Nape Nnauye: Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi

Nape Nnauye: Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
1686205833892.png

Picha: Nape Nnauye

Habarini JF GT!

Jana wakati Membe akirudishiwa kadi ya CCM, Mbunge wa Mtama na Wazari wa Habari nchini aliongea kauli mbaya Sana Na Yenye kufedhehesha kwa Marehemu.

Kwa tamaduni za kitanzia Sio sawa kumsema Marehemu, na hata Ukitaka kumsema Marehemu utamsema kwa Mazuri. Lakini hii imekuwa Tofauti kabisa kwa baadhi ya Wanachama wa CCM na Viongozi wa CCM, wamekuwa Wakimsema Hayati Magufuli Hadharani mbele ya wananchi waliomchagua kwa kura nyingi. Hakika CCM inajiua Yenyewe

Jana Ndugu Nape (Namuita Ndugu kwasababu kwangu mimi sioni kama Anafaa kupewa heshima ya Jina Mheshimiwa) wakati wa Sherehe zile alisimlia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na Yeye alivyo nusurika kufukuzwa CCM na Membe kumsadia, kipindi hicho naamini Magufuli hakuwa Kiongozi mkubwa wa CCM, Nape aliongea kumaanisha kuwa Magufuli alikuwa chanzo kikubwa cha Membe kuondoka CCM na Kutengeneza ugomvi mkubwa na Wana CCM wengine.

Nape akaenda mbali zaidi na Kusema Kuwa Ugomvi huo Mungu ndio ameamua na sasa bahari imetulia iko shwari, akimaanisha Kifo cha Magufuli ni Maamuzi ya Mungu katika Kutatua ugomvi wa Wana CCM na Membe… Akaendelea mbele na Kusema nani Kama Rais Samia Suluhu.

Ikumbukwe kuwa Huu utamaduni uliopo sasa kwa kumsifia rais hata pale anapo fanya Baya ulianza kipindi Cha Magufuli na Umeendelea hadi awamu hii kwa kusema Mama anaupiga mwingi. Nyakati za Kikwete, Mkapa hakukuwa na huu ujinga.

Turudi kwenye mada, Nape Nauye ni lini Ataacha kuwa na Kinyongo na Marehemu? Nilini ataacha Kumsema Marehemu? Huu umekuwa muendelezo wake toka Awe Waziri tena Wa Habari, Je aliteuliwa kuja Kumsema Marehemu?

Ni wakati sasa Wa Nape kumuacha Marehemu Apumzike Mahali pema na kwa amani. Asitafute chuki na watu zisizo za msingi
 
Yeye Magufuli alipokuwa hai mbona hakuwaacha wenzie wapumzike kwa amani?

Yuko wapi Ben Saanane? Azori Gwanda, Lissu Lema na wengineo tusiojua majina yao.

Acha watu waseme ya moyoni, kama alifanya mazuri atasemwa kwa mazuri na kama alifanya maovu atasemwa kwa maovu yake, kila mtu ana hadithi yake.
 
Ni kweli alichosema Nape, Mungu amelata amani

Na kifo chake sio kimeleta amani kwa CCM tu, bali kwa vyama vingine na kwa nchi kiujumla, vyama vya upinzani walikuwa wakiwindwa kama swala,

hata ugomvi wetu na nchi jirani umeisha na sasa Tz inafanya biashara na majirani zetu vizuri

Na sio nchi jirani tu, hata jamii kubwa ya kimataifa ilikuwa na ugomvi na Tanzania ila baada ya Mungu kufanya yake, sasa hivi Tanzania ni rafiki wa kila nchi, za Mashariki na Magharibi

Ama kweli Mungu ameleta amani, MUNGU NI FUNDI
 
Acheni ujinga. Nyie mbona kila kukicha mnamsema vibaya Idd Amin au Hitler? Ukizuia watu wasikuseme ukiwa hai watakusema ukiwa mfu.

Kupanga ni kuchagua
Hakuna mtu nimewahi kusoma sehemu yoyote akikejeri kifo Cha Hitler Wala Idd Amin, HAKUNA!

Kwanza Hitler aliamini hawezi kuuliwa na ni vigumu Sana yet kufa, aliwahi hata kutaja hadharani kwamba yeye hawezi kufa,
 
jamaa amekufa lakini kuna watu micundu inapwita[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

kweli magu ilikuwa komesha ya wasenge.
poleni jamani iwekeni chini haamki huyo.
Ila kina Nape haya maneno ya shombo yatawacost ikitokea Rais Ajaye akawa na akili atawapiga chini wote

Ningekuwa Rais uchaguzi ujao Kuna majimbo Bora niwape wapinzani tu, Nape ni mropokaji
 
Viongozi waandamizi wa chama kile kile hadharani wanamnanga Rais na mwenyekiti wao ambaye ni marehemu. Hawa ndio walikuwa wanalia baadhi ya wastaafu kusemwa lakini kumbe issue ilikuwa ma godfather wao kusemwa ila nao ni sehemu ya hako kaugonjwa.

Chama ni kama wamebariki haya matusi toka JPM afariki! Hii mbegu ilipandwa awamu ya 4 ikajikita awamu ya 5 na sasa imestawi na itawagharimu kuifuta maana kwa walivyo watu wa chama kile visasi havitakoma.
 
Back
Top Bottom