Van pebles
JF-Expert Member
- Oct 23, 2018
- 2,861
- 5,305
.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na Huu ndio ukweli, Rais JPM hakua na uchaguzi mwingine zaidi ya kua mkoloni ,na matokeo yake tuliyaona.
Sasa angalieni, ya 2005 mpaka 2015 Yale ambayo hata mtoto Mdogo alichukizwa nayo, ndio yamejirudia.
Mwosha huoshwaView attachment 2649739
Picha: Nape Nnauye
Habarini JF GT!
Jana wakati Membe akirudishiwa kadi ya CCM, Mbunge wa Mtama na Wazari wa Habari nchini aliongea kauli mbaya Sana Na Yenye kufedhehesha kwa Marehemu.
Kwa tamaduni za kitanzia Sio sawa kumsema Marehemu, na hata Ukitaka kumsema Marehemu utamsema kwa Mazuri. Lakini hii imekuwa Tofauti kabisa kwa baadhi ya Wanachama wa CCM na Viongozi wa CCM, wamekuwa Wakimsema Hayati Magufuli Hadharani mbele ya wananchi waliomchagua kwa kura nyingi. Hakika CCM inajiua Yenyewe
Jana Ndugu Nape (Namuita Ndugu kwasababu kwangu mimi sioni kama Anafaa kupewa heshima ya Jina Mheshimiwa) wakati wa Sherehe zile alisimlia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na Yeye alivyo nusurika kufukuzwa CCM na Membe kumsadia, kipindi hicho naamini Magufuli hakuwa Kiongozi mkubwa wa CCM, Nape aliongea kumaanisha kuwa Magufuli alikuwa chanzo kikubwa cha Membe kuondoka CCM na Kutengeneza ugomvi mkubwa na Wana CCM wengine.
Nape akaenda mbali zaidi na Kusema Kuwa Ugomvi huo Mungu ndio ameamua na sasa bahari imetulia iko shwari, akimaanisha Kifo cha Magufuli ni Maamuzi ya Mungu katika Kutatua ugomvi wa Wana CCM na Membe… Akaendelea mbele na Kusema nani Kama Rais Samia Suluhu.
Ikumbukwe kuwa Huu utamaduni uliopo sasa kwa kumsifia rais hata pale anapo fanya Baya ulianza kipindi Cha Magufuli na Umeendelea hadi awamu hii kwa kusema Mama anaupiga mwingi. Nyakati za Kikwete, Mkapa hakukuwa na huu ujinga.
Turudi kwenye mada, Nape Nauye ni lini Ataacha kuwa na Kinyongo na Marehemu? Nilini ataacha Kumsema Marehemu? Huu umekuwa muendelezo wake toka Awe Waziri tena Wa Habari, Je aliteuliwa kuja Kumsema Marehemu?
Ni wakati sasa Wa Nape kumuacha Marehemu Apumzike Mahali pema na kwa amani. Asitafute chuki na watu zisizo za msingi