Nape Nnauye amjibu Mangula, ni Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo

Nape Nnauye amjibu Mangula, ni Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo

Nape atulie, hana hadhi wala sifa za kuhoji hoja za mwenyekiti wake.

Nape ameshajulikana ni mtu anaetawaliwa na njaa kuliko kitu chochote. Sasa anajaribu kujionyesha kwa samia ili angalau akumbukwe.

Nape's integrity is compromised, he has no moral authority to question or advise anything kwa sababu ameonyesha kwamba he is working for his stomach.

Makamu Mwenyekiti amesema Bagamoyo haikuahidiwa Bandari, iliahidiwa gati, shida iko wapi?
Mtukufu Rais anataka kuwapa bandari kamili.
 
Tatizo vitu vingi vinafichwa na uongo ni mwingi

Ukweli kwao mwiko
Nawashangaa waandishi wa habari ambao huwa wanatafuta habari mke kamuuwa mmewe
Badala ya kuomba mahojiano na wahusika
Tuwe na utaratibu wa kuhoji live badala ya kujificha nyuma ya Twitter na insta
 
Sio kiLa anayeomba samahani Ana Nia ya dhati wengine bado wanna chuki .
 
Salaam Wakuu,

Baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula kuzungumzia Bandari ya Bagamoyo kwamba haipo kwenye ilani, Mbunge wa Mtama Moses Nnauye(CCM) ameibuka na kusema kwamba kuna miladi mingi imetekelezwa ambago haikuwa kwenye ilani.

Mangula alisema anashangaa huu mjadala wa Bandari ya Bagamoyo unatokea wapi kwa kuwa mradi huo haupo. Mangula kasema hakuna haja ya watu kupotosha wananchi,” Mangula akizungumza na Gazeti la Uhuru ameeleza kwamba kilichoahidiwa ni ujenzi wa gati ya Bagamoyo.

“Ipo miradi ya maboresho ya bandari, lakini kwa upande wa Bagamoyo kilichopitishwa ni ujenzi wa gati, sio bandari,” amesema Mangula.

Baada ya kauli hiyo, Moses Nape Nnauye ikamlizimu aandike kwenye Mtandao wa kijamii kwamba sio kila miradi inayotekelezwa ipo kwenye ilani.

Nape kaandika hivi:

Nini Mtazamo wako wewe MwanaJF? Kwamba Serikali itekeleze yaliyopo kwenye ilani tu au iangalia vipaumbele vya wananchi?

Pia soma: Makamu mwenyekiti CCM, Mzee Mangula: Bagamoyo tuliahidi kujenga gati sio Bandari
Kuna shida kati ya bi mkubwa na gazeti la uhuru.. Na ishu ilianzia kwenye urais kipindi cha pili
 
Ni hatari sana eti kuzunguka nchi nzima kuitangaza Ilani yako ili uchaguliwe kumbe ni danganya toto. Hii ni hatari sana! Kama Ilani inashindwa kudumu kwa miaka 5, hii ni zaidi ya hatari. Inamaanisha .P W Boatha ni ukweli maneno ya aliyekuwa Rais wa Afrika kusini aliyesema- Mtu mweusi plan yake ni ya siku moja tu, na ya keshokutwa yatajulikana kesho kutwa. Du, hapa ndipo Nape anapotueleza kuwa CCM fikra zake haziwezi kuplan kwa miaka 5.

Kwa kawaida vitu vya dharura ndio hubadilika, kwa Nape ni amka na uje na wazo jipya kila kukicha - Populist! Makosa ni makosa hata kama yalifanyika toka kwa baba wa Taifa aka Mazoea...Tusihalalishe. Inawezekana hii ndio sababu ya kuwa hapa tulipo baada ya miaka 60 toka mkoloni atuachie nchi yetu aka tupate uhuru.

Jamani, kama hiki chama hakiwezi kuplan kwa miaka 5, kitaweza kweli kuwa na plan ya miaka 10, 15, 20........... Kama hivyo ndivyo, samahani nitakopa neno la Mh Rais "Nonsens" kuwa kuisoma Ilani ya uchaguzi ya CCM ni NONSENS.

M/ mwenye kiti Mangula yupo sahihi 100%, kama tunahitaji kutekeleza vipaumbele vya miaka 5 (2020-2025)wananchi walivyoiingiza CCM madarakani kwa bajeti yetu Finyu ya max 1.9 trilion kwa mwezi. Vipaumbele ndio kila kitu, leo yaliyoelezwa kwenye kilimo yamesahaulika kabisa na yalisahaulika vile vile (2015-2020). Hii inamaanisha miaka 10 bila kilimo, sigusii sakata la kilimo cha miwa/sukari.... Ah acha tu Pole waziri wa kilimo Profesa Mkenda - Pesa yako inakwenda Bagamoyo/Bandari....
Kwani uliambiwa bandari ya bagamoyo mradi wa serikali wana funds project. Mradi wa Bagamoyo port ni wa mwekezaji sio kama SGR au Bwawa la Nyerere. Hii ni 100% mwekezaji kwa hiyo lakini akija mwekezaji anataka kufungua kiwanda cha mbolea au vyuma utasema haiko kwenye ilani yetu? wa Rundi wanajenga kiwanda cha mbolea Dodoma wazuiwe kwa kuwa haiko kwenye sera? tofautisha miradi ya kimaendeleo serikali ikiwa wabia na miradi ya uwekezaji. Bandari ni wawekezaji sio mkopo na LNG ni wawekezaji sio mkopo mtofautishe mambo. ilani inakuja na miradi ya kimkakati ya kimaendeleo. narudia tena Bandari ni wawekezaji na sera moja kuu kuvutia wawekezaji waje kuwekeza shida iko wapi?
 
Nimemjibu Nape, soma tena alivyoandika.
 
Hawa vijana wasioweza kulitumikia taifa mpaka wawe mawaziri hawafai, wanajiona bora zaidi ya wengine, uongozi wa serikalini usitafutwe kwa kelele nyingi za mitandaoni, uadilifu wa mtu na uchapakazi wake ndio uwe vigezo.
Kwa mara ya kwanza nakupa heko saana kwa point nzuriiiii,
 
Nimemjibu Nape, soma tena alivyoandika.
Sijakuelewa umemjibu Nape kitu gani? nimeona jana Mangula kusema Bagamoyo haiko kwenye sera ndio utashangaa hajui kwamba ule uwekezaji au anajitoa ufahamu. wawekezaji walishandwa kuafikiana na awamu ya tano kwa baadhi ya masharti kama tulivyoambiwa hii awamu wanasema hakukuwa na makubaliano ila maongezi tu hivi sasa ndio wanataka kuingia kwenye majadiliano wa mradi. Kitu kikubwa hapa huu sio mradi wa serikali ni mwekezaji 100%. Sera peleka huko kwenye afya, miundo mbinu sera za mambo ya nje na kadhalika.
 
Ni hatari sana eti kuzunguka nchi nzima kuitangaza Ilani yako ili uchaguliwe kumbe ni danganya toto. Hii ni hatari sana! Kama Ilani inashindwa kudumu kwa miaka 5, hii ni zaidi ya hatari. Inamaanisha .P W Boatha ni ukweli maneno ya aliyekuwa Rais wa Afrika kusini aliyesema- Mtu mweusi plan yake ni ya siku moja tu, na ya keshokutwa yatajulikana kesho kutwa. Du, hapa ndipo Nape anapotueleza kuwa CCM fikra zake haziwezi kuplan kwa miaka 5.

Kwa kawaida vitu vya dharura ndio hubadilika, kwa Nape ni amka na uje na wazo jipya kila kukicha - Populist! Makosa ni makosa hata kama yalifanyika toka kwa baba wa Taifa aka Mazoea...Tusihalalishe. Inawezekana hii ndio sababu ya kuwa hapa tulipo baada ya miaka 60 toka mkoloni atuachie nchi yetu aka tupate uhuru.

Jamani, kama hiki chama hakiwezi kuplan kwa miaka 5, kitaweza kweli kuwa na plan ya miaka 10, 15, 20........... Kama hivyo ndivyo, samahani nitakopa neno la Mh Rais "Nonsens" kuwa kuisoma Ilani ya uchaguzi ya CCM ni NONSENS.

M/ mwenye kiti Mangula yupo sahihi 100%, kama tunahitaji kutekeleza vipaumbele vya miaka 5 (2020-2025)wananchi walivyoiingiza CCM madarakani kwa bajeti yetu Finyu ya max 1.9 trilion kwa mwezi. Vipaumbele ndio kila kitu, leo yaliyoelezwa kwenye kilimo yamesahaulika kabisa na yalisahaulika vile vile (2015-2020). Hii inamaanisha miaka 10 bila kilimo, sigusii sakata la kilimo cha miwa/sukari.... Ah acha tu Pole waziri wa kilimo Profesa Mkenda - Pesa yako inakwenda Bagamoyo/Bandari....
Yote tisa chama gani unadhani ktakuwa na plan ya mda nzuri naomba usinitaji CDM tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa na bias lazima utapotoka kwani mawazo yako yataegamia upande mmoja. Tufanye analysis kuangalia pande hizi mbili zinazokinzana ili tupate kitu kimoja kitakachoifaidisha nchi yetu. Mzee wetu mangula ana hoja na kijana wa mtama ana hoja pia
Mangula ana hoja ila kijana ana agenda ya siri, msikilize na kumtazama kwa sikio na jicho la tatu respectively
 
Hiyo tunaita going extra mile. Matokeo yake no exceed expectation tukiweka endurance perfomance management. Chapeni kazi
 
Tusikubali bandari ya Bagamoyo kuingia mikononi mwa Wachina.
Bandari ijengwe itupunguzie foleni huku Morogoro road na Mandela road.

Copper yote ya Wachina iende Bagamoyo.
 
Tatizo sio kujengwa bali inajengwa na nani kwa masharti gani? Ingependeza hata pwani yote ya Tanzania kila mkoa uwe na bandari kubwa.
Mvua iwake jua linyeshe bagamoyo port lazima ijengwe.

Hata akifa Leo rizimoko atasimama kidete.
 
Sijakuelewa umemjibu Nape kitu gani? nimeona jana Mangula kusema Bagamoyo haiko kwenye sera ndio utashangaa hajui kwamba ule uwekezaji au anajitoa ufahamu. wawekezaji walishandwa kuafikiana na awamu ya tano kwa baadhi ya masharti kama tulivyoambiwa hii awamu wanasema hakukuwa na makubaliano ila maongezi tu hivi sasa ndio wanataka kuingia kwenye majadiliano wa mradi. Kitu kikubwa hapa huu sio mradi wa serikali ni mwekezaji 100%. Sera peleka huko kwenye afya, miundo mbinu sera za mambo ya nje na kadhalika.
Serikali itahitaji ilipe gharama zote ili mradi urudi kwa serikali
 
Pesa wanazotoa Wachina iwe misaada, mikopo au uwekezaji haina uwajibikaji kabisa kutoka kwa watawala , wanaitoa hewala hewala makusudi tu wakijua mwisho wa siku itashindikana kulipwa na taifa litanasa katika mtego deni.

Pia mambo yao mengi hayana uwaza kabisa, hii ni hatari kwa mataifa ambayo yanakabiliwa na matatizo makubwa ya ufisadi wa mali za umma.
Kwanini Mkuu?
 
Back
Top Bottom