Nape Nnauye: Hatukuwakatalia Starlink kufanya kazi Nchini, walikwama wenyewe

Nape Nnauye: Hatukuwakatalia Starlink kufanya kazi Nchini, walikwama wenyewe

Kwani wewe umewasiliana na Starlink wakakwambia walinyimwa lesseni licha ya kutimiza masharti ya leseni waliyopewa na yaliyotokewa?
Kwa hio ni kwa masharti ya Tanzania tu ndipo wameshindwa kutimiza, Kenya wameweza, Nigeria wameweza, Rwanda wameweza, yaani Tanzania tu, acheni uhuni nyie.

Kwa makusudi mlitaka starlink isifanye kazi hapa kwa kutoa masharti kama ya mganga, mzungu hana huo muda.
 
HIZI SIASA ZA UONGO UONGO NI ZA MUDA MFUPI TU Lucas,utakumbuka Haya menono.
Ulipaswa kuwa mtu wa kohoji vitu kama kijana badala ya kusifia sifia hovyo,

Kwa faida ya Nani?Nikuambie kwa hizi ngonjera hawatawajibika hawa watawala.Bibi zetu akiwemo wa kwako na ndugu zetu wataendelea kulala chini wakiwa hospitalini,Bima ya Afya ya kilaghai, Dhuruma zaidi ya wananchi kwenye matumizi mabaya ya serikali.

Sijawahi sikia hata siku moja ukihoji kuhusu kupuuziwa riport ya CAG iliyojaa wizi ufisadi,wewe kazi yako ni kusifia tu vitu visivyo na kichwa wala miguuu.

Mashart gani?kwanini asiyaweke wazi,Je walikataa kulipa kodi?

Je walitaka makampuni mengine Ya simu/Mtandao yafutwe au?

Kwakuwa ni swala la uma basi iwekwe wazi walipewa masharti gani.

Mbona Magufuli alikataa mradi wa bandari ya Bagamoyo na kusema wazi sababu,iwaje kuwe na usiri kwenye mawasiliano.

Mama alienda kuzindua Kiwanda cha Howo Juzi kati Hapo alisema jamaa wanataka Hili na lile,sisi tumewapa Hili na lile,shida iko wapi.

Nape aache,Acheni ujanja ujanja sisi sio wajinga.

Alienda media tour kufanya nini si angeeleza sababu moja kwa moja?

Hilo Taifa ifike mahali mnaposema maslahi ya nchi mbele muwe mba maanisha sio porojo tuu.
Lucas hizi siasa za uongo uongo ni za muda tuu narudia ni za muda tuuu.
Any way nalala maana naijepandisha sukari buree bila sababu.
Lucas Mwashambwa ni kama toilet paper TU, haiwezi kuhoji, inatumika TU na kutupwa shimoni
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Nape Nnauye waziri wa Habari ,Mawasiliano na teknolojia ya habari amesema ya kuwa serikali haikuwakatalia Starlink kufanya kazi Nchini bali walikwama wenyewe kutimiza mashariti yaliyohitajika kukamilishwanl ili kupewa lesseni.

Kauli hii imekuja kutokana na manung'uniko na kelele nyingi sana za watanzania mbalimbali mitandaoni kuilaumu serikali hususani waziri mwenye dhamana wakati huu ambao mtandao wa internet umesumbua sana na kukwamisha shughuli nyingi sana katika maofisi mbalimbali ya watu binafsi pamoja na serikali yenyewe.

Ambapo watu mbalimbali na wadau mbalimbali wa habari na mawasiliano wameonekana kutoa maoni yao mitaani na mitandaoni kuwa pengine kama Starlink angekuwepo hapa nchini ,suala lililokuwa limejitokeza hapa nchini la kukatika kabisa kwa huduma ya internet pengine lisingeathiri shughuli za watu binafsi pamoja na serikali yenyewe kama ilivyotokea.

Naweka kalamu chini na kuishia hapa. Chanzo cha taarifa yangu Ni clouds. Ukitaka kwa undani sana ingia clouds ujionee video yake kama una Mb au bando la kutosha kiasi.kama huna mb za kutosha basi wewe chukua hii taarifa kuwa serikali haikuwakatalia Starlink kufanya kazi Nchini bali wao ndio walikwama wenyewe kutimiza mashariti ya kupatiwa lesseni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Bumunda lingine hili!
 
Starlink wapewe masharti spesho kama nani wao labda? Masharti ni Yale Yale ya siku zote
K
Bibi Yako ndio analala chini na hizo blaa blaa zingine.

Mwisho ehee Machadema wasio na sera Wakishika Dola ndio watakuwa wanawagawia pesa au? 🤣🤣🤣🤣

Ni punguani tuu ndio anadhani Wanasiasa wanamfanya awe maskini na kwamba wakija wale anaowataka atakuwa Tajiri.Tafuta pesa acha kutegemea favor za Kisiasa
aisee,Kumbe naongea na Wavulana hapa.
 
Kwani umeambiwa wapi kazuiwa? Serikali inasema kuwa alikwama Mwenyewe
Mambo mangapi serikali inasema kumbe ni wahuni wametuingiza chaka halafu nchi inakuja kupata hasara?!.
Mikataba ya hovyo ya Songas, Meremeta, Kagoda kwa uchache tu.
Wewe ndio wale utakuja kuambiwa vua boksa halafu utavua kweli kisa tu umeambiwa ufanye hivyo na Waziri!!.
 
Mambo mangapi serikali inasema kumbe ni wahuni wametuingiza chaka halafu nchi inakuja kupata hasara?!.
Mikataba ya hovyo ya Songas, Meremeta, Kagoda kwa uchache tu.
Wewe ndio wale utakuja kuambiwa vua boksa halafu utavua kweli kisa tu umeambiwa ufanye hivyo na Waziri!!.
Acha kutumia lugha za kihuni na kidhalilishaji.
 
Kufungua Nchi haimaanishi kuifanya nchi kuwa kama Jalala au jengo lisilo na mlango ambalo kila kitu kinaingia tu bila utaratibu wala hodi.
Screenshot_20240516-110500.png
 
Kufungua Nchi haimaanishi kuifanya nchi kuwa kama Jalala au jengo lisilo na mlango ambalo kila kitu kinaingia tu bila utaratibu wala hodi.
Kwahiyo Starlink ni sawa na jalala? Maana mkuu hauna cha ziada unachojua kuhusiana na ukweli hasa wa hili jambo ila ajabu unaona Starlink ndio kashindwa masharti na si kwamba kawekewa mazingira magumu kwa maksudi.
 
Masharti ni kwamba, walivaa shati la mikono mifupi. Nchi hii bila kuhonga masharti lazima yawe magumu.
 
Kitu chochote, hata iwe ni tekinolojia nzuri kiasi gani, kuna wakati inaweza kukumbwa na tatizo.

Hapa tunaongelea alternatives. Ni sawa uwe na gari moja. Lazima kuna siku utakosa usafiri. Ukiwa nazo angalao 2, moja itakapoenda garage, utaitumia nyingine, na mipango yako haitakwama kwa 100%.
Huenda pia wakawa wameshindwa kuendana na Terms za Kisheria za nchi kwa wao kufanya kazi nchini
 
Back
Top Bottom