Kwani uchunguzi ukifanyika kuna shida gani. Kukitokea tabia ya uuaji tunanyamaza ni kujenga utamaduni mbaya ktk Taifa. Mengi alikuwa mtu binafsi, ambaye familia yake ndo inahusika zaidi. Hata weye ungekuwa kiongozi wa nchi tungechunguza. Rais anabeba uhusika wa kitaifa.
Na watu wanao husika na mauaji, lazima wachukuliwe hatua za kisheria.
Maandiko matakatifu yanaeleza Kaini alimuuwa nduguye, japo nduguye tayari alikuwa kafa, lakini bado Mungu alimlaani Kaini. Na Mungu alimhoji kaini kwanini kamuuwa Habeli. Hivyo kuuwa si swala halali ati kwa kuwa tu mtu kafa, basi tuache.
Ingekuwa hivyo hatungehitaji sheria za kifungo cha maisha au kunyongwa kwa wale wanao uwa. Ati kwasababu alie uwawa hayupo tena na hajui chochote.
Ingekuwa hivyo unavyodai wewe, mauaji yaliyozuka ya albino tungeacha tu yaendelee yasikomeshwe kisa wanao uwawa hawajui tena kitu.
Uchunguzi ni kuleta haki ifanyike kwa mujibu wa sheria. Si kumfurahisha marehemu, bali kuzuia uharifu zaidi. Na kutoa adhabu kwa waliotenda.