Jana nilikuwa jimboni Mtama, sehemu ambayo mwakilishi wake kwenye bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nape Moses Nnauye mwanasiasa kijana aliyewahi kuwa Mwenezi wa CCM na Waziri wakati fulani.
Akiwa kwenye mikutano yake kwa wapiga kura wa Mtama, jioni ya jana ilikuwa zamu ya Nyangao sehemu ambayo ipo kilomita chache toka makao makuu ya halmashauri ya Mtama.
Katika hali ambayo iliniacha na maswali ni namna Nape alivyokuwa anajibu maswali ya wananchi wake kwa kupeleka lawama kwa Hayati JPM.
Mfano alipotakiwa atolee maelezo kwanini zao la korosho msimu huu bei yake ghalani imekuwa ndogo Nape akaaminisha umma hayo ni matokeo ya mfumo mbovu uliotumika wakati uliopita wa Serikali kununua Korosho.
Sipo hapa kusadiki ama kutosadiki aliyozungumza Nape bali ni kuishangaa chuki ya wazi kwa Hayati JPM mwenyewe. Ningemwelewa Nape kama angesema haya ni matokeo mabovu ya serikali ya chama cha Mapinduzi badala ya kum'attack mtu ambaye hawezi kujitetea tena.
Serikali ya CCM ingali madarakani bado inao wajibu wa kueleza haya kwa wananchi wake kuliko kujificha kwenye kivuli cha hayati.
Msafiri.
Safarini Mtama.