Napenda sana majirani wa aina hii

Napenda sana majirani wa aina hii

Aiseeeee habari za leo wazee.........

Huyu jirani yangu ana watoto wawili mmoja yuko darasa la tano mwingine yuko darasa la pili, ni mdada wa makamo shughuli yake kuu ni kupika vitafunwa asubuhi na kuzungusha Kwa wateja wake. Shughuli zake zingine sizijui na huwa sizifwatilii kabisa.

Hawa watoto wake ni wanagombanaga vibaya mnoo, kama mnavyojua watoto wa kiume wakifwatana wanakuwaga na mtiti ni balaa.

Sasa bwana huyu mkubwa huwa anamtandikaga sana huyu mdogo japokuwa haka kadogo kana hasira hatari ila ndiyo hivyo kwakuwa ni kadogo huwa kanapewa sana kichapo na kaka yake na marayingi nikiwakuta wanagombana huwa namkoa makwenzi huyu mkubwa maana anamdundaga sana sana huyu mdogo wake.

Juzi jumamosi asubuhi wakati mama yao kaenda kuzungusha vitafunwa huko madogo wakaanza kugombana tena wanagombana nje nikatoka kama kawaida nikamkoa makwenzi yule mkubwa akaanza kulia, ile analia mama yao akaja kuulizwa nini dogo akasema huyu anko kanipiga, nikamweleza mama yao kuwa huyu mkubwa anampigaga sana huyu mdogo hivyo nilikuwa namuonya watakuja kuumizana hawa.

Ebwana yule dada si akaanza kuniwashia moto.... Akasema usije kumpiga mtoto wangu hata mmoja na hata hata ukiwakuta wanauana waache usinipigie wanangu Babu weee... Tena komaa.

Duuu mbele za majirani nikakaa kimya ila wakamuonya kuwa kauli yake sio nzuri yeye akakomaa niàcheni watu tukasema poa.

Sasa jana wakati kaenda kuzungusha vitafunywa huko huku madogo wakaanza kukung'utana Mimi nipo zangu nje nafua nikawaacha kama siwaoni, mdogo kapigwa kalia weeee kaka mtu akajua ameshinda sasa kaka mtu akajisahau kumbe dogo kaenda ndani kabeba kisu kamvizia kaka yake kamdomeka kisu cha jicho tena kilizama kabisaa dogo akaanza kupiga makelele pale uso mzima umejaa damu tupu.

Majirani wengine hawakuwepo Mimi na jirani mmoja ni mdada alikuwa kalala ila Kwa Yale makelele ikabidi aamke kutoka tu anakutana na hicho kisanga anataka kwenda kumuhudumia yule dogo nikampga mkwara rudi ndanii.. unakumbuka mama yao juzi alisemaje? Demu akakumbuka akarudi ndani Mimi huyo naendelea kufua majinzi yangu pale huku naendelea kuburudika na kilio cha uchungu toka kwa yule dogo.

Mama yao anarudi anakuta dogo anagalagala chini damu uso mzima na kisu bado kimetulia palepale jichoni alafu mjuba nipo pale kimyaa naendelea kuanika nguo zangu... Yule dada akaanza kupiga makelele pale huku akilia ananilaumu eti Kwa nini watoto wanaumizana vile alafu nipo hata sishtuki na sijachukua hatua yoyote!!!

Kwa kauli aliyonitolea juzi kuhusu wanae nikasema hapa nikimjibu naweza nikatwa na hasira nikamtia ngumi buure, sikumjibu kitu,.. nikamkata jicho eeweeeeee.... Nikaaendelea kuanika nguo zangu akazidi kulia yule dada anashindwa kile kisu akitoeje pale jichoni, nikamkata tena jicho kali saaana nikamalizia kuanika nguo zangu nikaingia geto nikaoga nikatoka namkuta bado analia akiomba msaada nikamkata tena jicho la kibandidu mbaya mbovu nikaamsha zangu kuelekea mtaani.

Jana toka nilivyotoka geto pale sikurudi kabisa huwa sipendagi sana makelele ya kipuuzi puuzi. Nilienda zangu lodge nikaita manzi flani nikaagiza valeur kubwa na kitimoto kilo moja na nusu tukapiga tukafanya yetu muda huu ndo naamka ndiyo nikakumbuka kile kisanga cha Jana pale geto nikacheka saaana hahahahahaha.

Haya maisha hayahitaji mpuuzi mmoja akupigie makelele ya hovyo hovyo tu.
Naweza kusema bila shaka kuwa kwa ulichokiandika (kama ni kweli) basi wewe huna akili na huyo mama mwenye watoto hana akili, yaani mmekutana mazoba. Kwa nini? Watoto wanafundishwa kwa kuwaonyesha upendo. Yaani wakipigana wewe badala ya kumpiga mmoja, unatakiwa uwafundishe jinsi ya kuishi kwa upendo. Kuwapiga inawafanya nao wazidi kuwa wagomvi kwa sababu ni kama unawafundisha ugomvi huamuliwa kwa ugomvi na wanakuwa wanawekekeana visasi muda wote. Kingine, hao wote walikupa ''likes'' nao ni wajinga.
 
Iwe chai au mtindi hii habari inataka kufanana na tukio langu moja
Watoto Wana michezo ya kipuuzi sana Kuna mchezo unaitwa mbong'oko yaani ukiinama tu mwenzio uliyepinga naye mchezo anakuja kukukita au kukupiga teke la matako

Jirani hivyo hivyo watoto wake na michezo yao ya kijinga wakawa wanafanya Kuna siku niliwakamata nikawafinya ngozi ili waache wakaenda kusema eti nimewapiga mama yao wacha anijie juu, Mimi nikajawa na hasira kifuani nikaachana nao siku ya siku mmoja akamkita mwenzie akadondokea kwenye shimo lililochimbwa kwa ajili kalo akavunjikabl mkono mi nikasema hatawi hayawi yametimia huyo mama ndo anajifanya kumchapa mtoto aliyemuumiza mwenzio
Mi hata pole sikumpa na hatukuongea tangu kipindi hiki hadi nahama mtaa
Hivi hakuna njia nzuri zaidi ya kufundisha mtoto bila kumpiga? Unaonaje ungewaelimisha kwa upendo? Huoni kuwa wangekuona ni maana na kukuheshimu?
 
Kwenye malezi katika rika la utoto kupigwa au kuadhibiwa hakukwepeki ni muhimu sana kumkanya mtoto mtukutu na kipigo kinyume chake unatengeneza bomu kubwa sana Mimi ni mzazi na mlezi najua ninachokifanya

Labda kama hujawahi kulea ndo huwezi kuelewa hili jambo
Hivi hakuna njia nzuri zaidi ya kufundisha mtoto bila kumpiga? Unaonaje ungewaelimisha kwa upendo? Huoni kuwa wangekuona ni maana na kukuheshimu?
 
Kwenye malezi katika rika la utoto kupigwa au kuadhibiwa hakukwepeki ni muhimu sana kumkanya mtoto mtukutu na kipigo kinyume chake unatengeneza bomu kubwa sana Mimi ni mzazi na mlezi najua ninachokifanya

Labda kama hujawahi kulea ndo huwezi kuelewa hili jambo
Kwa taarifa yako mimi nimeishi kwenye nchi ambazo watoto hawachapwi na ukimchapa mtoto ni kosa la jinai na watoto wa hizo nchi ukubwani wanakuwa na akili na adabu kuliko hao wewe unaowatandika bakora. Kama wewe ni mzazi na unatandika watoto wako ukidhani ndiyo watakuwa na tabia njema basi unajidanganya. Huwezi kujiuliza kwa nini huku kwetu tunachapa watoto lakini ukubwani wanapofanya kazi wanakuwa madaktari makatili. viongozi mafisadi, wanafunzi machangudoa, vijana waporaji na kila aiana ya unyama ambao sehemu ambazo hawachapi watoto huwezi kuona?
 
Boss mzma wewe
Samahani ivi mzazi wako ndio akiwa anataka kujipiga kitanzi watu wakamwona akawaambia niacheni utapenda wamwache au wamdhibiti asijipige kitanzi
 
Mtoa mada kwenye jicho kazidisha chumvi sana[emoji23][emoji23]..ila kama ni single maza sishangai maana wana malezi ya kipuuzi sana!
 
Umezingua sana , umekosea sana utakuja kuelewa siku za mbele.
 
Kwa taarifa yako mimi nimeishi kwenye nchi ambazo watoto hawachapwi na ukimchapa mtoto ni kosa la jinai na watoto wa hizo nchi ukubwani wanakuwa na akili na adabu kuliko hao wewe unaowatandika bakora. Kama wewe ni mzazi na unatandika watoto wako ukidhani ndiyo watakuwa na tabia njema basi unajidanganya. Huwezi kujiuliza kwa nini huku kwetu tunachapa watoto lakini ukubwani wanapofanya kazi wanakuwa madaktari makatili. viongozi mafisadi, wanafunzi machangudoa, vijana waporaji na kila aiana ya unyama ambao sehemu ambazo hawachapi watoto huwezi kuona?
Oya Babu! we endelea na hizo nchi zako lakini sisi ni wabantu na hizi taratibu ndiyo zinazoufanya jamii yetu leo kuwa bora na ngangali kiustawi wa jamii

Hakuna jamii zenye ustawi mzuri kama za afrika na Asia hata wazungu wenyewe wanathibisha hilo wanatamani sana makuzi ya huku

Wewe kama umevutiwa na ustaarabu wa huko huo ni mpango wako hakuna anayekuzuia na sisi tuache na taratibu zetu halafu mwisho wa siku kila mtu avune alichopanda
 
Back
Top Bottom