Napenda sana majirani wa aina hii

Naweza kusema bila shaka kuwa kwa ulichokiandika (kama ni kweli) basi wewe huna akili na huyo mama mwenye watoto hana akili, yaani mmekutana mazoba. Kwa nini? Watoto wanafundishwa kwa kuwaonyesha upendo. Yaani wakipigana wewe badala ya kumpiga mmoja, unatakiwa uwafundishe jinsi ya kuishi kwa upendo. Kuwapiga inawafanya nao wazidi kuwa wagomvi kwa sababu ni kama unawafundisha ugomvi huamuliwa kwa ugomvi na wanakuwa wanawekekeana visasi muda wote. Kingine, hao wote walikupa ''likes'' nao ni wajinga.
 
Hivi hakuna njia nzuri zaidi ya kufundisha mtoto bila kumpiga? Unaonaje ungewaelimisha kwa upendo? Huoni kuwa wangekuona ni maana na kukuheshimu?
 
Kwenye malezi katika rika la utoto kupigwa au kuadhibiwa hakukwepeki ni muhimu sana kumkanya mtoto mtukutu na kipigo kinyume chake unatengeneza bomu kubwa sana Mimi ni mzazi na mlezi najua ninachokifanya

Labda kama hujawahi kulea ndo huwezi kuelewa hili jambo
Hivi hakuna njia nzuri zaidi ya kufundisha mtoto bila kumpiga? Unaonaje ungewaelimisha kwa upendo? Huoni kuwa wangekuona ni maana na kukuheshimu?
 
Kwa taarifa yako mimi nimeishi kwenye nchi ambazo watoto hawachapwi na ukimchapa mtoto ni kosa la jinai na watoto wa hizo nchi ukubwani wanakuwa na akili na adabu kuliko hao wewe unaowatandika bakora. Kama wewe ni mzazi na unatandika watoto wako ukidhani ndiyo watakuwa na tabia njema basi unajidanganya. Huwezi kujiuliza kwa nini huku kwetu tunachapa watoto lakini ukubwani wanapofanya kazi wanakuwa madaktari makatili. viongozi mafisadi, wanafunzi machangudoa, vijana waporaji na kila aiana ya unyama ambao sehemu ambazo hawachapi watoto huwezi kuona?
 
Boss mzma wewe
Samahani ivi mzazi wako ndio akiwa anataka kujipiga kitanzi watu wakamwona akawaambia niacheni utapenda wamwache au wamdhibiti asijipige kitanzi
 
Mtoa mada kwenye jicho kazidisha chumvi sana[emoji23][emoji23]..ila kama ni single maza sishangai maana wana malezi ya kipuuzi sana!
 
Umezingua sana , umekosea sana utakuja kuelewa siku za mbele.
 
Oya Babu! we endelea na hizo nchi zako lakini sisi ni wabantu na hizi taratibu ndiyo zinazoufanya jamii yetu leo kuwa bora na ngangali kiustawi wa jamii

Hakuna jamii zenye ustawi mzuri kama za afrika na Asia hata wazungu wenyewe wanathibisha hilo wanatamani sana makuzi ya huku

Wewe kama umevutiwa na ustaarabu wa huko huo ni mpango wako hakuna anayekuzuia na sisi tuache na taratibu zetu halafu mwisho wa siku kila mtu avune alichopanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…