Napenda sana majirani wa aina hii

Napenda sana majirani wa aina hii

Kaka hili utalilipia kwa kujua Au bila kujua.
Una bahati hakuna kifo hapo.
Huwezi Acha watoto wanaumizana eti kisa mama Yao alikufokea.Wanawake wanahasira za karibu sanaa anaweza akatamka neno hapo na asiwe amemaanisha. Wanawake ni wagumu sana kuomba msahaha pia ujue Hilo ni nature yao.
Hukupaswa pia kumpiga yule mtoto mkubwa Makonzi, ulipaswa kuchukua nafasi ya baba hata Kama wale sio wanao.Ungewaita na kwenda nao dukani ukawanunulia pipi ukaanza kusema nao wapendane,Ungemsihi mkubwa amlinde mdogo wake na mdogo amlinde mkubwa ungebarikiwa mno.Kutoa adhabu ulizidisha chuki kwa watoto hawa.

Unapata wapi ujasiri watoto wanaumizana wewe unaenda kufanya uzinzi?hapo kwenye tendo la ndoa ulilofanya ikitokea mimba imetunga unafikiri mtoto atakua na Roho gani.
Omba Toba kaka kwa Mungu

Samahani kama nimekukwaza pia.
What a marvelous comment
 
Chief naomba kwanza nikwambie wewe ni mpumbavu mmoja mkubwq sana!

Kwahiyo maneno ya mama yao kwa situation hiyo yana uzito gani,,,kweli unashindwa kuchanganua mambo nakuona ni msaada upi ulihitajika kwa huyo malaika wa mungu?

Halafu unaona fahari kuongea huo upuuzi kuwa ulienda sijui wapi na kupata kinywaji na dem wako!

Ovyo kabisa!
Kwahiyo mama yao hakuona umuhimu wa msaada wa makonzi anayotoa jamaa? Huyo jamaa angeenda kusaidia pale, mama mtu angesema jamaa ndiye kamchoma mtoto kisu kisa kuna historia ya makonzi kupigwa
 
Uwanunulie Pipi? Alafu baadaye wakiumwa tumbo mama yao aseme umewalisha uchafu.

Kumbe Baba atakiwi kutoa adhabu? Kumbe Baba akitoa adhabu amazidisha chuki baina ya watoto?

Alafu nature nature nature, hiyo kauli ndipo wanapojificha. Kila binadamu ana wajibu wa kujifunza mambo, kijirekebisha.
Inategemea Kama wewe ni mwanaume au mvulana.

Wacha nikupe somo luch time iende vyema.

Hatukatai kutoa Adhabu ila Binadam wana mapumgufu na magonjwa,unaweza piga konzi mtoto wa watu akanyooka. hivyo alipaswa kutumia mbinu mbadala kama mwanaume (Babà) sio mvulana.

Ungemtuma Yule mdogo kwenda kununua pipi pipi kisha ukawasemesha kama watoto wako.

hapo ungejua kisa cha hao ndugu kugombana na ukawapatanisha

Ukamwambia mdogo amgawie pipi yule mkubwa.

Swala la kuumwa Tumbo lipo tuu Au lingetokea Mungu angekua upande wako kwakua hukuwa na jambo baya dhidi ya malaika hawa.
 
Kuna watoto kama wana laana yani wanapenda ligi tu hawakubali kushindwa. Hasa watoto wa kwanza hujiona wao ni sehemu ya wazazi hivyo ku exercise ukubwa kwa wadogo zao wakati wote ni watoto hukutana na upinzani mkali sana. Matokeo yake ni ngumi za hapa na pale na bila uangalizi huishia kuumizana vibaya.

Sometimes sababu ni za ujinga tu unakuta wanagombania kitu tu. The best way ni kumfundisha mkubwa ku give in kumuachia mdogo wake kwa upendo. Itakuwa inamuuma ila atazoea kuwa kumpa priority mdogo wake ni swala la upendo na sio unyonge.
 
Hiyo issue ya kutoa kitu cha kula kwa watoto wa wenzio iliwapeleka jirani mpaka polisi. Mama mtoto nasema jirani yake kawapa uchafu kumbe jirani huyo alisaidia tu.

Mtoa post kasema hao watoto wanagombana mara kwa mara, ina maana walishakanywa, mama yao alishaambiwa ila bado watoto hawasikii. Sawa jamaa alizingua kumpiga sababu nayo ni mbaya, hajui historia ya kiafya kwa hao watoto.
 
Aiseeeee habari za leo wazee.........

Huyu jirani yangu ana watoto wawili mmoja yuko darasa la tano mwingine yuko darasa la pili, ni mdada wa makamo shughuli yake kuu ni kupika vitafunwa asubuhi na kuzungusha Kwa wateja wake. Shughuli zake zingine sizijui na huwa sizifwatilii kabisa.

Hawa watoto wake ni wanagombanaga vibaya mnoo, kama mnavyojua watoto wa kiume wakifwatana wanakuwaga na mtiti ni balaa.

Sasa bwana huyu mkubwa huwa anamtandikaga sana huyu mdogo japokuwa haka kadogo kana hasira hatari ila ndiyo hivyo kwakuwa ni kadogo huwa kanapewa sana kichapo na kaka yake na marayingi nikiwakuta wanagombana huwa namkoa makwenzi huyu mkubwa maana anamdundaga sana sana huyu mdogo wake.

Juzi jumamosi asubuhi wakati mama yao kaenda kuzungusha vitafunwa huko madogo wakaanza kugombana tena wanagombana nje nikatoka kama kawaida nikamkoa makwenzi yule mkubwa akaanza kulia, ile analia mama yao akaja kuulizwa nini dogo akasema huyu anko kanipiga, nikamweleza mama yao kuwa huyu mkubwa anampigaga sana huyu mdogo hivyo nilikuwa namuonya watakuja kuumizana hawa.

Ebwana yule dada si akaanza kuniwashia moto.... Akasema usije kumpiga mtoto wangu hata mmoja na hata hata ukiwakuta wanauana waache usinipigie wanangu Babu weee... Tena komaa.

Duuu mbele za majirani nikakaa kimya ila wakamuonya kuwa kauli yake sio nzuri yeye akakomaa niàcheni watu tukasema poa.

Sasa jana wakati kaenda kuzungusha vitafunywa huko huku madogo wakaanza kukung'utana Mimi nipo zangu nje nafua nikawaacha kama siwaoni, mdogo kapigwa kalia weeee kaka mtu akajua ameshinda sasa kaka mtu akajisahau kumbe dogo kaenda ndani kabeba kisu kamvizia kaka yake kamdomeka kisu cha jicho tena kilizama kabisaa dogo akaanza kupiga makelele pale uso mzima umejaa damu tupu.

Majirani wengine hawakuwepo Mimi na jirani mmoja ni mdada alikuwa kalala ila Kwa Yale makelele ikabidi aamke kutoka tu anakutana na hicho kisanga anataka kwenda kumuhudumia yule dogo nikampga mkwara rudi ndanii.. unakumbuka mama yao juzi alisemaje? Demu akakumbuka akarudi ndani Mimi huyo naendelea kufua majinzi yangu pale huku naendelea kuburudika na kilio cha uchungu toka kwa yule dogo.

Mama yao anarudi anakuta dogo anagalagala chini damu uso mzima na kisu bado kimetulia palepale jichoni alafu mjuba nipo pale kimyaa naendelea kuanika nguo zangu... Yule dada akaanza kupiga makelele pale huku akilia ananilaumu eti Kwa nini watoto wanaumizana vile alafu nipo hata sishtuki na sijachukua hatua yoyote!!!

Kwa kauli aliyonitolea juzi kuhusu wanae nikasema hapa nikimjibu naweza nikatwa na hasira nikamtia ngumi buure, sikumjibu kitu,.. nikamkata jicho eeweeeeee.... Nikaaendelea kuanika nguo zangu akazidi kulia yule dada anashindwa kile kisu akitoeje pale jichoni, nikamkata tena jicho kali saaana nikamalizia kuanika nguo zangu nikaingia geto nikaoga nikatoka namkuta bado analia akiomba msaada nikamkata tena jicho la kibandidu mbaya mbovu nikaamsha zangu kuelekea mtaani.

Jana toka nilivyotoka geto pale sikurudi kabisa huwa sipendagi sana makelele ya kipuuzi puuzi. Nilienda zangu lodge nikaita manzi flani nikaagiza valeur kubwa na kitimoto kilo moja na nusu tukapiga tukafanya yetu muda huu ndo naamka ndiyo nikakumbuka kile kisanga cha Jana pale geto nikacheka saaana hahahahahaha.

Haya maisha hayahitaji mpuuzi mmoja akupigie makelele ya hovyo hovyo tu.
Chai,kisu kikae jichoni masaa yote hayo
 
Hiyo issue ya kutoa kitu cha kula kwa watoto wa wenzio iliwapeleka jirani mpaka polisi. Mama mtoto nasema jirani yake kawapa uchafu kumbe jirani huyo alisaidia tu.

Mtoa post kasema hao watoto wanagombana mara kwa mara, ina maana walishakanywa, mama yao alishaambiwa ila bado watoto hawasikii. Sawa jamaa alizingua kumpiga sababu nayo ni mbaya, hajui historia ya kiafya kwa hao watoto.
Kaka hii dunia sio mbaya sana kama unavyosema. nikuulize swali?

Kipi bora kuwanunulia pipi hao watoto ukawapatanisha wakaharisha alafu ukapelekwa polisi na mama Yao au
Watoto kuchomana visu?
 
Hap
Kuna watoto kama wana laana yani wanapenda ligi tu hawakubali kushindwa. Hasa watoto wa kwanza hujiona wao ni sehemu ya wazazi hivyo ku exercise ukubwa kwa wadogo zao wakati wote ni watoto hukutana na upinzani mkali sana. Matokeo yake ni ngumi za hapa na pale na bila uangalizi huishia kuumizana vibaya.

Sometimes sababu ni za ujinga tu unakuta wanagombania kitu tu. The best way ni kumfundisha mkubwa ku give in kumuachia mdogo wake kwa upendo. Itakuwa inamuuma ila atazoea kuwa kumpa priority mdogo wake ni swala la upendo na sio unyonge.
Hapa umesema vyema kabisa.

Binafsi nimebarikiwa watoto wawili.Wakike na wakiumeWamepishana miaka minne.

Hawa vijana usije home na kitu kimoja au vinavyotofautiana. kama baiskel babà ni mbili.Hata kama ni toys baba ni mbili nunua zinazofanana.Lasivyo watagombana sana.
Nikagundua mdogo yeye anahisi anahaki ya kila kitu sababu anakimbilia sana kusemea.mkubwa yeye anaona ana mamlaka ya kufanya kila kitu .Nikajifunza kumpa vitu mdogo ampe mkubwa na mkubwa awe anamuona mdogo kama mtoto ilizaa matunda sana,
 
Kwa hiyo ukarudi ukamkuta dogo kanyamaza ila kisu bado kipo jichoni anazunguka nacho kama sio yeye eti?

Na mama nae anapika vitafunio aende kuzungusha
Acha nimalizie story na uthubutu kunikosoa hapo
 
Kaka hii dunia sio mbaya sana kama unavyosema. nikuulize swali?

Kipi bora kuwanunulia pipi hao watoto ukawapatanisha wakaharisha alafu ukapelekwa polisi na mama Yao au
Watoto kuchomana visu?
Swali hilo hilo, kipi bora kwa mama, watoto waadhibiwe kidogo kwa makonzi au waachwe wachomane visu wauane kama alivyosema?
 
Hawa jamaa Wa valeur na kitimoto wanamambo ya hovyo sana. Yani watoto wanauwana wewe unafua jeans zako. Wewe jamaa roho mbaya sana.
Lakini si aliambiwa na mama wa watoto kwamba hata akikuta wanauana asijaribu kuwaamulia au kuwapiga? Tujisahihishe wazazi!
 
Back
Top Bottom