Nape Nnauye samehe na kusahau, mwache Hayati Magufuli apumzike

Nape Nnauye samehe na kusahau, mwache Hayati Magufuli apumzike

Kinghero

Member
Joined
Jul 22, 2021
Posts
8
Reaction score
15
Jana nilikuwa jimboni Mtama, sehemu ambayo mwakilishi wake kwenye bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nape Moses Nnauye mwanasiasa kijana aliyewahi kuwa Mwenezi wa CCM na Waziri wakati fulani.

Akiwa kwenye mikutano yake kwa wapiga kura wa Mtama, jioni ya jana ilikuwa zamu ya Nyangao sehemu ambayo ipo kilomita chache toka makao makuu ya halmashauri ya Mtama.

Katika hali ambayo iliniacha na maswali ni namna Nape alivyokuwa anajibu maswali ya wananchi wake kwa kupeleka lawama kwa Hayati JPM.

Mfano alipotakiwa atolee maelezo kwanini zao la korosho msimu huu bei yake ghalani imekuwa ndogo Nape akaaminisha umma hayo ni matokeo ya mfumo mbovu uliotumika wakati uliopita wa Serikali kununua Korosho.

Sipo hapa kusadiki ama kutosadiki aliyozungumza Nape bali ni kuishangaa chuki ya wazi kwa Hayati JPM mwenyewe. Ningemwelewa Nape kama angesema haya ni matokeo mabovu ya serikali ya chama cha Mapinduzi badala ya kum'attack mtu ambaye hawezi kujitetea tena.

Serikali ya CCM ingali madarakani bado inao wajibu wa kueleza haya kwa wananchi wake kuliko kujificha kwenye kivuli cha hayati.

Msafiri.
Safarini Mtama.
 
Mimba ya Magufuli itawatesa wengi na siyo Nape tu, wapo pia akina Lema na Lisu

Muulizeni kwenye huo mfumo anaouita mbovu Korosho ilikuwa bei gani na sasa mfumo ukiwa mzuri korosho ni shs ngapi?
 
Mtoa hoja ngoja tuwe sober hapa,wewe inafikiria mh. Nape hakua mkweli alipotamka kuwa bei ya korosho imeshuka kutokana na serikali ya President Magufuri kutokusema ukweli na kuwa na mwelekeo wa bei ya korosho?its not a rocket science bei ya korosho iliathirika mno na awamu ya tano ya kuingiza siasa mno kwenye jambo hili
 
Wajuzi wa mambo wanasema kwamba:-

Ukiwa hodari wa kuvamia na kuvimeza vya wenzako vilivyo vitamu basi hata vile vilivyo vichungu huna budi kuvimeza!!

Na lau kama uchungu ukikuzidia na hivyo kulazimika kuvitema, basi usiviteme kwa chuki na hasira!!

Wakati bei ya korosho ipo juu, mkatuambia "ni kwa sababu ya Magufuli..."

Bei iliposhuka, hamkutaka tena kumhusisha Magufuli bali hivi sasa ni soko la dunia...

Narudia, ukiwa hodari wa kuvamia na kuvimeza vya wenzako vilivyo vitamu, hata vile vichungu huna budi kuvimeza!!

Hakuna jambo baya kama kuleta siasa kwenye masuala ya kiuchumi!!!
 
Huo ndiyo ukweli! Enzi za dikteta jambazi Magufuli CCM haikuwepo bali kulikuwa na Magufuli na Polepole, wengine wote waliufyata!
 
Matokeo ya majibu yake atayaona 2025 hapiti bila kupingwa!
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
---------------------------------------------
Mzilankende Aachwe Apunzike Kwa Amani
 
Back
Top Bottom