Hii story yako imenikumbusha mbali, unajua wadada tumekuwa na shahuku ya ndoa sasa inakera sana,hayo yote analazimisha ndoa. Kuna Shoga yangu alimbambikizia mwanaume mtoto nikambembeleza hatopata amani akagoma, akalazimisha huyo Mme akamuoa, ukawa ni mwendo wa kunitumia picha za harusi kama vile ananiringishia kaolewa.ikabidi nipunguze urafiki maana kweli yule mtoto sio wa Mme wa ndoa.
Baada ya miezi sita vurugu na visanga vikaanza ndoa si ndoa nikamshauri atubu kwa Mme wake akagoma nikakaa pembeni. Nachoamini ile ndoa haiwezi fika popote.uongo ni dhambi kubwa.
Nachoamini hakuna mapenzi bila amani.yawezekana anataka child support ila katumia njia ya kishamba sana, sijui mlikutana wap maana hizo ghasia anazowaletea wazazi wako sidhani kama hata shule kichwani mwake anayo.
Sasa wewe punguza stress ongea na ndugu zako huyo mwanamke block, maana utashindwa kufanya kazi zako. Kata mawasiliano kwa sasa mpaka utakaporudi. Mwende hospital mkapime DNA
Hawezi leta vurugu zaid ya miezi 6, atafika mwisho aache Kuhusu kuwaletea vurugu ndugu zako, waambie akileta vurugu wapeleke police embu jifanye kama humjui tuone nn kitatokea.
Huwezi lazimisha mwanaume akupende kwa kumtafutia vikwazo.sikio halizidi kichwa.