Jiulize ni kwanini Kenya yupo mbali sana kuliko sisi, jiulize ni kwanini Kenya, Nigeria, Uganda, Ghana nk wana raia wengi nchi za nje hasa Ulaya na Marekani, Jiulize ni kwanini wa Kenya wengi wapo kwenye Mashirika ya kimataifa ikiwa ni pamoja na UN.
Siseme kujua kiingereza ndio akili, la hasha bali kuijua hiyo lugha inakufanya ufunguke kiakili zaidi na kifikra, inakufanya uwe mjanja zaidi tofauti na kuwa msomi usiyejua Kiingereza vema ina maana utakuwa umeji limit na utakuwa mjanja wa hapahapa tu. Hivi unajua ni kwanini wasomi wetu wa Sheria ni wa hapahapa tu, hebu mchukuwe wakili wa kibongo akakutetee kwenye mahakama za ughaibuni.
Jiulize ni kwanini wahindi wametapakaa kila kona duniani, jiulize ni kwanini wa hindi waliopo hapa Bongo wanahakikisha watoto wao wanajua kiingereza vizuri nafasaha kuliko kiswahili.
MNATAKA TUJIFUNGIA KAMA KOREA KASKAZINI.
Mnataka wachezaji wetu waendelee kutapeliwa kusaini mikataba feki(Fei toto).