Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Makonda --- Magufuli --- Makonda --- Hapi --- SSP Maisha yana endelea.
 
Unamsifia lakini alivyowafungia binge mlimtukana sana, alivyomtusi Lowassa wenu mlimsema maneno yote ya hovyo eti leo mnamwita shujaa wenu. Mnapoteza dira
Kazi yetu ni kuleta ukombozi kwa waTz wote ikiwa ni pamoja na wasiojielewa kama wewe. Kwa hivyo kila tunapoweza kulikomboa gamba moja (hata kimtazamo tu, sio lazima avae gwanda) hilo kwetu ni mafanikio makubwa na ni sherehe. Huyu aliyekuwa jemadari wa magamba, leo hii anazungumza 'dhambi kubwa duniani ni wogo, vijana msiwe waoga' - unataka ukombozi gani zaidi ya hilo. Kujivua ugamba (kifikira) ni USHUJAA, ni UKAMANDA.
 
Nape amesoma Public Adminidtration pale Mzumbe. Wenzie hawana hata cheti cha form four, ndio maana kila mtu anajiongozea anavyojua na wanapishana katika kazi zao
 
Hiyo ya mwisho ndo nimeipenda,,amin amin nakwambia mda unakuja hawa watu watatoa mabom
 
Ni zaidi ya miezi miwili sasa tangu kuanza kuzagaa kwa habari kuhusu utata wa elimu ya kidato cha nne ya bwana Makonda ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Kama inavyosemekana makonda alitumia cheti cha kidato cha nne cha bwana Paul Christian baada ya yeye RC Makonda (wakati huo akiitwa Albert Bashite) kupata division 0. Kughushi Cheti hicho ambapo kisheria ni kosa la jinai ndio kimemsaidia kupata fursa mbalimbali kielimu na kiuongozi mpaka hapa alipo leo.

Ni wakati mwafaka mawaziri hawa ambao ndo wanaosimamia masuala ya elimu na Utumishi kutoka hadharani na kutujulisha umma wa Watanzania juu ya ukweli wa jambo hili kama hatua aliyochukua Mheshimiwa Nape mara baada ya Chombo cha habari kuvamiwa. Ni vema hawa mawaziri wakaanzisha uchunguzi na kutoa taarifa juu ya utata wa elimu ya Bwana Makonda, kwani huyu ni mtumishi wa Umma tena ni Mkuu wa jiji kubwa kuliko yote nchini, kwa maana hiyo jiji hili lazima liongozwe na kiongozi aliye na sifa stahili hususani kielimu. Na ifahamike wazi kuwa maelfu ya watumishi wa umma kama alivyo makonda wamefukuzwa Kazi Na kufunguliwa mashitaka kwa kosa la kughushi vyeti vya elimu.

Wito wangu kama mawaziri watashindwa kutupa ukweli wa suala hili basi watangaze kuwa watumishi wote waliofukuzwa kazi Kwa kosa la kughushi vyeti warudishwe makazini kwani hata wao walikuwa wachapa kazi mahili kuliko hata Makonda, pia hawa mawaziri inabidi wajipime uhalali wao wa kuendelea na nafasi zao za uwaziri kwa kushindwa kutimiza wajibu wao Na ikibidi wajiuzulu na kuwaomba radhi watumishi waliowafukuza kazi kwani nchi hii hatuna double standard.

Zoezi la uhakiki wa Vyeti lilihusu watumishi wote wakiwemo wakuu wa mikoa, sasa kuna tatizo gani kutoa taarifa ya uhakiki wa vyeti vya bwana Makonda? Watujibu hawa mawaziri na kama hawawezi wajiuzulu Kwa maslahi ya Umma, kwani hawakuzaliwa ili wawe mawaziri, wapisheni watu watakaokuja kutupa majibu ya hoja hii.
 
nilimsikia akisema au unataka niseme? inaonekana kuna siri kubwa sana na sijui kitu gani alitaka tuseme
 
Liuzi lote hilo ni la sizonje?
 
Sidhani kama watathubutu! Uprofesa tu alionayo mmoja wao unaleta kigugumizi kikubwa! Anapata wapi nguvu ya kuzibua mtaro wa maji chafu wa Cheti cha Bashite!
 
"..., rafiki yangu Lowassa anadhani ikulu ni wodi ya wagonjwa.., (ovyo).., anadhani ikulu wodi ya wagonjwa, na wenzake akina Mbowe.., wakamdanganya, lakini kila akiuangalia muziki wa CCM, breki za mwili zinaendelea kulegea.., ndio maana mambo yake yanaharibika ovyo.., la kwanza kubwa, watanzania hatutaki Rais wa majaribio, hatuwezi kuwa na Rais wa majaribio, Rais ambaye tukimwambia akakague majeshi yetu hawezi huyo hafai...., juzi nilikuwa Mbeya, vijana wale wakapiga Push-ups, nikauliza yule Fisadi anaweza.., wakasema atajisaidia jukwaani achana nae...."

- Nape Moses Nnauye, Iringa, Mkutano wa kampeni za CCM, 28.09.2015
 
Hahaaaa....vibaya hivyo kaka...yaani sio freshi kabisa[emoji23]
 
Nukuu za Nape za siku za nyuma hazitafuta ukweli kwamba JPM yupo tayari kutumbua wanaotetea utendaji bora na kuacha majambazi kama Daudi Albert Baashite!! Kwahiyo ahsante kwa kutukukumbusha lakini ukweli unabaki pale pale; JPM hana lolote zaidi ya kutaka watu wamuamini kwamba anapinga vita ufisadi wakati ni mlinda mafisadi wakubwa kwenye nchi hii na ndio maana hadi leo pamoja na kelele zake hajapeleka mahakamani fisadi hata mmoja zaidi ya ku-deal na watumishi wa umma!!!

Grand corruption inayofanywa na wanasiasa ameifumbia macho mamoja!!! Hadi leo ni yeye na watu wake ndio wanafahamu mchakato wa kununua Bombardiers umefanyika fanyika vipi na wapi zabuni zilitangazwa!!!!
 
Bado Nape ni jasiri!
Alimsimamia raisi aliyeamini anafaa, na alipoona hafai hakuwa mnafiki kubaki naye, alimuweka Ikulu na amempinga ndani ya mwaka mmoja! angeweza kuwa mnafiki na kubaki kimya ili awe salama muda wote! toka raisi alipokuwa anakosea, taratibu Nape alijionesha kuwa hayuko pamoja, ni mwezi sasa au Zaidi taratibu Nape alikuwa anatweet kuashiria kuwa hali si shwari, I do believe kuwa alionywa lakini bado alisimamia kilichokuwa ni haki kwake!

Kazi iliyofanywa na Nape mwezi huu huwezi hata kuilinganisha ile aliyoifanya mkuu wa kambi ya upinzani ambaye alipekuliwa hadi chumbani yet akawa mpole!
 
Ss si alikuwa kwenye campain we ulitaka aponde chama chake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…