Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Nape nakushauri nenda nyumbani kwako, kisha ita waandishi wa habari waje huko ufanye Press conference hapo! Tuone kama hao polisi wanaokuzui kukutana na waandishi wa habari wataforce kuingia kwako.

Wakifanya hivyo , umoja wa vyombo vya habari ufanye kama ulivyofanya kwa Daudi Bashite kwa jeshi la polisi, hadi watawala washike adabu !

Na Utawala huu ukiendelea kunyanyasa waandishi wa habari , naye Magu awe banned! mwisho abaki na TBC yake.
 
Kutumbuliwa kwa nape na kupata suport kubwa sana kutoka kwa watu mbalimbali imeaminisha kuwa watanzania wanachuki na Mwenyekiti wa CCM na si CCM.
 
Thank to God that we actually don't have trouble in the real sense. this is just political jungle we are passing through which is meant to strengthen ourselves. Other countries have no food, water, only wars and much suffering. we enjoy our peace thanks to God
 
nikikumbuka maneno ya nape kama oil chafu, goli la mkono naye leo katumbuliwa ama kweli magu si wa mchezo mchezo.
 
Hilo ndiyo la msingi. Nitamwona angalau wa maana(siyo shujaa) kama atajivua uanachama na kuiacha Ccm. Lakini kubaki humo ni upuuzi tuu
Mkuu Kilaga napingana na wewe, nape abakie humo humo ili wapigane wenyewe kwa wenyewe wadhoofishana mpaka 2020 kazi itakuwa rahisi sana kwetu! Wasipewe nafasi ya kujipanga kabsa!
 

Nimecheka sana ,

Ila wewe ni kachochezi kadogo au bado ni ka chochezi katoto.
 
[emoji137]
 
Nape anabahati sana jamaa ndio wamemuinua juu sasa hivi ameondoka kama shujaa
 
Kupitia runinga,katika kituo cha E,nimemuona Nape Nnauye akianza kuongea kwa jazba na kumaliza kwa busara. Nape alimudu kushusha jazba zake na kufikisha ujumbe wake kwa waandishi wa habari na wengine waliokuwepo pale.

Nape alighadhabishwa na kitendo cha mtu mmoja kumtolea bastola na kumuamuru arudi garini na kuondoka badala ya kuingia kwenye Press Conference. Nape,mwanzoni, aliongea kwa hasira na uchungu mkubwa. Akazungumzia mchango wake kwa CCM na ushindi wa 2015.

Nape akasema kuwa wakati yeye analala porini kuipigania CCM,wengine kama waliotoa bastola walikuwa wakinywa bia baa. Baadaye Nape akashuka na kuzungumza kwa staha na busara. Akawaomba waandishi na vijana kuwa wazalendo na kusimamia wanachokiamini. Akasema kuwa hakuna haja ya kuivuruga nchi kwakuwa kuna mema mengi yanakuja

Akasema Nape ni mdogo,Tanzania ni kubwa. Akasema kuwa hana kinyongo na Rais wala chama chake. Akampongeza Waziri Mwakyembe na kuwataka waandishi kumuunga mkono. Akawashukuru wote na kuahidi kuwatumikia wananchi wake wa Mtama. Mwishoni,alizungumza kwa utulivu mkubwa

Hakika,ingawa mimi si mwanasiasa wala sina kadi ya chama chochote cha siasa,nimeuona ukomavu wa Nape Nnauye wa kisiasa. Alikuwa na angeweza kusema mengi kwa hasira. Lakini,akaweka akiba ya maneno. NB:Ikiwa mti mbichi umetendwa vile,itakuwaje kwa miti mikavu?

Siku njema waungwana!
 
Tanzania inawaka moto wa haki, haki imeshaanza kuwaka moto. Hima hima watanzania tuendelee kuchochea moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…