Pre GE2025 Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ccm imuite kwenye maadili amekosea sana.

Kama yeye amezoea hivyo anatakiwa ajue kwmaba Samia hahitaji kuiba Ili ashinde maana Kila mtu anaona Rais anachofanya Nchi nzima katika kutekeleza ilani 👇👇
 
Mungu anawaona.
 
Nape kwa kujinadi kwamba ndiye bingwa wa kuchezesha uchaguzi, na kwa kuzingatia ndiye, kiongozi wa wizara ya habari na techinologia, ana uwezo wa kuchezesha vishikwambi apendavyo hakuna sababu ya kupoteza mapesa ambayo yangesaidia maendeleo mengine.
 
Hizi kauli zinapaswa kupingwa kwa nguvu zote, hata kama hizo mbinu huwa zinafanyika hazipaswi kutangazwa hadharani kama vile ni halali wakati ni haramu kwa mjibu WA Sheria na taratibu za uchaguzi. Huko ni kulewa madaraka, kulewa fedha za umma za masikini, serikali na Chama cha mapinduzi zinapaswa kuchukua hatua Kali za kinidhamu kwa kudhalilisha Sheria za uchaguzi na CCM kwa ujumla. Itashangaza kwa serikali na CCM kama vitafumbia macho kauli kama hizi, lazima awajibishwe, tunaandaa siasa gani Kwa vizazi vijavyo kwa kauli kama hizi, uko wapi utawala Bora? Kauli hizi ni uchafu na aibu kwa vyombo vinavyosimamia haki na Sheria.
 
Tumefilia pabaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…