Nimesema hivyo kwasababu mimi ni mwanamke, ni mama wa watoto wawili, nina marafiki wa kiume nina kaka zangu, jamani tatizo la roho mbaya za wanawake limenizidi kukua siku baada ya siku, wanaofanya hivyo ni wanawake wenzangu wengine ni wazuri wanajistiri ukiwaona kama wastaarabu lakini vitendo vyao vinaogofya.
Ndio maana nikasema angalau kwenye uoaji wenu wanaume kitu cha kwanza kukiangalia kingekuwa Utu wa unayemuoa. Mavazi na tabia sidhani kama yanamsingi sana, na wasichana wengi wasiojistiri ni kwasababu tu hawajaolewa au hawajapata wakuwaoa, sifikirii kama kuna msichana leo hii ukamwambia nataka kukuoa bado aendelee kuvaa vibaya.
Kuna vitu vinabadilika vingine havibadiliki asilani.