Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

ipo hivi mkuu, alipokufa sokoine palizuka minong'ono. tume haikuundwa

akafa nyerere, palizuka vimaneno, tume haikuundwa.

aalikufa dr ali juma, palizuka maneno tume haikuundwa..

akafariki mkapa, maneno yakawepo, hakuna tume iliundwa...

kafariki magufuli, unataka tume iundwe. upo sahihi lakn why iwe kwa huyu tu bila kuanza kwa hawa wengine waliomtangulia? au at least yeye magu angeunda tume kuchunguz vifo vya watangulizi wake au waliofariki wakt wa awamu yake, lakn hata yy hakuunda.

why unalazimisha kwa huyu mama?

njoo tufagie barabra mkuu, huyu mama hana kundi atakalo lilipa kwa kusifia au kumsifia. kazi zake zitajiuza zenyewe..
 
Vifo vya Nyerere na Mkapa havikuchunguzwa huyo JPM alikuwa na utakatifu upi wa kipekee?.

Nyerere alifia hospitalini Uingereza kama kuuwawa yeye angekuwa wa kwanza.

Narudia kukwambia, ondokana na dhana nyingi kichwani mwako hazikusaidii.
 
Tume Ikiundwa Mtasema imepangiwa cha kusema...Nyie watu hamuaminiki...na Wala hamuani kama sisi ni wanadamu siku zetu huisha.
 
Kwani kiongozi wa kanisa LA uzima na ufufuko anasemaje?
 
Hata uchunguzi ukifanyika na ripoti ikitoka Bado itaonekana Ni ripoti ya kupika.kwa kua mwendazake kaenda zake acha maisha mengine yaendelee
 
Vifo vya Nyerere na Mkapa havikuchunguzwa huyo JPM alikuwa na utakatifu upi wa kipekee?.

Nyerere alifia hospitalini Uingereza kama kuuwawa yeye angekuwa wa kwanza.

Narudia kukwambia, ondokana na dhana nyingi kichwani mwako hazikusaidii.
Kifo cha Nyerere au Mkapa hakiondoi haki ya kifo cha Magufuli kuchunguzwa. Kila zama na kitabu chake.
Weye ndo ondoa dhana ulizokaririshwa kuwa kwakua kifo cha Nyerere na mkapa havikuchunguzwa basi na vijavyo visichunguzwe.
Inaonesha unaishi kwa nadharia. Badili fikra zako usishiliwe akiri kwa sababu ya ushabiki na kutojiamini. Kinachokuuma ni nini kifo cha Magufuli kikichunguzwa?
Nakwambia ipo siku inakuja. Yote watakuwa wazi. Mambo ubadilika, hatuishi kwa hadithi!
Mabadiliko yanakuja yapo njiani.
 
Acheni Mambo ya hivi , kiongozi alishasema , pamoja na siku zake kufika Kama mwanadam yeyote bado sababu ya kifo chake ilishatolewa,
Na bado mmepewa nafsi KWa yeyote Alie na mashaka na anaushahidi na chanzo kingine Cha kifo tofauti na mlichoambiwa anjongee CHAMWINO atapewa ushirikiano,
Mengine itakua kumkufukuru mungu maana siku za mwanadam zikifika za kuishi duniani lazima ufe tu
 
Mkuu hiyo siku haipo. Kama walivyokufa waliomtangulia JPM na kusahaulika na kwake itakuwa hivyo hivyo.

Hakuna lolote litakalokuja kutokea kesho wala miaka kumi ijayo.

Futa kabisa mawazo ya aina hiyo kichwani mwako.
 
Vifo vya Nyerere na Mkapa havikuchunguzwa huyo JPM alikuwa na utakatifu upi wa kipekee?.

Nyerere alifia hospitalini Uingereza kama kuuwawa yeye angekuwa wa kwanza.

Narudia kukwambia, ondokana na dhana nyingi kichwani mwako hazikusaidii.
Kifo cha Nyerere au Mkapa hakiondoi haki ya kifo cha Magufuli kuchunguzwa. Kila zama na kitabu chake.
Weye ndo ondoa dhana ulizokaririshwa kuwa kwakua kifo cha Nyerere na mkapa havikuchunguzwa basi na vijavyo visichunguzwe.
Inaonesha unaishi kwa nadharia. Badili fikra zako usishiliwe akiri kwa sababu ya ushabiki na kutojiamini. Kinachokuuma ni nini kifo cha Magufuli kikichunguzwa?
Nakwambia ipo siku inakuja. Yote watakuwa wazi. Mambo ubadilika, hatuishi kwa hadithi!
Mabadiliko yanakuja yapo njiani.
Mkuu hiyo siku haipo. Kama walivyokufa waliomtangulia JPM na kusahaulika na kwake itakuwa hivyo hivyo.

Hakuna lolote litakalokuja kutokea kesho wala miaka kumi ijayo.

Futa kabisa mawazo ya aina hiyo kichwani mwako.
Ha ha ha, sifuti kitu. Inakuja hiyo siku. Ni ngumu kuamini. Lakini inakuja. Tunza maneno haya. Haya maneno hayako kichwani bali yapo katika nafsi na roho. Yanaishi.
 
JPM ameshalala usingizi wa milele hakuna hata mmoja utakayemsikia akianzisha uchunguzi wa kifo kinachojulikana chanzo chake ni kipi.
 
Kila masika na chura wake. Urithi haufi. Mwaminifu hafariki isipokwa amezaliwa mwaminifu mwingine. Tumuache apumzike!
 
Kila nafsi hai itaonja mauti, that was a natural death, acheni kutufarakanisha tuchape kazi kwa salamu ya jamhuri ya muungano, mnaoleta hypothesis chonganishi acheni.
 
Watu watajipa moyo kuwa yatapita, lakini nasema ipo siku. yaweza isiwe leo lakini ipo siku. Nayo inakuja!
Kama walikufa kina Nyerere walioanzisha Tanzania wanaitwa Baba wa Taifa na hatukusikia uchunguzi mpaka leo kuanzia 1999 hili suala la kifo cha JPM ndio sahau mapema kabisa.
 
Jinsi alivyokuwa akilindwa vile usiku na mchana ingewekaje kuuawa?

Huenda ndiye rais wa kwanza kulindwa kwa gharama kubwa sana na misafara mikubwa kuliko marais wote tangu Uhuru!
 
Kama walikufa kina Nyerere walioanzisha Tanzania wanaitwa Baba wa Taifa na hatukusikia uchunguzi mpaka leo kuanzia 1999 hili suala la kifo cha JPM ndio sahau mapema kabisa.
weye naona umekaririshwa. Ongea mengine. Hilo la Nyerere ulishalisemea. Kifo cha Nyerere siyo msingi wa kifo cha Magufuli kutochunguzwa. Kila jambo lina mwisho wake.
 
Tumuogope Mungu sana!

Saingine kuzania zania siyo vizuri tusijetufanya dhambi kubwa unless uwe na sababu za msingi za madai yako na uwe tayari kuyathibitisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…