Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari

Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari

Tunapotaka Jeshi la Polisi liboreshwe na liachane na kasumba za mkoloni tunataka kuepukana na ubabaishaji kama huu wa kuamrisha kufanya kitu hata kama hakina msingi wa kisheria. Kuna wapuuzi wanadhani hili jeshi ni poa tu maana linashughulikia zaidi wapinzani(Lissu na Lema), lakini upuuzi huu unajengeka ndani ya jeshi na matokeo yake watakaoumia zaidi ni wanyonge ambao hata elfu tano ya kumhonga askari amuachie hana.

Haya mambo hayana mwenyewe. Hata rais anaweza kuwa victim wa jeshi kama hili-maana kuna kustaafu. Kuna ndugu na jamaa ambao wanaweza wakaangukia ktk mikono ya jeshi hili babaishaji. Hata askari wenyewe hawako salama ndani ya jeshi hili. Fikiria mtu anakutuma wewe askari ukaue wakati yeye amekaa na mke wake nyumbani. Kumbuka unaua mtu-sio kuku na hivyo damu ya mtu huyo inakuandama maisha yako yote. Mshahara mnaopata enyi askari hautoshi kuua raia wema wanaotumia haki yao ya kikatiba kuwa na mawazo tofauti na watawala.

Hata huyu alikuwa Rais na aliagiza wengine wafanyiwe kama ilivyokuwa kwa Nape lakini naye walipochoka yakamkuta"
b86a08935bb0c1ce63f398639cf47387.jpg

28cc82ebd091288a45748b55a6742682.jpg

da19762d5d6a99fb5cfe405a361e0f4f.jpg
 
Aiseee, leo Nape ni wa kufanyiwa hivi. Kweli namba imesomeka.
 
Dah!

Mimi si mpenzi wa CCM na si shabiki wa Nape ila hicho nilichokiona kwenye hiyo video sijakifurahia.

Kwangu haki ni haki tu.

Ni nini hasa kilipelekea yote hayo?

Kuna anayejua humu anieleweshe zaidi?
kuna namba inaitwa KolamiJ Bashite ipigie itakupa ufafanuz
 
Kwani alitaka kupindua nchi au kuvunja amani nchini!?

Imefika muda watu tuache kufatilia issue za Mh. Makonda, tumuache afanye kazi yake vizuri na Mh Rais wetu pia alitumikie taifa.

Nape huyo atapangiwa kazi ingine ikipatikana kujua itakayomfaa na pia mambo yakipoa, kuna gemu na leo ndio mipango yao imeishia hapo.

Ilibidi nyie wananchi mbaki mnayaongelea, ha ha haaaaaaaa


Movie ya Nape baada ya kunaswa mchezo wake Junatatu, imebidi tu aimalizie kwa kuwaomba iishe hivi. Ndio maana hajatamkwa kwenye Barua kuwa yeye vipeeeee.

Hivyo Nape kapata kuondoka na bonge la plan aliyomuomba Rais au RC wa Dar apate leo, nanyi wananchi mmefurahia na kumuombea huruma na ndilo hiyo movie mmepewa.

Future ya madaraka, jina libaki kwenye midomo yenu. Na hivi wengi hamjifikirishi basi tena, wachache tu ndio watakuwa wamedaka gemu.


Nimempenda Rais kwa kumuacha asogee pembeni kwa style yake, bila kumuongelea kwa maneno mengi or kumtumbua live.


Mungu ibariki Tanzania.

Makonda oyeeeee

Tumuache aendelee kutapeli watu.
 
Back
Top Bottom