Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Ni vita kati ya wauza unga ba washiroko wao dhidi ya wazalendo akina Makonda n.k.

Mungu tuepushe na balaa hili.
 
Ni fundisho kwa wote watunge sheria ambazo zipo fair kwa watu wote, ni hatari sana kuwa na katiba inayompa madaraka makubwa sana mtu mmoja bila kuhojiwa na chombo chochote.


Ina faida na hasara zake, Maisha siyo black and white kama unavyofikiri!
 
Nape kutoka waziri hadi kutishiwa silaha tena hadharani? hii ni hatari sana.
Na hapa ndio watanzania watie akili sasa. Kama mtu aliyekuwa na nyadhifa ya uwaziri Jana tu Leo hii anatishiwa bastola kana kwamba yeye si kitu tena kwenye system, vipi wewe mwenzagu na mimi ambae hujawahi kuukwaa hata ujumbe wa nyumba kumi watakuwa wanakuchukuliaje!!

Na hili liwe fundisho kwa hawa wazee wa buku saba watambue kwamba umuhimu wao kwa huyo wanaemtetea humu daily ni sawa na herufi P kwenye term "psychology".
 
Kuna mtu unaweza ukamvamia nyumbani kwake, ukavunja mlango, ukambaka mkewe, ukamuua mwanaye, ukabeba pesa zote ukaondoka nazo, But akikukamata atakushtaki kwa kuingia sebuleni kwake na viatu.....They always miss the point and discuss trivial matters
 
Ni vita kati ya wauza unga ba washiroko wao dhidi ya wazalendo akina Makonda n.k.

Mungu tuepushe na balaa hili.
Brother this is not about wauza unga... hakuna mtu anapinga hii vita... bali ishu hapo kuvamia clouds... na mitutu kujarib kulazimisha jambo lifanyike... ndio imefanya nape kafikia hapa.
Ishu ya kuvamiwa clouds na ishu ya madawa ya kulevya vina uhusiano gani?
 
Jibu kwa hoja faida ni zipi na hasara ni zipi!


Ni mada ndefu sana na sina mood ya kuanza kuelezea hilo, lkn walioweka hivyo walikuwa na sababu, ila tambua moja tu nchi nyingi Duniani pamoja na za Ulaya zina fall back position, yaani mambo yanapoharibika kuna Kiongozi au mfumo ambayo huingilia na kuokoa nchi kusambaratika, ndiyo maana unaona hata Uingereza, Mkuu wa nchi ni Ufalme chini Malkia Elizabeti na hachaguliwi na yoyote na wala hashitakiki popote pale yuko Juu ya Sheria za Uingereza, na kama mambo yakiharibika yeye ndiyo mwenye uwezo wa kuingilia, hajihusishi na Siasa za kila siku lkn Wanasiasa wakizingua ana uwezo wa kuvunja Serikali na kuunda mpya, ...
 
Haya mahaba ya upinzani kwa Nnape yanathihirisha kuwa upinzani huwa wana ugonjwa wa kusahau haraka sana.

Dr Slaa pamoja na kupigania chadema kutoka wabunge wawili hadi wabunge 20, Slaa alivunjwa mkono pamoja na mke wake kuharibiwa mimba wakiwa Arusha.
Mwisho wa Siku Dr Slaa alifukuzwa chadema dakika za mwisho na chama kuuziwa Lowasa!!
Leo hii yote hayo chadema wamesahau wako bize kumuonea huruma Nape Nauye kada wa ccm!!

Swali la kujiuliza, tangu lini chadema na upinzani kwa ujumla wakaitakia mema CCM??
 
Ilikuw si jambo la busara... kujaribu kutumia silaha.. kwa mtu kama nape.. huyo askar amekuja na wenge balaa....
Maulid wakitenge... asante kwa kumtuliza huyo bwana mdogo....
 
Habari wa wana jamvi...
Nape waziri mahiri ulipendwa na watz wengi nakupa pole nikiwa zangu ndani ya kivuko cha misungwi nikitoka geita kwao msukuma na anko kutafuta mlo japo wa siku moja...Pole waziri wangu....
Habari za kutumbuliwa au kwa lugha ya kijanja mabadiriko ya baraza la mawaziri kwa kweli zimenishitua sana japo nilijua chochote chaweza tokea hasa kwako..na wenzio kama watatu hivi ndani ya baraza lenu pendwa...
Mh mzee wa "bao la mkono" pole...Hii dhambi yenu sasa inawatafuna na dhahiri mungu kaamua kumtumia ngosha kulidhihirisha hili(mawazo yangu).
Ccm wengi mliamib siku zote nchi yenu mtafanya mlitakalo mfn wewe hukujali watz tunataka nini ukatuambia ata kwa "goli la mkono" mtarudi ikulu.. naamini haya yanayowapata ni matokeo ya vilio vyetu kwani wengi hatuamini hii nchi kuendelea ikiwa mikonon mwenu, sababu nyie huamini katika chama kwanza nchi baadae. Mfn kipindi cha katiba mpya hamkujari kipi tulikiitaji watz wenzenu mkachukulia poa tu mkiamini mtaendelea kuwa on top..
Mh unakumbuka kipindi cha bunge live hukutaka kutusikia je io nalo sasa utatuambia nini??. Uliwai kuja jembe festival watu walikuimbia bungelive bungelive hukujali mh malipo dunian mbingun tutaenda kukamilisha torati... nadhan hata mh jk haamini kinachotokea yaaa dhambi yenu hii tuombeni msamaha watz..
Mh umebadirika ghafla mpk mwenyewe nikaanza pata waswas kipi kimekupata umeamka usingizin.. kanisan kwetu mtu akimkubari na kumkili muumba kwetu uwa sherehe... tutafanya sherehe ila mpk utuombe msamaha kwa dhambi zako waambie na wenzio mlioshiriki tutawasamehe ata kama mtabaki ndan ya ccm ila mjue tunaumia..
Mh kitendo cha wewe kutolewa bastola ni dhahiri kuwa hakuna alie juu ya mwenzio jana hukulifikilia ilo leo limekupata mh sie huku tunaumia sana japo hamjui tu .... Nadhani mmezoea kuwaona akina mdee, mnyika wenje lisu wakibughudhiwa mnachukulia poa... mh sasa io yako ya leo ni kionjo.. waulize bulaya,lowasa na sumaye vipi sasa wakoje..
Mh pole...sishangai soon hawa nao wakakufuata mwi, ma,mwa na mmoja hivi mjanja mjanja..huyu mjanja yeye zigo flan litamuelemea mh then dhambi itakua yake...
POLE MH NAPE... JAPO UANDISHI WANGU TABU MIE NILISOMA MAINJIA SASA KUANDIKA KIDOGO TABU.... POLE MH WE LOOOOOVE YU
 
In short, upinzani hawana VISASI kama boyz2kolomije
 
Ina faida na hasara zake, Maisha siyo black and white kama unavyofikiri!
Hapa ndio ugumu ulipo,madogo nowadays wanadhani serikali ni kama chumba cha bachela,ukichungulia hata dirishani unaona kila kitu,tuwe wakweli kuwa ni mengi hatuyajui na hatutaishi tuyajue hata tukijaliwa 1000yrs kuishi.
Tusipende kudandia gari mbele na tusitoe maoni kwa kila tunalosikia.Kuna wakati inalipa kushusha macho,na kuziba masikio,ukishindwa basi japo zuia kinywa kunena.
 
Haya mahaba ya upinzani kwa Nnape yanathihirisha kuwa upinzani huwa wana ugonjwa wa kusahau haraka sana.

Dr Slaa pamoja na kupigania chadema kutoka wabunge wawili hadi wabunge 20, Slaa alivunjwa mkono pamoja na mke wake kuharibiwa mimba wakiwa Arusha. Mwisho wa Siku Dr Slaa alifukuzwa chadema dakika za mwisho na chama kuuziwa Chadema!! Leo hii yote hayo chadema wamesahau wako bize kumuonea huruma Nape Nauye kada wa ccm!!

Swali la kujiuliza, tangu lini chadema na upinzani kwa ujumla wakaitakia mema CCM??
 

CCM ya Magufuli haikaa iwepo.Poleni sana.Kinyago chenu wenyewe hicho.
 
Kweli dingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…