KERO Nape Nnauye afungia mtandao wa Clubhouse, haupatikani Tanzania bila VPN

KERO Nape Nnauye afungia mtandao wa Clubhouse, haupatikani Tanzania bila VPN

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wanawalinda dhidi ya nani? Mwaka juzi tundulissu alipoporwa kura 87%/13% akakuamrisheni mhamie barabarani yeye akahania Ulaya mbona hukuenda barabarani, mbona hatukuona mitutu? Nenda Kenya wanaume hawaogopi mitutu.

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
Wanasingizia mitutu tu wakati hata kufanya migomo tu hawawezi.
 
Samia anataka kuonekana mwanademokrasia lakini kumbe kaficha fimbo ya kuichapa hiyo demokrasia
 
FpCDQUvXEAsWUTO
 
....naongeza....Nape, Tundu Lissu, Mbowe na Waliominywa mirija wako sambamba katika kueneza uwongo na upotoshaji uliojaa chuki binafsi.

Nape kama kiranja wa habari Nchini ameachia Wananchi, pamoja na Familia ya Magufuli kufanyiwa Ugaidi pasipo hata n kuwa washiriki wa aina yeyote na hayo wanayodai walifanyiwa na Hayat Rais.

Ugaidi huu ni hatari kwa afya ya jamii kwa ujumla. lakini pamoja na Nape kujua hayo, ameachia vyombo vinavyoeneza habari hizo za unyanyasaji, ukimbari na yote yanayofanana nayo ilimradi tu wapate kulipiza kisasi.... waendelee bila ya Serikali kutoa tamko, kwa nini? Je ni kwa sababu tu Hayat Rais hakumwachia avimbe kwa bao lake la mkono, au kwa sababu hakuachia nadharia inayojengeka/iliyojengwa kuhusu nani haswa aliyehusika katika lile tukio? pamoja na CHADEMA kutengeneza mazingira za kuichafua Serikali?

Hakika sijui ni nini haswa kilichopeleka mtandao huo kutopatikana, na hivyo basi, siwezi dai hata kwa sumni kama mada inasimama.

Ila naweza sema kuwa, kama mada inasimama na taarifa zake basi hiyo itatosha mimi kusema ...anajali zaidi Nguvu za dola,(power) anajali zaidi tumbo lake(maslahi binafsi) pamoja na kukumbatia uhasama hasi ulioelekezwa kwa Wananchi na Familia ya Hayat Rais hususan mjane wake na watoro wake....kwa visasi vyake....na vile vya watajwa juu na vilevile kwa sababu anajua kudondoka kwa CCM ndio utakuwa mwisho wa Legacy ya NNauye.

Nape atuwekee filter ya maudhui ya upotoshaji(mis-information) maudhui ya ukimbari na unyanyasaji(dis-information) aweze kuokoa Vijana wa Kesho.

Kama kiranja Mkuu wa Habari atujuze hapa, kwani upo uwezekano ana vibaraka wake humu jamvini. Watujuzee! Kulikoni Club House?
Suala la Jiwe kuhusika katika shambulio la Lissu hiyo iko wazi na circumstantial evidences zote zinaonyesha kuwa kulikuwa na mkono wa serikali otherwise mkono wa chuma uliokuwa ukiiburuza nchi wakati wa awamu ya tano wangeshikwa wengi kuanzia polisi waliopaswa kuwa lindoni, majirani waliokuwa majumbani muda ule wa shambulio, wapangaji wa ratiba ya ulinzi hata viongozi kwani hata nyumba aliyokuwa akiishi Lissu same yard alikuwa akiishi waziri na geti huwa na polisi 24/7 strangely geti lilikuwa wazi na polisi wa zamu was no where to be seen vilevile gate la opposite alikuwa akiishi the then naibu spika Tulia na polisi walilinda 24/7 lakini muda wa shambulio hawakuwepo na hakuna aliyehojiwa kuhusu hilo.
CCTV cameras kung'olewa baada ya shambulio, nani angethubuti kama si serikali yenyewe?
CCTV camera footages polisi wanazo? Si kila kitu kiko wazi kwenye hizo footages?
Magu alikuwa akimlinda nani kwa kutokuweka wazi yote hayo mtu aliyependa publicity kiasi kile?
Hakuwa akijilinda mwenyewe? Je si kwamba ukimya wa serikali ni kwamba wanajilinda wenyewe kukwepa kuipaka matope dola pamoja na chama tawala?
Wengine(ambao hawakuhusika lakini ni vigogo serikalini) wameamua kunawa mikono wasijihusishe na yale ambayo hawakushiriki hiyo wamemuachia muhusika hilo gunia la 'mavi'.

Ingekuwa ndiyo CHADEMA wametengeneza mazingira hayo serikali ya Jiwe ingeliweka wazi muda uleule, na kama haingekuwa imehusika ingekubali lile wazo la kushirikisha FBI au MI6 ya Scotland Yard ili wahusika waumbuke na serikali iwe imejisafisha.
Jiwe alihusika kupanga na kuratibu na kama Lissu angekufa CHADEMA wangebebeshwa hilo gunia la 'mavi' kwa bahati mbaya(kwa Jiwe) hakufa na anaujua ukweli kwani alisharipoti kwenye vyombo vya dolakuwa anafuatiliwa na polisi hawakuchua hatua yoyote wakati hata namba za gari walipatiwa.
 
WaTz hawana cha maana wanachojadili huko , wacha Nape afungie tu wanajadili upupu mtupu.
Mkuu mm naungana na ww, Watanzania kwakweli wanashangaza sana,haya uliyoyasema nayaona ata kwenye Magroup yetu ya kutafta ugali huku mtaani....Watu wanaongea mambo ya kijinga sana wanaleta mapicha ya uchi na kujadiliana kuhusu kulewa tu....walio na uwezo wanapiga picha mpaka vitandani kwao wanakolala ili kutishiana kisa gep la maisha....Wanashindwa kujadili mambo ya msingi kabsaaa.
 
Nape strikes again.

Ukishaonja kula nyama za watu, kamwe hutoacha.

Yuleyule aliyetuondolea bunge live wakati huo akiwa waziri wa habari kipindi cha utawala wa Magufuli, Leo tena akiwa na dhamana hiyohiyo ya Waziri wa habari ameufungia kimyakimya mtandao maarufu wa Clubhouse.

Mtandao wa Clubhouse, ni mtandao ambapo watu popote pale walipo duniani huingia kujadiliana vitu mbalimbali kwa Sauti. Kupitia mtandao huu watu hujadili mada mbalimbali za maisha yao, ikiwemo uchumi, mambo ya kijamii, siasa n.k Nape mwenyewe ashaalikwa katika mada mojawapo kujadili ishu za anwani makazi.

Kutokana na elimu ya kuwaamsha watu na maarifa makubwa ambayo watanzania wamekuwa wakipata kupitia mtandao huo, serikali ya CCM imeona ni tishio kwao. Sasa Nape kama kawaida yake kaufungia mtandao huu ili Watanzania waendelee kuwa gizani.

Nape alipofungia bunge live wananchi walimlaani sana, baadae alipowekwa nje ya madaraka na JPM alikiri kuwa anajuta kushiriki maamuzi yale ya kufungia bunge Live. Leo Nape karudi madarakani kafungia tena mtandao wa Clubhouse ili Watanzania wasiweze kucongregate na kujadili mambo muhimu ya nchi yao.

Tukumbuke Nape huyuhuyu ndo alikuwa kinara wa kutetea sheria kandamizi ya vyombo vya habari wakati alipokuwa waziri wa habari kipindi cha JPM.

Tunamtaka Nape na TCRA, wafungulie mara moja mtandao wa clubhouse. Haiwezekani Rais Samia anasema kuwa anataka kuifungua nchi, na uhuru wa maoni uwepo, na kukosoa utawala wake ruksa, halafu anakuja Waziri kimyakimya bila kuutarifu Umma anafungia mitandao.

Kwa hivi sasa bila kuwasha VPN huwezi kuupata mtandao huu kwa sababu Nape Nnauye kaufungia.

Huyu Nape anajisahau sana, hii mitandao anayoiona ni mibaya ndiyo hiyohiyo iliyokuwa sauti ya pekee kumtetea kipindi kile katolewa bunduki njenje. Hivi huwa hawajifunzi kitu hawa?
VPN tunazo kipindi kirefu tangu enzi za jiwe alipofunga mitandao kisa uchaguzi
 
Back
Top Bottom