Nape na ombi la CAG kukagua mikopo; kuna watu wamepanic!

Nape na ombi la CAG kukagua mikopo; kuna watu wamepanic!

CAG kimsingi amekubali kukagua fedha za mikopo iliyoingiwa na serikali ya Awamu ya 5.

CAG Kichere amesha sema anasubiri maelekezo tu.

Kutokana na mijadala, hata humu JF, kuna watu wamepanic.

Kisirisiri wengi wanajua frdha zilivyoliwa, mitambo nyeti imenunuliwa st inflated prices, na hakuna aliyeuliza.

Miradi haikuhakikiwa na bunge, hilo linajulikana.

Nenda Tegeta A, Mbweni na kwingineko, majumba yalipaa kama uyoga, na ni watu fulani tu.

Nape umetonesha kidonda.
Wewe muongo!!!!!!!! Mbweni ni magofu tu. Sema awamu ya nne
 
Kuna kitu hawa wanasiasa lazima wakijue, kwanza hakuna mtanzania wakudanganywa kwa miaka hii, pili dunia imebadirika sana kiasi kwamba tunazo kumbukumbu zote na yote yaliyofanyika kabla ya Late John Joseph Pombe na yanayoendelea sasa.

Tusianze na lolote lile kati ya Richmond au Dowans either wanajua kila kitu or wanatafuta kumchafua mtu kwa kile alichofanya kuonekana was fashisti than those still living, hii ni nchi yetu sote siyo ya wazi na wanyang'anyi flani.

Huyo CAG tutamuomba arudi kuanzia nyuma wkt mmea ndiyo umeamishiwa eneo lingine ukiwa bado haujazoea aridhi mpya.
Naunga mkono hoja. Isiwe Awamu ya tano tu. Ianze awamu ya nne uone watu. watakavyoumbuka
 
Zimbabwe kuna waziri alikumbwa na tuhuma za rushwa, na kwakua ilimhusisha mkuu, walipomfuata kumhoji akasema "go on but I will not sink alone" aliishia kubadilishwa wizara tu.

Nnachotaka kusema ni kwamba, hata ukifanyika ukaguzi madudu yakabainika, hakuna wa kumuwajibisha mwenzake, wengi sio wasafi. Watu ni walewale waliokuwepo awamu iliyopita.

Nnachojiuliza sasa, Nnnnape anafanya haya yote sasa hivi kwa uzalendo au kwa vile hakunufaika na ufisadi?
Ni kama unamsema Dr.Mpango aliyekuwa pale wizarani. Hiki ndio sababu kubwa ya kina Dotto kuhakishwa wizara tu na Bashiru kupunguziwa ulaji
 
Kuna waliofaidika na JPM kwa kula cha juu kikubwa!
Utawasikia wakienda kwa waganga ili kuzuia uchunguzi🙂🤣🤣
Mbegese yaani hayati vile alivyokata ile budget ya ukaguzi mwaka Juzi, hakuna mkaguzi anafagilia ule uzombi...ni kwamba jamaa watachambuliwa zaidi ya karanga!!!
 
Huo uchunguzi ukishafanyika ikagunduoika kuna watu waliharibu hao wahusika watachukuliwa hatua au watafichwa kama ile ripoti ya fedha zilizochotwa BOT Magufuli alipofariki?

Huyu Nape naamini kabisa anapiga hizo kelele kwa malengo yake binafsi kisiasa ili akamate nyumbu wake, lakini anazijua vizuri tabia za chama chake kuwalinda wahalifu, anajua hakuna watakachofanywa hizi kelele zake ni upepo tu utapita.
Pia anasahau kuwa Mama naye alikuwepo kwenye system.
 
Huo uchunguzi ukishafanyika ikagunduoika kuna watu waliharibu hao wahusika watachukuliwa hatua au watafichwa kama ile ripoti ya fedha zilizochotwa BOT Magufuli alipofariki?

Huyu Nape naamini kabisa anapiga hizo kelele kwa malengo yake binafsi kisiasa ili akamate nyumbu wake, lakini anazijua vizuri tabia za chama chake kuwalinda wahalifu, anajua hakuna watakachofanywa hizi kelele zake ni upepo tu utapita.
Usililojua nape sio mtu ni taasisi kwaio io ni meseji imetumwa upande wa pili
 
Zimbabwe kuna waziri alikumbwa na tuhuma za rushwa, na kwakua ilimhusisha mkuu, walipomfuata kumhoji akasema "go on but I will not sink alone" aliishia kubadilishwa wizara tu.

Nnachotaka kusema ni kwamba, hata ukifanyika ukaguzi madudu yakabainika, hakuna wa kumuwajibisha mwenzake, wengi sio wasafi. Watu ni walewale waliokuwepo awamu iliyopita.

Nnachojiuliza sasa, Nnnnape anafanya haya yote sasa hivi kwa uzalendo au kwa vile hakunufaika na ufisadi?
Mkuu ni Mkwere, prince na Membe wamemtuma abwatuke
 
Huyo CAG Kichere naye kwa nini asubiri maelekezo? Katba imeshatoa maelekezo tayari
Kama uchunguzi ukifanywa na Bunge kwa kuamriwa hivyo, basi utakuwa uchunguzi dedicated kwa hiyo mikopo tu ya Awamu ya Tano, kama alivyoomba Nape!
Kumbuka CAG alifungishwa virago alipohoji Trillioni 1.5 zimeenda wapi!
 
Awamu ya 5 si tulikua tunaongozwa na mzalendo, kiongozi wa malaika,mh. 'mungu' Kama Kabudi alivyomuita?Madudu yanatokea wapi Sasa?
Hivi wewe na akili yako ulimuona JPM anaweza kuficha hela hata Billion moja wewe? Azifiche wapi? Huelewi jinsi walivyokuwa wanamuwinda kumuumbua? Aipeleke benki ipi? Angalikuwa ni JK sema huyo ni mjanja tangu awamu ya pili na Barick yake.
 
Hoja yake ina mashiko? Tuanzie hapo.
Mashiko sana,
Kwa hiyo ukaguzi ufanyike au usifanyike?

Kwanza nakubali kabisa hoja hiyo ina mashiko, na pia ukaguzi huo ufanyike. Lakini je, unadhani kwa mazingira yaliyopo utafanyika? Ni sawa na mbwa anabweka, halafu ukimfuata anakimbia, au mwanasiasa kama Nape kwenda kwenye jukwaa la siasa na kuongea hayo. Inakuwa ni kutaka tu kusikika kuwa yupo, lakini in reality hata yeye anajua hilo halitafanyika, ila anajua atakumbukwa na kuzungumzwa kwa kuongea hivyo na pengine ataitwa mezani.
Kumbuka walio fanya hayo ndio waliopo serikalini kwa sasa tena kwenye nafasi kubwa. Hizo ni siasa tu.
 
Awamu hiyo kuna watu walipiga hela za kufuru
Sijui nilikuwa wapi
 
Back
Top Bottom