Nape na ombi la CAG kukagua mikopo; kuna watu wamepanic!

Nape na ombi la CAG kukagua mikopo; kuna watu wamepanic!

Awamu ya nne ufisadi ulifanyika na kila mmoja ameuona.
Maana awamu hiyo serikali iliendesha mambo yake hadharani, ufisadi ulisemwa Bungeni, CAG amekagua, baadhi ya Mawaziri walipoteza kazi, magazeti yameandika na wananchi wamesikia.

Lakini ufisadi wa awamu ya tano hauatakiwi ujulikane maana mtawala wa wakati huo alifananishwa na Masihi.
Awamu ya 5 hakuna ufisadi wewe! Hela imetumika hata kipofu anaona
 
Huwa nawashangaa sana watu wakisema na kujimwambafai Magufuli kafanya hiki, Magufuli kafanya hiki. Ingekuwa kazi ya urais ni kuchukua mamikopo na kujenga madalaja basi Marais wote wangefanya hivyo. Urais una takiwa kuangalia mambo mengi sana na yote yaende kwa pamoja.

Awamo ya tano tuliingizwa chaka na itachukua miaka mingi sana kufix athari iliyosababaisha
Yule alikuwa Rais wa Dar Dodoma na Chato.mikoa mingine hakuwa na habar nayo kabisa.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri serikali iliyopo Sasa ni ile ile iliyokuwepo, kuanzia Rais, Makamu na waziri Mkuu.
hapana, hufikiri sawa sawa

hizo ni serikali mbilo tofauti

iliyopita ni awamu ya tano, na hii ni awamu ya sita ijapo sura ni zilezile tu, nia na miongozo ya awamu hizi ni tofauti
 
Siyo ku-panic; bali kudadisi mantiki ya pendekezo au ushauri huo. Nape alikuwa Mbunge tangu wakati wa JPM. Kwa nini hakutumia wadhifa wake huo wakati ule kupendekeza anayoyasema hivi sasa, akasubiri hadi leo kuja kufanya hivyo? Hapo hapo, alikwenda kumwomba msamaha JPM na hakuwa na la kumtonya Rais kuhusu udhalimu anaoufahamu ukifanyika. Hiyo ndiyo shaka yetu kwamba ni uchumia tumbo ndio unamtuma kufanya hivyo. Siyo shauri la ku-panic.
Mbona mnakosa uelewa.
Kichaa mwenye panga unaongea naye vipi kwa mfano!
 
CAG kimsingi amekubali kukagua fedha za mikopo iliyoingiwa na serikali ya Awamu ya 5.

CAG Kichere amesha sema anasubiri maelekezo tu.

Kutokana na mijadala, hata humu JF, kuna watu wamepanic.

Kisirisiri wengi wanajua frdha zilivyoliwa, mitambo nyeti imenunuliwa st inflated prices, na hakuna aliyeuliza.

Miradi haikuhakikiwa na bunge, hilo linajulikana.

Nenda Tegeta A, Mbweni na kwingineko, majumba yalipaa kama uyoga, na ni watu fulani tu.

Nape umetonesha kidonda.
Naamini taarifa ya ukaguzi itakaliwa kama zingine. Ile ya BOT ilishatolewa hadharani ?!
 
Nani anaogopa ukaguzi. Naomba kwa mola wakague na wafanye public ili wabaya wa JPM waumbuke
Wabaya wa JPM ni akina nani?
Ukimkosoa kiongozi wako unakuwa na ubaya naye?
Nyi ndiyo mlimpotosha.
Hakuna mkamilifu, ila Mwenyezi Mungu. Milishangilia kila alichofanya mkasahau kwamba yeye ni mwana wa Adamu kama wengine.
Na sifa moja ya binadamu ni kukosea
 
Chief hangaya nae anahusika kwa sababu alikuwa namba 2 ya awamu ya 5.

endeleeni kufukua makaburi mkidhani mnamuabisha au kumkomoa mtu wakati MNAJIDHALILISHA wenyewe.

mpaka kigogo2014 tushamjua ni nani na nani ,nyie endeleeni tu.

NB: Legacy ya Magufuli hamuwezi kuifuta kamwe,mambo yake wanaoneka kwa macho na Watanzania walimuelewa sasa nyinyi kazaneni na majungu halafu msifanye kazi za kuonekana TUONANE 2025.
 
Zimbabwe kuna waziri alikumbwa na tuhuma za rushwa, na kwakua ilimhusisha mkuu, walipomfuata kumhoji akasema "go on but I will not sink alone" aliishia kubadilishwa wizara tu.

Nnachotaka kusema ni kwamba, hata ukifanyika ukaguzi madudu yakabainika, hakuna wa kumuwajibisha mwenzake, wengi sio wasafi. Watu ni walewale waliokuwepo awamu iliyopita.

Nnachojiuliza sasa, Nnnnape anafanya haya yote sasa hivi kwa uzalendo au kwa vile hakunufaika na ufisadi?
Kunskuwaga na mbuzi wa kafata kwenye haya mambo.

Lowasa alitolewa kafara kwenye Richmond.

Tibaijuka na Ngereja wakatolewa kafara kwenye Escrow.

Kitwnga akayolewa kafara kwenye... The list goes on.
 
Endeleeni kusubiria mkuu. Zile alizohoji CAG aliyepita mliwahi kujua zimeishia wapi?
Watanzania ni wepesi sana kuwaamini viongozi wao. Kuna watu hawaamini kabisa kuwa awamu ya 5 kuna watu wamepigia cha kufa mtu. Kwa wao kushindwa kuelezea zile 1.5 Trillion na baadaye kumtoa CAG ni ushahidi tosha.

Kama Jamaa aliweza kuchukua tausi wa Ikulu na kujimilikisha kweupe mchana what else do you need to believe.....!!
 
Umenena vema mkuu.
Kumbuka wakati mwamba yupo madarakani ilikuwa ukimkosoa tu unaambiwa ulikuwa fisadi sasa unanyooshwa.

Leo hawataki hata uchunguzi wa CAG.
Tulieni mnyooshwe.
Jamaa alikuwa na visasi na roho ambayo ni kama nyoka swila mwenye sumu na anakugonga bila sababu.
Wengi wamekufa chini ya utawala wake.
 
Jambo ni muendelezo wa upotevu wa hela za wananchi . Ukaguzi utafanyika aidha majibu ya report yawe public na hatua zisichukuliwe kwa watakao bainika ama report itakuwa mali ya waliomtum kukagua tu na hatua hazitachukuliwa kwa watakaobainika kula hela za wananchi. Hivyo kama wanajua hiyo report haitakuwa na athari yoyote ni bora wakaacha
 
CAG kimsingi amekubali kukagua fedha za mikopo iliyoingiwa na serikali ya Awamu ya 5.

CAG Kichere amesha sema anasubiri maelekezo tu.

Kutokana na mijadala, hata humu JF, kuna watu wamepanic.

Kisirisiri wengi wanajua frdha zilivyoliwa, mitambo nyeti imenunuliwa st inflated prices, na hakuna aliyeuliza.

Miradi haikuhakikiwa na bunge, hilo linajulikana.

Nenda Tegeta A, Mbweni na kwingineko, majumba yalipaa kama uyoga, na ni watu fulani tu.

Nape umetonesha kidonda.
Ukaguzi mihimu sana walituaminisha kwamba miradi yote inajengwa kwa kodi za ndani ss watuambie zile walizokopa zimeeda wap tunahitaji majibu
 
Back
Top Bottom