Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Hivi hawa viongozi wa dini wapo kweli hili swala la kuonyesha silaha wanalichukuliaje au mnataka hawa watu mpaka watumie ndiyo mtoe nyaraka zenu? Juzi bashite amevamia kwa kutumia za moto mnadai ni habari za mitandao leo mmemuona yule lofa aliyekuwa anamzuia nape amewahi kuonyesha ile silaha palikuwa na haja ya kuonyesha silaha kwa tukio lile? Sasa hawa wataendelea hivi kuna siku watatumia hizi silaha. Ila mkae mkijua nguvu ya umma haijawahi kushindwa tumieni za moto ss tutatumia mawe ila mwisho wa siku ss tutashinda japo wengi tutapotea watakaobaki watatangaza ushindi. Hongera nape umethubutu
 
Mababu zetu wipigania uhuru kutoka kwa wakoloni wa kizungu na kiarabu...
Wajukuu zao tumeshindwa kupigania uhuru kutoka kwa Wasukuma wawili
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mi bado naamini Uongozi wa saivi umeshindwa na bado utaendelea kushindwa kutokana na aina ya uongozi wanayoitumia.

Tanzania ni nchi kubwa sana kieneo kiasi kwamba ni vigumu kwa stail ya uongozi wa mtu m1 kufanikiwa.Niliwahi kuposti nikisema kuwa Wateule wa Mkuu wa kaya saivi wamepoteza uelekeo hawajui wafanye nini na hawajui Bosi wao anapendelea nn.Walianza kwa mbwembwe sana ila saivi wapo kimya hawajui wafanye nn na watoke na staili gani itakayompendeza mkuu wa kaya.

Uzuri ni kwamba kuna mawaziri na baadhi ya viongozi wameanza kuchoshwa na mfumo wa Uongozi uliopo.Nape ni mmoja wao.

Kwa nchi za wenzetu walioendelea Kiongozi wa juu yako akikuingilia katika maamuzi ambayo unaamini yapo katika mamlaka yako na ukijiona upo sahihi na msimamo wako hiyo ni sababu tosha ya kujiuzulu.

Dr dalaly Kafumu ameonesha hilo.Ameshangaa kiongozi wa juu kumuingilia katika majukumu yake.Hajaona faida ya yeye kuendelea kuwa kiongozi wa kamati wakati anaingiliwa kwenye majukumu yake.

Nape kashindwa kuvumilia.Kashindwa kuona ananyanyaswa yeye abaki kimya.Alianza kuonesha msimamo wa kutokukubaliana na uongozi alipoanza kukosoa baadhi ya vitu vilivyokuwa vinaungwa mkono na mkuu wa kaya.

Nape sio waziri wa kwanza kuchukua hatua kwa wateule wa Rais.Na alijua kwa utawala huu hayupo salama kwa uamuzi aliouchukua ila amefanya kuonesha kuwa hakubaliani na kinachofanywa na Bosi wake.

Waziri wa TAMISEMI Hawa Ghasia kipindi cha kikwete aliwahi kuwasimamisha kazi Wakurugenzi wa Halmashauri walioshindwa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa na mhe. R ais aliridhia uamuzi wa waziri wake ila kwa Uongozi uliopo saivi usingekubali mana ungehisi unaingiliwa mamlaka yake.Huu ndo uongozi ambao Nape ameonesha kuutaka na asilimia kubwa ya mawaziri japo wameshindwa kuonesha kutokana na uoga waliokuwa nao.

Narudia tena Mkuu wa kaya atashindwa kwa staili ya Uongozi inampasa arudishe mamlaka kamili kwa mawaziri wake na awe tayari kusikiliza ushauri wa washauri wake na kuufanyia kazi.Aache utaratibu anaotumia sasa wa kuwashauri washauri wake.

N.B NASIKIA MHANDISI MSHAURI ANAYESIMAMIA UJENZI WA TERMINAL III JNIA AMETOA NOTISI KWA SERIKARI BAADA YA KUTOLIPWA KWA MIEZI 8.WAZIRI MKUU, WAZIRI WA UJENZI NA WIZARA YAKE WANASUBIRI MUONGOZO WA MKUU WA KAYA ILI WACHUKUE HATUA.

Kosa la Nape halimfanyi Daudi Bashite kuwa sahihi.Mkuu chukua hatua.
 
Baazi yawasanii ngada bado zinawasumbua sana wankamatwa nakuwekwa ndani nakisha wanapotoka wanaenda kwenuevyombo vyahabali kusifia kukamatwa kwao na wanashukulu mkuu wamkoa kwa kuwakamata hapondipo nilipogundua mtu ukisha kula ngada nakuanzakupoteaza akili kumbe unapopona hua akili hailudi kama zamani uchizi hubakia kichwani mwake
 
Umenena vyema. Nape wa siku za karibuni ni tofauti sana na Nape wa miaka miwili mitatu nyuma.

Kwa lugha nyepesi naweza sema Nape kakomaa kisiasa sasa na ameanza kuwa mzalendo halisi. Nahisi ndio muda mwafaka sasa wa Nape kudhihirisha ukomavu wake wa kisiasa.
 
Huyu aliechaguliwa atafanya Kazi kiuoga saana kwani km mwenzie kasimamia ukweli kapigwa chini vp na yeye atawezaje kubatle na Bashite
 
Dr Slaa alivunjwa mkono na pamoja na mke wake kuharibiwa ujauzito akiwa Arusha wakati wakitetea Chadema.

Lakini alifukuzwa dakika za mwisho na chama kuuziwa Lowasa.


Leo wako bize kumhurumia Nape!!


That is why politics is not science.

In Science the higher you go the Cooler it become, but in politics the higher you go the hotter it become.
 
Nami nasema nimgekuwa harisonee mwakabale nisinge enda kukalia kiti kilicho jawa na manumg'uniko lukuki kutoka kwa raia mpaka baadhi ya viongozi
 
Wasanii wa bongo ni wapuuzi,
Wanafiki, na suwezi waunga mkono pamoja na kazi zao ambazo hazina maadili ya kitz
 
Hii taarifa haijabalance.. mbona Hamo rapa hajaulizwa?
 
hao uliowataja huwa wanaingilia kwa maslahi yao sio kwa kwaajili ya kuokoa nchi na maslahi ya wananchi .
 
Ni heri kufia kwenye haki kuliko kufia kwenye utumwa wakati huo moyo wako hakustahili kuwa huko nape maisha ni popote na mungu anakuona wewe ni mkweli na utaendelea kuwa mkweli
 
Leo chadema wana mahaba kweli kweli na Nape.!!


Ama kweli kuwa kichwa panzi ni gharama kubwa maishani
 
Kipanya anawakilisha mawazo ya wengi sana!
Ndugu yetu Nape una haraka ya kwenda wapi?
NIMESIKITISHWA NA SAKATA LOTE, LAKINI KILICHONIKWAZA ZAIDI NI UKOSEFU WA SUBIRA ......!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…