Napenda sana majirani wa aina hii

Napenda sana majirani wa aina hii

Hawa jamaa Wa valeur na kitimoto wanamambo ya hovyo sana. Yani watoto wanauwana wewe unafua jeans zako. Wewe jamaa roho mbaya sana.
Jamaa hana baya, si kafata tu ushauri wa yule mama kwamba usithubutu kuwagusa wanawe
 
Hahaha! Nitashangaa sana kama kuna mtu atachukulia hii story seriously.

Sababu technically jicho ni sehemu sensitive sana yenye mishipa mingi ya fahamu kutokana na kuwa connected directly na ubongo. Hivyo realistically kwenye situation kama hiyo, kisu kikipita na kuzama ndani ya jicho, huyo dogo wala asingepiga kelele wala kulia, angezima kimyakimya kwa kupoteza fahamu mara moja na kudondoka kama kiroba cha viazi. Sababu maumivu yake sio mchezo. Angetoka damu nyingi na kufa hapohapo chini ya dk 15.

Na wewe ungeshitakiwa kwa kuwa shahidi na kutofanya chochote, mbaya zaidi ungeenda jela kwa kusaidia kifo cha huyo mtoto kwa kitendo chako cha kumkataza huyo jirani yako kutoa msaada. Ungekuwa mahabusu sasa hivi na hii story isingekuwemo humu.

Anyway, kwenye upande wa utunzi story nitasema ni 6/10. Una safari ndefu kama nia ni kutunga realistic stories. Unless hii ni dark comedy. Which is funny kama wewe ni shabiki wa American Pyscho ya mwaka 2000.

"Now, let's see Paul Allen's card?"
 
Muda sasa wa kumburuza mahakamani mleta maada
1. Maudhui yake yameniathiri kisaikolojia

2. Amejaribu kusababisha kifo

3. Kasababisha maumivu makali kwa mtoto
 
Mkuu una roho mbaya,kwanza kitendo cha wewe kumpiga makwenzi kaka yake badala ya kuamua na kuwaelekeza inaonyesha wewe una shida mahala,Pili mtoto amechomwa kisu cha jicho upo hapo unafua nguo eeeh!Badilika wanaume hawana tabia hizo
 
Mitoto aliyeisema jana kishimba

Watoto wanaopatikana baba zao kwa kujumua uji wa mama zao ndoshida kila toto na babake

Akome ,mama na mdogo mtu wamekomeshwa na dogojanja
 
Watoto wa siku hizi ukitaka hata kumtuma dukani chapu lazima umuombe ruhusa mama yake, anyway hpo kwenye kisu cha jicho imetufunga kamba.
Hata mm nimeshtukia. Hapo amekoleza uzi aisee! Kisu hakiwezi kukaa jichoni wakati dogo anapiga kelele huku majirani wengine wapi wasitoe msaada. Hili haliwezekani. Hapa katia chumvi aisee!
 
Mkuu una roho mbaya,kwanza kitendo cha wewe kumpiga makwenzi kaka yake badala ya kuamua na kuwaelekeza inaonyesha wewe una shida mahala,Pili mtoto amechomwa kisu cha jicho upo hapo unafua nguo eeeh!Badilika wanaume hawana tabia hizo
Mkuu hii ni fiction isikuumize kichwa aisee!
 
Aiseeeee habari za leo wazee.........

Huyu jirani yangu ana watoto wawili mmoja yuko darasa la tano mwingine yuko darasa la pili, ni mdada wa makamo shughuli yake kuu ni kupika vitafunwa asubuhi na kuzungusha Kwa wateja wake. Shughuli zake zingine sizijui na huwa sizifwatilii kabisa.

Hawa watoto wake ni wanagombanaga vibaya mnoo, kama mnavyojua watoto wa kiume wakifwatana wanakuwaga na mtiti ni balaa.

Sasa bwana huyu mkubwa huwa anamtandikaga sana huyu mdogo japokuwa haka kadogo kana hasira hatari ila ndiyo hivyo kwakuwa ni kadogo huwa kanapewa sana kichapo na kaka yake na marayingi nikiwakuta wanagombana huwa namkoa makwenzi huyu mkubwa maana anamdundaga sana sana huyu mdogo wake.

Juzi jumamosi asubuhi wakati mama yao kaenda kuzungusha vitafunwa huko madogo wakaanza kugombana tena wanagombana nje nikatoka kama kawaida nikamkoa makwenzi yule mkubwa akaanza kulia, ile analia mama yao akaja kuulizwa nini dogo akasema huyu anko kanipiga, nikamweleza mama yao kuwa huyu mkubwa anampigaga sana huyu mdogo hivyo nilikuwa namuonya watakuja kuumizana hawa.

Ebwana yule dada si akaanza kuniwashia moto.... Akasema usije kumpiga mtoto wangu hata mmoja na hata hata ukiwakuta wanauana waache usinipigie wanangu Babu weee... Tena komaa.

Duuu mbele za majirani nikakaa kimya ila wakamuonya kuwa kauli yake sio nzuri yeye akakomaa niàcheni watu tukasema poa.

Sasa jana wakati kaenda kuzungusha vitafunywa huko huku madogo wakaanza kukung'utana Mimi nipo zangu nje nafua nikawaacha kama siwaoni, mdogo kapigwa kalia weeee kaka mtu akajua ameshinda sasa kaka mtu akajisahau kumbe dogo kaenda ndani kabeba kisu kamvizia kaka yake kamdomeka kisu cha jicho tena kilizama kabisaa dogo akaanza kupiga makelele pale uso mzima umejaa damu tupu.

Majirani wengine hawakuwepo Mimi na jirani mmoja ni mdada alikuwa kalala ila Kwa Yale makelele ikabidi aamke kutoka tu anakutana na hicho kisanga anataka kwenda kumuhudumia yule dogo nikampga mkwara rudi ndanii.. unakumbuka mama yao juzi alisemaje? Demu akakumbuka akarudi ndani Mimi huyo naendelea kufua majinzi yangu pale huku naendelea kuburudika na kilio cha uchungu toka kwa yule dogo.

Mama yao anarudi anakuta dogo anagalagala chini damu uso mzima na kisu bado kimetulia palepale jichoni alafu mjuba nipo pale kimyaa naendelea kuanika nguo zangu... Yule dada akaanza kupiga makelele pale huku akilia ananilaumu eti Kwa nini watoto wanaumizana vile alafu nipo hata sishtuki na sijachukua hatua yoyote!!!

Kwa kauli aliyonitolea juzi kuhusu wanae nikasema hapa nikimjibu naweza nikatwa na hasira nikamtia ngumi buure, sikumjibu kitu,.. nikamkata jicho eeweeeeee.... Nikaaendelea kuanika nguo zangu akazidi kulia yule dada anashindwa kile kisu akitoeje pale jichoni, nikamkata tena jicho kali saaana nikamalizia kuanika nguo zangu nikaingia geto nikaoga nikatoka namkuta bado analia akiomba msaada nikamkata tena jicho la kibandidu mbaya mbovu nikaamsha zangu kuelekea mtaani.

Jana toka nilivyotoka geto pale sikurudi kabisa huwa sipendagi sana makelele ya kipuuzi puuzi. Nilienda zangu lodge nikaita manzi flani nikaagiza valeur kubwa na kitimoto kilo moja na nusu tukapiga tukafanya yetu muda huu ndo naamka ndiyo nikakumbuka kile kisanga cha Jana pale geto nikacheka saaana hahahahahaha.

Haya maisha hayahitaji mpuuzi mmoja akupigie makelele ya hovyo hovyo tu.
Kama sio chai basi akili zako n kama jicho lenyewe
 
Ukitaka kumlea mtoto wa jirn ni lazima ujipange kuvuna lawana kulik shukulan especially ukiwa una hela jamii inakua aipokei hekima zako bali wanaona kelele
 
Mbali na kwamba hii chai haina sukari mwamba una roho ya DP World
 
Uyo mwanamke mpuuzi enewei ndo ilivyo mjanamke isioishi na mume hao watot hawajakutana na mimi watot wanaoonewa huchoka kinachofuata mnyonge atashinda tu one day , so mi huwa nawaleta pamoja yule mkubwa nampa onyo sometimes wadogo huwa wakorofi nae nampa onyo wakirudia ni kipigo wote hasa yule mkubwa
 
Back
Top Bottom