Pre GE2025 Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hata, hivyo, kuna kosa gani alilofanya katika serikali hii!? 🤔...

Mimi binafsi, kutoka katika sakafu ya moyo wangu, sioni ajabu, sishangai na wala sikasirishwi na alichokisema Mh. Nape (tena natumia neno Mh. nikimaanisha anastahili kuitwa Mh.)...

Jamani, si tunataka kiongozi mkweli, ambaye si mnafiki?

Sasa Mh. Nape amekosea kitu gani kuweka wazi kile ambacho wasimamizi wa uchaguzi (inayoitwa tume huru ya uchaguzi) wamekuwa wakikifanya kwa miaka yote?

Kosa lake ni lipi jamani? Kusema ukweli? Mnataka kusema kwamba mlikuwa hamjui kwamba anachokisema Nape ndo huwa kinafanyika siku zote? Uchaguzi wa 2019 (serikali za mitaa) na 2020 (madiwani, wabunge na Rais) anachosema Nape si ndo kilifanyika?

Wote mnajua na mmeshuhudia kile alicho kisema Nape!

Kwa maoni yangu, tunawahitaji viongozi wengi aina ya Nape Mnauye. Pengine umma utawaelewa...na hatimaye labda ufanye uamzi stahiki wa kuchukua hatua.

Nionavyo mimi,Nape ni kama Yuda Iskariotu, mpango wa Mungu usingekamilika bila Yuda Iskarioti kufanya alicho fanya!

Wenye kunielewa wameelewa, ambao hamjanielewa, KAZI IENDELEE
 
Acheni wizi wa kura
Hamna wizi uliotokea so far ndugu yangu wa kutokea upande wa pili . 2024 mjipange kweli kweli. 2025 ndio kabisa. Wananchi watawaacha mdomo wazi . Kelele ziko kwenu mtandaoni , ila kwa ground mambo yako different ambao ndio wengi wanaelewa ubora wa CCM . Sidhani kama nyie mko tayari kuishikiria hata ubunge viti 10 , mmechoka sana kwa sasa , hamtustui kabisa. MAMA NJIA NYEUPE . MITANO 5 .
 
Nimesikitika saanaa,ila nchiii hiii mtu akiwanakinga serikalini anaweza ropoka lolote na raia wasipate Cha kufanya. Hii ilikua palepalee wangembakaa!
Hayo yamesemwa nje ya uchaguzi . Wakati haujafika na wala hayo yaliyosemwa hayajatendeka. Acheni siasa chafu. Mangapi yanaongelewa kwenye majukwaa yenu . MTAENDELEA KUSEMA VICHACHE ambavyo havina TIJA . nguvu wekezeni kwenye SERA BORA , acheni kufanya siasa za MATUKIO . wenzenu ngoma inazidi kusonga mbele . SAMIA NJIA NYEUPE 2025
 
Wewe Kamanda wa Mbowe acha kupotosha umma
Hawa ngoma ngumu , wamebaki kupiga kelele za kueneza tu chuki kila ya leo . Wazee wa MATUKIO . MAJI YA SHINGO , CCM NDIO KWANZA IMEZALIWA UPYA , INA VIJANA WAPYA NA WENYE UPEO MPYA NA WA KISASA , CPA MAKALA siku za karibuni kasema CCM INAWALETEA VIONGOZI WAPYA NA BORA ZAIDI , KAZI KWENU WAZEE WA UFIPA .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…