Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Unadhani watakaomuua amiri jeshi ni wajinga wajinga wasio na mafunzo ya kijeshi? Jeshi halikwepeki kukitokea mauaji ya amiri jeshi, na uchunguzi ni jeshi. Ipe majina unayotaka ww sijui tume, sijui kikoba lakini uchunguzi lazima uwe wa kijasusi.
 
moja ya sita ya madkatari ndio waaminifu wengine hakuna kitu kama kuna fungu natekeleza unachotaka tu. Hata hivyo, maoni ya daktari sio ushahidi wa mwisho kisheria anaweza kuhojia pia kwa kuwa ni binadamu na utashi wake
 
Tatizo lenu amkujiandaa na njia mbadala ya kuishi nje ya kusafisha mikojo leo sio dili tena.limeni hata michicha maisha yaende.
 
Labda ufanywe na wanufaika but wengine tuna heshimu maamuzi ya Mwenyezi Mungu baada ya kusikia maombi ya wengi.
Ok, amefariki ulichofaidika nini? Unadhani wewe huto kufa? Mch. Mtikila alikejeri sana kifo cha Nyerere lkn yeye akafa tena kifo kibaya tu.
Hivyo jitafakari kifo chako kitakuwaje? Cha mateso au? Na je unadhani utaishi milele! Tuache kashfa.
 
Endelea kusubiri kama unategemea mama kuja kupiga kampeni chumbani kwako!!! Sisi wananchi wapiga kura tunamuelewa sana na tunasema mama mitano, mitano na mitano tena, ikiwezekana maisha kabisa.
Mama milele
 
Ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Bora fedha hizo za hiyo kamati na bajeti yake ijengwe zahanati
 
Unadhani watakaomuua amiri jeshi ni wajinga wajinga wasio na mafunzo ya kijeshi? Jeshi halikwepeki kukitokea mauaji ya amiri jeshi, na uchunguzi ni jeshi. Ipe majina unayotaka ww sijui tume, sijui kikoba lakini uchunguzi lazima uwe wa kijasusi.
Ok, ndo tunataka kama aliuwawa na jeshi ijulikane. Iundwe tume. Ili kila kitu kijulikane. Porojo nyingi haziwezi saidia. Jeshi aliwezi ogopeka. hata wao ni binadamu, na wanachunguzwa. Kama jama zipo watajibu.
Fatilia mauaji ya alie kuwa Rais wa Bukinafaso, Sankara.
Aliuwawa na Mtu wake wa karibu, na baadhi ya waasi. Imepita miaka zaid ya thelathini. Rais aliekuwepo madarakani alie muuwa Sankara, aligoma uchunguzi usifanyike. Lakini baada ya kutoka madarakani, alishitakiwa na kuwekwa hatiani kwa mauwaji ya Rais Sankara zaidi ya miaka 37 iliyopita.
Leo mtapinga, lakini ipo siku haijarishi. Hata kama kuna watu jeshini waliusika ipo siku, itajulikana ukweli.
 
Kwani Gwajima na mautundu yake ya kufufua wafu alishindwaje kumfufua,huyu naye lazima ahojiwe atakuwa anahusika ndiyo maana kauchuna.
 
Kwani uchunguzi ukifanyika kuna shida gani. Kukitokea tabia ya uuaji tunanyamaza ni kujenga utamaduni mbaya ktk Taifa. Mengi alikuwa mtu binafsi, ambaye familia yake ndo inahusika zaidi. Hata weye ungekuwa kiongozi wa nchi tungechunguza. Rais anabeba uhusika wa kitaifa.
Na watu wanao husika na mauaji, lazima wachukuliwe hatua za kisheria.
Maandiko matakatifu yanaeleza Kaini alimuuwa nduguye, japo nduguye tayari alikuwa kafa, lakini bado Mungu alimlaani Kaini. Na Mungu alimhoji kaini kwanini kamuuwa Habeli. Hivyo kuuwa si swala halali ati kwa kuwa tu mtu kafa, basi tuache.
Ingekuwa hivyo hatungehitaji sheria za kifungo cha maisha au kunyongwa kwa wale wanao uwa. Ati kwasababu alie uwawa hayupo tena na hajui chochote.
Ingekuwa hivyo unavyodai wewe, mauaji yaliyozuka ya albino tungeacha tu yaendelee yasikomeshwe kisa wanao uwawa hawajui tena kitu.
Uchunguzi ni kuleta haki ifanyike kwa mujibu wa sheria. Si kumfurahisha marehemu, bali kuzuia uharifu zaidi. Na kutoa adhabu kwa waliotenda.
 
🤣🤣
Tuishie hapa boss, nimeshaelewa nazungumza na mtu wa aina gani.
Ok, nami nimeelewa toka mwanzo ni watu wanamna gani wanao pinga uchunguzi kwa visingizio vya nafsi zao. Nikakumbuka usemi wa wahenga. "Mbaazi akikoswa maua usingizia jua". Asante!
 
Hayati JPM alisumbuliwa na moyo tangu akiwa waziri, na miaka ile alishakwenda nje kutibiwa.

Mama Samia pale bungeni aliweka wazi kama kuna mtu anazo taarifa za kifo chake kwa mapana na azifuate mamlaka ili aweze kupewa ushirikiano.

Mambo mengine yatakuumiza tu ukiyachukulia kwa undani. Huyo JPM mwenyewe anazo tuhuma za kuhusika kwenye vile vifo vya wale watu waliokuwa wanaokotwa miili yao kule Coco Beach, nani aliyewatetea wale marehemu?.

Kuna tuhuma za JPM kuhusika na upoteaji wa Ben Saanane, nani aliyeilazimisha ofisi ya rais au wasaidizi wake juu ya umuhimu wa kupeleleza kuhusu kifo cha Ben?.

Kuna suala la RIP Mkapa kudaiwa kutuma watu wakamuua Kombe aliyekuwa usalama wa taifa, nani aliyemhoji Hayati Ben kuhusu kifo kile mpaka siku yeye mwenyewe alipoaga dunia?.

Hatuna utamaduni huo wa kuhoji vifo vya wakubwa wa nchi, Alikufa Edward Sokoine kwa ajali ya gari akiwa njiani kutoka Dodoma, nani aliyewahoji wote waliokuwa wakitajwa kuhusika na kifo kile?.

Ishi maisha yako pasipo kujitafutia masumbuko yasiyoweza kuongeza chochote kwako.
 
Imagination imagination imagination
Nashkuru kwa maandishi yako mkuu. SIKU njema.
Unapayuka mtandaoni, tukikuita uthibitishe utaweza!? Acha kuichongamisha serikali na wananchi wake, ukiendelea itakugharimu.
[emoji28]Nikikujibu ipasavyo ntakosea. Usikome kunitisha lakina. SIKU njema
 
Mimi siamini kuishi kwa hadithi, siamini kuishi kwa kuiga ati tu fulani hakufanya hivi basi tusifanye. Nchi ina uhai na wananchi ndiyo weye uhai. Mabadiliko hutokea. Hatuwezi ishi kwa hadithi ati mbona hiki kilitokea tuendelee hivyo hivyo. La hasha!
Unadai Magufuli kuuwa ati maiti waliokutwa kwenye viroba. Na kumuuwa Ben Saanane. Hivi Chama husika Ben alikuwa msaidizi wa Mbowe. Kwanini Mbowe hakwenda kutoa taarifa polisi kuhusu hayo mauaji kwa kuwa alikuwa na ushahidi. Hivi mtu wako wa karibu auwawe, na unajua nani kamuuwa, unashindwa kweli kuchukua hatua?

Hivi vyote ulivyovisema watu waliokuwa na uhakika wange fungua hata kesi ambazo ni private prosecution.
Hayo yote hayaondoi uhalali wa kuundwa tume ya kuchunguza kifo cha Rais.
Kila kitu kina namna yake na uja wakati muafaka. Marekani kumekuwa na mauaji ya watu weusi. Ikazoeleka. Mhakama zilitoa haki kwa polisi.

Lakini mauaji ya George Floyd yaligeuza kila kitu. Dunia nzima iliungana. Hata wakati wa kutoa maamuzi dhidi ya mtuhumiwa, yalitazama hasira za wananchi. Hatimae kwa mara ya kwanza mambo yalibadilika na huyu Askari kukutwa na makosa ya kuuwa kwa kukusudia.
Pamoja na hayo yote uliyoongea, ipo siku mabadiliko yanakuja Tanzania kuchunguza kunapotokea vifo vya utata vya viongozi wa Taifa.
Pia kwa taarifa yako, haya ndo maisha yangu. Nimezaliwa duniani kwa lengo maalum si kuishi tu kama unavyodhani. Hivyo si masumbuko kwangu bali ndo natimiza nilichoumbiwa kuja hapa duniani.
 
Ameshakufa na tumemsahau
 
Kifo cha mkapa sio muhimu? Tuache ujinga kifo kipo tu ndugu zako waliotangulia umefanya uchunguzi ?acha ukenge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…