anafanya kazi yake kila mwaka kwa ufanisi mkubwa.
JPM alipoanza kukafiliwa tu, kwa vile anajua anakwapua fedha za umma , akamfukuza CAG Assad, hilo kila mtu anajua.
Ni wewe tuna akili yako kung'amua kuwa tulikuwa na kiongozi si mwamiifu.
Umenena vema mkuu.
Kumbuka wakati mwamba yupo madarakani ilikuwa ukimkosoa tu unaambiwa ulikuwa fisadi sasa unanyooshwa.

Leo hawataki hata uchunguzi wa CAG.
Tulieni mnyooshwe.
 
CAG kimsingi amekubali kukagua fedha za mikopo iliyoingiwa na serikali ya Awamu ya 5.

CAG Kichere amesha sema anasubiri maelekezo tu.

Kutokana na mijadala, hata humu JF, kuna watu wamepanic.

Kisirisiri wengi wanajua frdha zilivyoliwa, mitambo nyeti imenunuliwa st inflated prices, na hakuna aliyeuliza.

Miradi haikuhakikiwa na bunge, hilo linajulikana.

Nenda Tegeta A, Mbweni na kwingineko, majumba yalipaa kama uyoga, na ni watu fulani tu.

Nape umetonesha kidonda.
Siyo ku-panic; bali kudadisi mantiki ya pendekezo au ushauri huo. Nape alikuwa Mbunge tangu wakati wa JPM. Kwa nini hakutumia wadhifa wake huo wakati ule kupendekeza anayoyasema hivi sasa, akasubiri hadi leo kuja kufanya hivyo? Hapo hapo, alikwenda kumwomba msamaha JPM na hakuwa na la kumtonya Rais kuhusu udhalimu anaoufahamu ukifanyika. Hiyo ndiyo shaka yetu kwamba ni uchumia tumbo ndio unamtuma kufanya hivyo. Siyo shauri la ku-panic.
 
Chief, sipo kabisa kwenye kutoa maamuzi au kupendekeza nini kifanyike, lakini ni haki yangu kutoa maoni. Chukulia haya kama maoni yangu na mtazamo wangu.

Uchunguzi/ ukaguzi unahitaji pesa. Na kama CAG anafanya kazi zake kwa ufanisi, alitakiwa awe ameshabaini tuhuma za huyu Nnnnnape.

Ni kupoteza rasirimali za taifa kwa vitu ambavyo mnajua havitatufikisha popote zaidi ya kutumika kisiasa tu.
Usikute wewe ndiyo mwizi mwenyewe mliokula mikopo ☹☹☹
 
Zimbabwe kuna waziri alikumbwa na tuhuma za rushwa, na kwakua ilimhusisha mkuu, walipomfuata kumhoji akasema "go on but I will not sink alone" aliishia kubadilishwa wizara tu.

Nnachotaka kusema ni kwamba, hata ukifanyika ukaguzi madudu yakabainika, hakuna wa kumuwajibisha mwenzake, wengi sio wasafi. Watu ni walewale waliokuwepo awamu iliyopita.

Nnachojiuliza sasa, Nnnnape anafanya haya yote sasa hivi kwa uzalendo au kwa vile hakunufaika na ufisadi?
Shushia na maji baridi mkuu jiji lamoto hili
 
Siyo ku-panic; bali kudadisi mantiki ya pendekezo au ushauri huo. Nape alikuwa Mbunge tangu wakati wa JPM. Kwa nini hakutumia wadhifa wake huo wakati ule kupendekeza anayoyasema hivi sasa, akasubiri hadi leo kuja kufanya hivyo? Hapo hapo, alikwenda kumwomba msamaha JPM na hakuwa na la kumtonya Rais kuhusu udhalimu anaoufahamu ukifanyika. Hiyo ndiyo shaka yetu kwamba ni uchumia tumbo ndio unamtuma kufanya hivyo. Siyo shauri la ku-panic.
Umepata muda wa kuandika utoto humu. Yaani tunajadili nani kasema badala ya ngapi zimeibwa na nani ili zirudishwe? Kwa hiyo wewe mwizi akikupa tips za wezi wenzie walivyokuibia utaacha kufanyia kazi kwa sababu naye ni mwizi?
 
Zimbabwe kuna waziri alikumbwa na tuhuma za rushwa, na kwakua ilimhusisha mkuu, walipomfuata kumhoji akasema "go on but I will not sink alone" aliishia kubadilishwa wizara tu.

Nnachotaka kusema ni kwamba, hata ukifanyika ukaguzi madudu yakabainika, hakuna wa kumuwajibisha mwenzake, wengi sio wasafi. Watu ni walewale waliokuwepo awamu iliyopita.

Nnachojiuliza sasa, Nnnnape anafanya haya yote sasa hivi kwa uzalendo au kwa vile hakunufaika na ufisadi?
Mbombo ngafu
 
Naunga mkono hoja. Isiwe Awamu ya tano tu. Ianze awamu ya nne uone watu. watakavyoumbuka
Awamu ya nne ufisadi ulifanyika na kila mmoja ameuona.
Maana awamu hiyo serikali iliendesha mambo yake hadharani, ufisadi ulisemwa Bungeni, CAG amekagua, baadhi ya Mawaziri walipoteza kazi, magazeti yameandika na wananchi wamesikia.

Lakini ufisadi wa awamu ya tano hamtaki tiujue maana mtawala wa wakati huo mlimfananishwa na Masihi.
 
Umepata muda wa kuandika utoto humu. Yaani tunajadili nani kasema badala ya ngapi zimeibwa na nani ili zirudishwe? Kwa hiyo wewe mwizi akikupa tips za wezi wenzie walivyokuibia utaacha kufanyia kazi kwa sababu naye ni mwizi?
Unasema tunajadili 'ngapi zimeibiwa' na si 'nani kasema'. Labda hayo ndiyo mawazo yako lakini kwenye uzi mhusika hakuna hata mstari mmoja unaojadili 'ngapi zimeibiwa'. Badala yake uzi unamtaja Nape kwamba ndiye aliyesema ninayoyajibu. Sasa ni 'utoto' upi ambao nimeuzungumzia? Wewe ndiye unayeunganisha mawazo yako katika uzi unaozungumzia mambo tofauti kabisa. Anzisha uzi wako kwa yale yaliyomo moyoni mwako. Usilete mambo ya 'kitoto' kuunganisha mawazo yako na nyuzi zinazozungumzia mambo tofauti kabisa.
 
Usikute wewe ndiyo mwizi mwenyewe mliokula mikopo ☹☹☹

Naheshimu maoni yako mkuu, uchunguzi ufanyike na ikibainika nimeiba, sheria ichukue mkondo wake.

Kama watu walibeba pesa kwa mifuko, wengine wakawekewa kwa akaunt na wakasema pesa ya mboga na hawajaguswa hadi leo unafikiri kuna maajabu yatafanyika safari hii?

Huyo jamaa kwanza anatakiwa awe shahidi namba moja, inaonekana anafaham jinsi pesa ilivyotafunwa.
 
Back
Top Bottom