Nape Nnauye: Rais Samia Suluhu aendelee mpaka 2030

Nape Nnauye: Rais Samia Suluhu aendelee mpaka 2030

Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Moses Nnauye akihojiwa na Mwananchi amependekeza kwamba Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka 2030....
Nape na January hata wakijipendejeza vipi hawafai kuaminiwa na Rais yeyote!
 
Ajasema kama wakati ule Mungu anaweza hamua tofauti
 
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Moses Nnauye akihojiwa na Mwananchi amependekeza kwamba Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka 2030..
Huyu kifutu hana lolote, Mama yuko smart haingiliki kwa cheap politics. Alimuuza Membe kwa meko kama anauza njugu.
 
Kwa utamaduni wa CCM Rais Samia atadumu madarakani hadi 2030.

Huo ndio utaratibu Nape anakumbushia tu maana asije akaibuka Membe mwingine akaleta figisu zake 2025!
Tupo hapa!
Uzuri tekinolojia ni shahidi mzuri
 
Nape Nnauye mbunge wa jimbo la Mtama leo ameamua kufunguka liwalo na liwe.

Amesema kuwa mama Samia ni mwanasiasa mzuri tofauti na mtangulizi wake hayati Magufuli. Aidha Nape anasema kuwa mama Samia ameletwa kutufariji wakati wa msiba na ataendelea kutufariji.

Nimemnukuu Nape kama alivyosema leo.
 
"...ameletwa kutufariji wakati wa msiba na ataendelea kutufariji..."

Haya maneno mazito sana.

Nawasubiri MATAGA waje wamporomoshee matusi bwana NAPE.
 
"Mama @SuluhuSamia ni zawadi ya Mungu kwa Watanzania. Amekuja kutufariji wakati wa msiba, lakini pia ataendelea kutufariji kwa kufanya mambo ambayo kwa kweli yatakuwa ni mema kwa nchi yetu. Mama Samia ni mwanasiasa mzuri, tofauti na mtangulizi wake (Rais Magufuli)" @Nnauye_Nape
 
Hawa akina Nape na njaa zao ndio watatuvurugia Rais wetu Samia.

Huyu Nape kama aliweza kumsengenya Magufuli atashindwaje kumfitini mama yetu?

Wamakonde hawanaga misimamo!
 
Huyu mama kutaka kushindana na mwendazake ndo utakua mwisho wake kwa wengi. Hao akina nape and team walimsengenya akiwepo no wonder watasema shit hadharani asipokuwepo kabisa. Lakini wananchi tuna akili kuchanganya nani ni nani
 
Sio Wamakonde tu

Chini ya Dr Magufuli tumegundua, Wachaga, wakurya, wamasai yaani yale Makabila tuliyokuwa tunaaminishwa yana msimamo yameunga mkono sana juhudi za Mzee Mpendwa
Hawa akina Nape na njaa zao ndio watatuvurugia Rais wetu Samia.

Huyu Nape kama aliweza kumsengenya Magufuli atashindwaje kumfitini mama yetu?

Wamakonde hawanaga misimamo!
 
Aiseee yanayoendelea nchini kwetu naona aibu mimi
Nape huyuhuyu 🤣🤣🤣🤣

Haki Magu alikua Mwamba na mwiba kwa wanasiasa waliokua wamejimilikisha nchi na mamlaka ya vyama wa ndani ya CCM na nje ya CCM

Rest well our hero President John Pombe Joseph Magufuli 🕊
 
Kumsema vibaya mtangulizi wa Rais Samia ni kumsengenya Rais Samia bila kutambua hilo, hivyo busara itumike katika hilo hata kama ni suala la chuki binafsi
 
Kumsema vibaya mtangulizi wa Rais Samia ni kumsengenya Rais Samia bila kutambua hilo, hivyo busara itumike katika hilo hata kama ni suala la chuki binafsi

FPT umesahau kile kikao walichofanya kumsengenya rais John Pombe Magufuli wakati ule?
 
Back
Top Bottom