INAUMA NA INA UMIZA SANA...
Na Charles Francis M,
Askari aliye vaa kofia akitoa BASTOLA mbele ya aliye kuwa waziri wa habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Ndugu Nape Nnauye. Askari huyu aliulizwa kitambulisho chake cha kazi lakini alitoa BASTOLA ambayo ni silaha ya moto. Yaani haya yanatokea katika nchi inayo itwa huru na yenye amani.
Askari huyu angetoa silaha ya moto ikiwa tu Nape angetoa silaha pia au kungekuwa na hali tete kiusalama inayo zuia polisi kufanya kazi yao au ina hatarisha uhai wa polisi, chini ya ruhusa ya matumizi ya "reasonable force". Lakini none of them happened, absolutely none!! Lakini polisi huyo aliona ni busara ya mwisho kutoa BASTOLA tena hadharani mbele ya wana habari na Camera zao na tukio hilo likiwa "live".
SWALI LANGU: Nape kafanyiwa hivi hadharani, ni mtu maarufu na kiongozi mkubwa, Je wananchi wa kawaida kule vijijini?? Je, kiongozi wa upinzani atafanyiwa nini akiwa katika anga za askari huyu?? Askari huyu weledi wake wa kazi ni kutumia BASTOLA anapo ombwa kitambulisho?? NAONA GIZA, imeniuma sana kuona hali hii nchini, sijawahi kuandika haya lakini moyoni nimeumia sana sana sana.
Nilikuwa nikiona haya kule Uganda akifanyiwa mpinzani Kiza Besigye lakini leo naona hadharani nchini kwangu, nimeumia sana, naandika ujumbe huu nikiwa nimeumia.
Pamoja na dhambi za Nape katika kauli ya "goli la mkono" ile ya kusema Lowassa na wanao ondoka CCM ni "oil chafu" na kadhalika lakini ushujaa wake ume onekana katika mwisho wa nafasi yake kama Waziri Mwenye dhamana ya habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo akitetea maslahi ya wana habari na watanzania.
MUHIMU SANA: Kila mmoja ajiulize, UKO SALAMA KIASI GANI ukiwa mikononi mwa mlinda usalama wa aina hii ambaye ana haraka ya kutoa silaha ya moto kuliko kitambulisho!!
"Caytano Maytano"
Charles Francis M.