Nape Nnauye: Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi

Nape Nnauye: Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi

Kauli hiyo kwa wale wanaoamini katika Mungu aliye hai Milele na Milele, tokea kauli hiyo isemwe, basi tusingelikuwa tunashuhudia manung'uniko na vilio kila mahali! Badala ya kwenda Kanaani, ndio kwanza tumerudi Misri utumwani, nadhani ndiko tulikozoea! Atatokea Musa mwingine tena? Ni lini na wapi!

Mungu hawezi kuamua ugomvi halafu hali ndo ikaharibika zaidi.

Kinyume Chake ni Mungu alisikia manung'uniko yenu na kisha akaamua kuchukua mtumishi wake ili mbaki na manung'uniko yenu mliyozoea!

Kumkomboa mtu mweusi inahitaji apelekwe kwa mijeredi na marungu ya kutosha!

Sasa tuna kuelewa zaidi Magufuli
 
Serikali ya sasa haivumiliki imezidisha upumbavu wa Hali ya juu.
Si mlitaka Mama afunguwe Nchi!? Haya Sasa Nchi isha funguliwa,kila Mtanzania akatafute Muwekezaji amletee tumpee Mkataba Miaka Mia bila kikomo! Mwendazake alituchelewesha sana au siyo waadau!!??
 
Ooh yule jamaa alikuwa shetani, sasa muda wa kushuhudia shetani kamili ni nani 😀! Hakupandisha madaraja haya sasa mtapandishwa meli airport
 
Watakao mkumbuka ni wakewake tu. Mtu na akili zake timamu kamwe hawwezi abadan
Wewe hata sikuweki kwenye kundi la mafisadi maana una njaaa, wee ni ama mtu wa vyetu fyeki au kijana tu Mwalimu wa HKL ambaye hujiongezi ,unangoja kuajiriwa wakati kipaumbele ni Sayansi.
 
Kiukweli yule mzee nilikuwa simpendi lakini ndio naanza kujua kwanini alikuwa katili. Kwenye nafasi aliyokuwepo option aliyokuwa nayo ndio hiyo tu ili taifa lisonge mbele.

Hapa kwa bibi tumeshapigwa mnada.
 
Kiukweli yule mzee nilikuwa simpendi lakini ndio naanza kujua kwanini alikuwa katili. Kwenye nafasi aliyokuwepo option aliyokuwa nayo ndio hiyo tu ili taifa lisonge mbele.

Hapa kwa bibi tumeshapigwa mnada.
Hakuna mwenye nafuu hapo.Wote ni CCM.Na ndiyo wenye kuleta dhahma,dhiki na mahangaiko nchini tena kwa makusudi wakijinasibu kwamba mtawafanya nini!?Kila mmoja wao huja kwa mwendo wake ila uumizao.Kazi inabaki kichwani mwako tu.Kulia au kulilia.
 
Kiukweli yule mzee nilikuwa simpendi lakini ndio naanza kujua kwanini alikuwa katili. Kwenye nafasi aliyokuwepo option aliyokuwa nayo ndio hiyo tu ili taifa lisonge mbele.

Hapa kwa bibi tumeshapigwa mnada.
Na Huu ndio ukweli, Rais JPM hakua na uchaguzi mwingine zaidi ya kua mkoloni ,na matokeo yake tuliyaona.



Sasa angalieni, ya 2005 mpaka 2015 Yale ambayo hata mtoto Mdogo alichukizwa nayo, ndio yamejirudia.
 
Wewe hata sikuweki kwenye kundi la mafisadi maana una njaaa, wee ni ama mtu wa vyetu fyeki au kijana tu Mwalimu wa HKL ambaye hujiongezi ,unangoja kuajiriwa wakati kipaumbele ni Sayansi.
Wewe niweke kundi lolote lile, unadhani mimi huwa najali kuhusu maamuzi ya mtu tuwapo mitandaoni? Hata kunifananisha na Mwalimu wa chochote kile mimi naona unawakosea waalimu adabu kwa kunifananisha fala kama mimi na waalimu. Mimi ni sifuri kabisq
 
View attachment 2649739
Picha: Nape Nnauye

Habarini JF GT!

Jana wakati Membe akirudishiwa kadi ya CCM, Mbunge wa Mtama na Wazari wa Habari nchini aliongea kauli mbaya Sana Na Yenye kufedhehesha kwa Marehemu.

Kwa tamaduni za kitanzia Sio sawa kumsema Marehemu, na hata Ukitaka kumsema Marehemu utamsema kwa Mazuri. Lakini hii imekuwa Tofauti kabisa kwa baadhi ya Wanachama wa CCM na Viongozi wa CCM, wamekuwa Wakimsema Hayati Magufuli Hadharani mbele ya wananchi waliomchagua kwa kura nyingi. Hakika CCM inajiua Yenyewe

Jana Ndugu Nape (Namuita Ndugu kwasababu kwangu mimi sioni kama Anafaa kupewa heshima ya Jina Mheshimiwa) wakati wa Sherehe zile alisimlia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na Yeye alivyo nusurika kufukuzwa CCM na Membe kumsadia, kipindi hicho naamini Magufuli hakuwa Kiongozi mkubwa wa CCM, Nape aliongea kumaanisha kuwa Magufuli alikuwa chanzo kikubwa cha Membe kuondoka CCM na Kutengeneza ugomvi mkubwa na Wana CCM wengine.

Nape akaenda mbali zaidi na Kusema Kuwa Ugomvi huo Mungu ndio ameamua na sasa bahari imetulia iko shwari, akimaanisha Kifo cha Magufuli ni Maamuzi ya Mungu katika Kutatua ugomvi wa Wana CCM na Membe… Akaendelea mbele na Kusema nani Kama Rais Samia Suluhu.

Ikumbukwe kuwa Huu utamaduni uliopo sasa kwa kumsifia rais hata pale anapo fanya Baya ulianza kipindi Cha Magufuli na Umeendelea hadi awamu hii kwa kusema Mama anaupiga mwingi. Nyakati za Kikwete, Mkapa hakukuwa na huu ujinga.

Turudi kwenye mada, Nape Nauye ni lini Ataacha kuwa na Kinyongo na Marehemu? Nilini ataacha Kumsema Marehemu? Huu umekuwa muendelezo wake toka Awe Waziri tena Wa Habari, Je aliteuliwa kuja Kumsema Marehemu?

Ni wakati sasa Wa Nape kumuacha Marehemu Apumzike Mahali pema na kwa amani. Asitafute chuki na watu zisizo za msingi
🤣🤣
 
Back
Top Bottom