Nape Nnauye: Hatukuwakatalia Starlink kufanya kazi Nchini, walikwama wenyewe

Hii Nchi kuna vitabia vya kiujamajamaa kwenye mambo ya biashara na masharti ya kipimbimbafuuuu.

Hata huo ujamaa haupo.

Huyu waziri yumkini alihongwa na watoa huduma za internet waliopo nchini, atengeneze mazingira ambayo yatazuia Starlink kuwepo nchini ili kuzuia ushindani. Hayo wanayafanya sana hawa watawala wa nchi hii, tangu zamani.

Namkumbuka waziri mmoja aliitwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee. Nami nikiwa mwalikwa pia. Yeye watengenezaji wa spring, ambao walikuwa chini ya wizara, wamchangie ili naye achangie kwenye harambee kama mgeni rasmi. Ilikuwa ni wakati wa utawala wa Kikwete. Watengenezaji wa spring za magari, wakamwambia waziri amtume msaidizi wake akachukue mchango. Msaidizi akaenda akapewa shilingi milioni 6. Waziri alivyoletewa, akamaka, tena mbele ya sisi wachache tuliokuwa pale tukiongea naye, "hawa wajinga sana. Wananichangia mimi milioni 6, wakati nimezuia spring kutoka nje ili wao wauze, halafu wananichangia milioni 6! Kawarudishie hiyo milioni 6 yao". Dereva akaondoka kwenda kurudisha pesa. Baada ya muda akarudi na pesa nyingi zaidi. Akamwuliza msaidizi wake, wamekupa shilingi ngapi? Msaidizi akasema milioni 12. Waziri akasema, afadhali. Cha ajabu kwenye harambee alichangia milioni 6.
 
Mimi nimeleta taarifa na siyo vinginevyo. Kwani umewasiliana na Starlink wakakwambia walinyimwa fursa ya kufanya kazi Nchini licha ya kuwa walitimiza masharti?

Lucas, wewe ni mchanga kwenye masuala ya uwekezaji wa kimataifa. Tuliofanya kazi kwenye taasisi za kimataifa za kibiashara, yabidi tukupe shule.

Unapotaka kwenda kuwekeza kwenye nchi yoyote, hukurupuki tu na kusema naenda kuwekeza.

Kwanza unaenda kwenye company selection criteria ranking. Hii inaonesha hiyo nchi ina-rank vipi katika vigezo vya kampuni. Hiyo ranking, inatengenezwa kwa kuitazama kila nchi kuhusiana na sheria na kanuni za uwekezaji katika hiyo nchi kwenye sekta husika. Nchi inavyozingatia utawala wa sheria, ubora wa mahakama zake, uanachama wake kwenye taasisi za kimataifa zinazosimamia biashara, uwezo wa wananchi wake katika kununua products zako, mikataba ya hiyo nchi na nchi nyingine katika biashara, sheria za kodi, miundombinu, corruption, government stability, n.k. Lakini pamoja na kuwa na taarifa hizi kuhusu nchi unayotaka kwenda kuwekeza, huu ni muongozo tu wa kukusaidia mahali pa kuanzia.

Unapokuwa umeamua kuwa unataka kwenda nchi fulani, mara nyingi unai-contract an independent firm, mara nyingi ni local firm, kufanya due diligence ya kila kitu kilichopo kwenye criteria ranking. Ukijiridhisha na hayo, ndipo unakuja kwa nia ya kukutana na wasimamizi wakuu wa sekta na kuwaeleza dhamira na maamuzi yako ya kutaka kuwekeza katika nchi husika. Na kama kuna kitu ambacho wakati wa due diligence kilionekana kuwa bado kuwa na mashaka, sasa unaweza kuomba ufafanuzi moja kwa moja kwa serikali husika.

Hivyo Starlink kabla ya kuja Tanzania, lazima sheria na taratibu zote za jumla zinazoongoza sekta watakuwa walizipitia na kuridhika nazo. Bila shaka walikwama kwenye level ya kukutana na wasimamizi wakuu wa sekta. Ndiyo maana ni muhimu sana kufahamu wakuu wa sekta waliwaambia nini Starlink ambacho hakipo public, kiasi cha wao kuona nchi yetu haifai wao kuwekeza. Hatutakiwi kupokea tu hadithi za Nape, eti tu walishindwa masharti. Ni kauli ambayo ni very unprofessional.
 
Umeyaelewa lakini maelezo ya serikali?

Maelezo ya Nape ni upuuzi mtupu! Ametoa maelezo kama vile babu anawasimlia wajukuu zake hadithi. Sijui ni lini viongozi wetu watakuwa na uwezo wa kutoa maelezo yenye facts wanapojibu hoja za wananchi!!

Uwekezaji wa kampuni kubwa kama ile una manufaa makubwa sana kwa wananchi, kuanzia huduma, mafunzo kwa watu wetu katika hiyo tekinolojia, mpaka ajira. Jukumu la kiongozi ni kusaidia uwekezaji ushamiri badala ya kutengeneza mazingira adui kwa uwekezaji.

Viongozi wa China, kila siku wapo Ulaya kutafuta wawejezaji, Nape anashindwa hata kumvakiza mwekezaji ambaye amekuja mwenyewe nchini. Huyu alistahili kufukuzwa.
 
Mama Anatosha na Chenji inabaki
 
Maelezo ya Nape ni upuuzi mtupu! Ametoa maelezo kama vile babu abawasimlia wajukuu zake hadithi. Sijui ni lini viongozi wetu watakuwa na akili na uwezo wa kutoa maelezo yenye facts wanapojibu hoja za wananchi!!
Tuambie wewe Starlink walikataliwa na nani? Thibitisha maana sio mara ya kwanza Nape kutoa haya maelezo
 
Walikwama kwenye level ya wasimamizi Wakuu? 🤣🤣🤣 Acha blaa blaa wewe kwamba kuanzia Waziri Hadi Wakuu wa sekta walikataa au? 😂😂

Umeandika maelezo meengi afu ujinga mtupu no facts,weka hapa sababu za Starlink Kushindwa maana Serikali ilisema walishindwa masharti.
 
Bibi Yako ndio analala chini na hizo blaa blaa zingine.

Mwisho ehee Machadema wasio na sera Wakishika Dola ndio watakuwa wanawagawia pesa au? 🤣🤣🤣🤣

Ni punguani tuu ndio anadhani Wanasiasa wanamfanya awe maskini na kwamba wakija wale anaowataka atakuwa Tajiri.Tafuta pesa acha kutegemea favor za Kisiasa
 
Kuna kila uwezekano kuwa masharti yetu ni pamoja na ku control watoa huduma za internet, wapi tuweze kuzima data na wapi tuweze kuruhiusu. Kitu ambacho Starlink wana kila sababu akukikataa na Tanzania wana kila sababu ya kuikataa starlink kwa kutokufata masharti.

Matokeo? Tutabana mpaka lini? Si yasemwe wazi hayo masharti waliyoshindwa kutimizwa na star link?

Weka link tumsikie Nape kasema nini.
 
Mheshimiwa waziri hajayasema hayo masharti ambayo Starlink walishindwa kuyatimiza kwa ajili ya kupewa lesseni ya kufanya kazi hapa nchini.
 
Tuambie wewe Starlink walikataliwa na nani? Thibitisha maana sio mara ya kwanza Nape kutoa haya maelezo

Taarifa ya Starlink ilisema wameamua kutoendrlea na mipango ya kuwekeza Tanzania kutokana na kuwekewa mazingira magumu. Hawakufafanua. Nape ndiye anatakiwa kutoa maelezo ni masharti gani hayo waliyowekewa Starlink. Dunia nzima, wawekezaji wanatafutwa. Sisi tunashindwa kumpata hata mwekezaji aliyekuja mwenyewe nchini. Halafu tunajificha kwenye hadithi kuwa alishi dwa masharti; ni masharti gani hayo, si aseme.

Ifahamike kuwa nchi inawahitaji zaidi wawekezaji kuliko wawekezaji wanavyoihitaji Tanzania.

Fikiria nchi kama China, inatoa vivutio vingi kwa wawekezaji wa nje kuliko hata wawekezaji wa ndani. Na hiyo ndiyo imeisaidia China kuwa mahali hapo ilipo leo. FDI ya China kwa kila mwaka ni kati ya dola bilioni 80 mpaka 100. Sisi haifiki hata bilioni 2 kwa mwaka. China ina makampuni ya kigeni zaidi ya milioni 1, sisi nchi kapuku tunawawekea vikwazo wawekezaji, na tukiwapokea wawekezaji, tunaingia mikataba ya hovyo inayolenga kuwanufaisha watu wachache badala ya Taifa zima.

"China's FDI Policies

China's laws and regulations on FDI also include related preferential policies and stipulations for special economic zones in the country. In a nutshell, China encourages favorable FDI policies. Therefore, FIEs enjoy preferential treatment when compared to domestic enterprises."
 
Nape amesema Wameshindwa masharti Kwa mujibu wa vigezo vya TRA.

Walioshindwa ndio waseme sio kazi ya Maofisa wa Serikali kuwasemea.Huo ujinga wa kusema madalali mfanye nyie Chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…